Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,282
Wanabodi,
Declaration of interest:
1.Mimi Paskali sio mwanachama wa Chadema ila ni kada wa chama cha siasa.
2.Mimi ni binadamu na mtu kutokea Kanda ya Ziwa, ambao wengi wetu tuna madhaifu na type fulani ya watu, hivyo naomba kukiri kuwa Wema ninampenda na kumkubali sana hata wife wangu hilo alinajua, hivyo maoni yangu kwenye bandiko hilo sio chuki binafsi na wala sio wivu kwa vile namzimikia Wema, au naona wivu wa jinsi anavyotokelezea na Mbowe, na jinsi wanapendezea kwa ukaribu huo, hivyo isije tafsiriwa namuonea wivu!.
Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, lakini hawakomi na wala hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!
.
Mwigizaji Wema Sepetu, Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni miongoni mwa waliojitokeza kuhudhuria mechi ya Simba vs Yanga kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam leo February 25 2017.
Mwigizaji Wema Sepetu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe baada ya kushuka kwenye gari wakiwa wanaingia uwanjani.
Kwa Maoni Yangu...
Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna any credible serious opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu, unless watu wachoke mpaka basi na kuamua liwalo na liwe, hata kama ni kufanya majaribio ya kuijaribishia tuu Ikulu, bora tujaribishe tuu hivyo hivyo! .
Paskali.

Sasa kama Chadema ndio chama tegemewa na usajili wenyewe ndio kama huu wa Warembo, Wanyange, Walimbwende wasio na msimamo kama Wema, unategemea nini kwa 2020?!.Nimeona baadhi ya viongozi, wanachama na washabiki wa Chadema, wakifurahia ujio wa mlimbwende Wema Sepetu kujiunga Chadema as if Chadema wamelamba dume, kiukweli Chadema wamelamba garasa, an empty shell kwa sababu mrembo huyu hanaga msimamo hata mara moja, kuanzia kwenye choice of friends na love life yake, has never been stable and settled, hivyo kujiunga kwake Chadema ni hasira tuu za kutuhumiwa bila CCM kuonyesha kumsaidia, hivyo anahama CCM, ili kuwakomoa na kujiunga Chadema ili tuu kuwaringishia CCM, but she has no value at all to add to Chadema, kwa sababu hasira zitaisha, na atarejea CCM!, just time will tell!.
Haki ya Wema Kujiunga Chama Chochote, ila The Timing ni Wrong Timing.
Wema Sepetu, kama Mtanzania mwingine yeyote, anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa kwa sababu zozote, au bila sababu zozote kwa mapenzi yake, sambamba na haki ya kujitoa chama chochote kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote, ila timing ya kujitoa chama fulani, na timing ya kujiunga chama fulani ni muhimu sana, kwa maoni yangu, hii timing aliyoitumia kujitoa CCM na kujiunga Chadema, is a wrong timing!, hata kama aliipenda Chadema siku nyingi tuu na alipanga kujiunga nayo, kujitoa CCM baada ya kulazwa selo wiki moja, kunatafsiriwa ni amejitoa kwa hasira baada ya kutetea CCM na kutesekea, malipo yake ndio haya, hivyo kwa hasira ameamua kujitoa, na kujiunga Chadema ili kuwakomoa CCM na kuwaringishia. It is a wrong timing, kwa sababu, Wema bado ana kesi mahakamani, usishindane na mwenye nguvu!, ungejua Godbless Lema hana kosa lolote zaidi ya kuisema tuu ndoto aliooteshwa, lakini kwa vile alipishana na Gambo, akamtunishia msuli, saa hizi yuko wapi?. Msije shangaa mtoto wa watu akafutiwa dhamana, au akazushiwa chochote na kupigwa mvua, Chadema haiwezi kumsaidia lolote!. Angesubiri yaishe kwa amani, kisha akajitimkia zake kwa uhakika, haya mambo, hayahitaji hasira.
Haki ya Chadema Kupokea Mwanachama Yoyote, Tatizo ni Umuhimu/Ukaribu Mkubwa
Mchungaji Mwema huwaacha kondoo wake 99 akaenda kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea, na hata mbiguni, huwa ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu, vivyo hivyo Chadema kina haki ya kufurahi kila kinapovuna mwanachama mmoja, nikimaanisha CCM inazidi kubomoka na kukimbiwa, na Chadema inazidi kujengeka kwa kuongeza. Pia Chadema kama chama cha siasa, kina haki ya kumpokea mwanachama yoyote kutoka popote, tatizo langu ni attention kubwa aliyopewa Wema, siku ya kwanza juzi pale Mahakama ya Kisutu, Wema ndio akae next to Mwenyekiti?!, hata Mdee, Bulaya na viongozi wengine walipunguzwa umuhimu, baada ya Mwenyekiti, Wema!. Leo mpirani kwenye mechi ya Simba na Yanga, Wema ametinga gari moja na Mwenyekiti!. Kweli Wema ni Super Star, ila kichama ni mwanachama tuu wa kawaida kama mwanachama mwingine yoyote, asionekane anapapatikiwa sana, ananyenyekewa sana, mtu kajiunga na Chadema jana tuu, leo anashuka gari moja na Mwenyekiti!, its too much of a VIP treatment, kesho atawaaibisha atakaporejea nyumbani CCM!.
