Inaonyesha maana ya "eneo la bondeni au maeneo ya bondeni haijaeleweka" kabisa. Sera ya mazingira ya 1998 na sheria ya mazingira ya mwaka 2004 zinasema hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya 60m kuzunguka au kwenye kingo za vyanzo vya maji. Na vyanzo hivyo vimeaninishwa kuwa ni; bahari, ziwa, mto, kijito, chemchemi ,bwawa, na eneo chepechepe (oevu).