Wema ni Asset or Liability? .
Wema ni mtaji, kibiashara tunaita ni asset kwa sababu hakuna ubishi kuwa Wema ni super star, Wema ni maarufu, Wema ana followers zaidi ya milioni 2 ambao kama kweli hawa wote watamfuata Wema Chadema, then Chadema itakuwa imepata mtaji mkubwa.
Wema Ni Faida Kidogo na Hasara Kubwa Hivyo ni Liability.
Pamoja na ukweli kuwa Wema ni asset, sio fixed asset, hii ni movable asset, current asset na liquid asset ambayo mtaji unahamishika, unaotumika na kuweza kuyeyuka wakati wowote.
Kwa Nini Wema ni A Liability?.
Mfano wa Gari Bovu.
Gari likiwa jipya linakuwa na thamani kubwa katokana na upya wake hivyo unaweza kulifanyia biashara likakuingizia faida hivyo utaliita mtaji. Lakini gari likiwa limechakaa na kuanza kuchoka, ukilinunua linaweza kukuingizia faida kidogo lakini running costs na maintainance cost zikawa kubwa na kumeza faida yote, hivyo kujikuta unafanya biashara ya hasara au biashara kichaa.
Ni Biashara Kichaa
Wema ndani ya Chadema ni biashara kichaa. Whoever aliyetoa fungu kumnunua Wema akijua amewekeza kwenye biashara ya faida, kiukweli kwa sasa Wema ni biashara kichaa.
Wema ni Jina Tuu, Muuza Sura, au Muuza...?!, Je Chadema ina Wanunuzi?!.
Hii ni kufuatia Wema Sepetu amebaki jina tuu na kuuza sura, au kuuza..., kwa sababu kwa sasa, Wema hana shughuli nyingine yoyote ya maana anayoifanya inayomuingizia kipato cha kuendesha maisha yake zaidi ya kuuza sura na zile huduma zetu zile!, Jee Chadema inao wanunuzi wa huduma hizo kwa kwa dau la Wema?.
Kwa sasa Wema hana movie, haimbi, hana ofisi, na hana mtu, hivyo alijiunga CCM akitegemea kukwaa viti maalum kama walibwende wenzake, Vicky, Juliana, Lucy, Catherine na wengine ila CCM walingundua siku nyingi kuwa upstairs yuko totally empty wakamtosa! ,hata hivyo aliendelea kuikumbatia CCM kwa ajili tuu ya kuvuta fungu nene in an exchange ya zile "huduma" kwa baadhi ya watu, haswa kwa uzuri ule, urembo ule na weupe ule, ambao ni ugonjwa wa watu wa kanda fulani akitegemea "yule jamaa mwenyewe" ndie angefika bei!,lakini "wale jamaa" walikuwa makini maana kila apitaye kwa Wema ni matangazo, hivyo jamaa akipita na matangazo yangefuatia ingekuwaje?!. (kama kumezea mate, kiukweli msema kweli mpenzi wa Mungu, hata mimi!, hebu jifikirie hata ungekuwa wewe?), hivyo akadondokea kwa yule Msukuma mwenye kisu kikali akamtuliza kipindi chote cha kampeni. Baada ya ushindi kazi yake ikaisha akatemwa!.
Thamani ya Wema ni Nini na Lini? .
Thamani ya Wema ni mtaji wa followers milioni 2 kwenye team Wema. Jee mtaji huu unafaida gani wakati wa kipindi hiki?. Kwa maoni yangu, thamani ya Wema ni kwenye uchaguzi tuu, kwa vile uchaguzi wa 2020 bado ni mbali, maintainance cost kumeintain Wema mpaka kipindi hicho zitakuwa too much kwa Chadema ku afford, ni CCM pekee ndio wenye fedha za mchezo unless wanaChadema individually wenye kisu kikali kama Mbowe, au 'Mzee Wetu' waamue kumshika mkono chini ya himaya zao, kwa mujibu wa zilepicha zile za mahakamani, kiukweli walipendezea, ila...tatizo waliopo watakubali?!.
Nini Kitatokea Kwa Wema Chadema? .
Kusipotokea sponsor wa kugharimia maitainence ya Wema, then kitakacho fuata ni kile kile kilichotokea kwa Nakaaya Sumari, Jackline Wolper, Anti Ezekiel na wengine wanaojiunga na vyama vya siasa sio kwa mapenzi ya vyama hivyo bali as a means ya kuendeshea maisha yao, wakigundua tuu kuwa Chadema ni juani, na CCM ndio kivulini, soon wataungua na jua kali na kujirudia zao kivulini.
Hivyo naomba sana wana Chadema, msije kushangaa soon ikaitishwa press conference nyingine Wema akaomba msamaha na kudai ni hasira tuu za kulazwa selo, hivyo ni shetani tuu alimpitia na kuhama CCM, hivyo ataomba asamehewe na atapokelewa na Ngosha mwenyewe kurejea CCM! .