Ujio wa Makonda na Utakaso wa Nape.Katika kuchanga Karata mmoja alilamba Dume mwingine Galasa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,314
moja ya tatizo kubwa nililo nalo na siku zote huwa nasikitika ni tatizo la kutokusahau. ila ukitaka uwe mwanasiasa mzuri inabidi uwe msahaulifu. nimekaa nikakumbuka nape ambaye leo anaonekana shujaa ndo huyu aliyekuwa akipita tanzania nzima akiwatukana wapinzani na mwishoni alitoa ile kauli ya "CCM ITASHINDA HATA KWA BAO LA MKONO" Ikashinda.

lakini huyu ni mtu ambaye katika sakata hili la ujio wa makonda au makonda era ameonekana kuwa ni mtu mwema kwa wale wenzangu wangesema hili ni Jini Rafiki. Makonda amewekwa kwenye kundi la majini wabaya na nape amekuwa kwenye jini ambalo linaonekana ni zuri.

lakini ukiangalia siasa utagundua kuna tatizo kati ya makonda na nape.na hili tatizo lao ndilo linalosababisha nape awe hivi alivyo. huyu huyu nape ambaye leo anaonekana ni mtu mwema alikuwa ni mmoja ya watu wenye maneno mabaya sana kwa wapinzani kipindi cha utawala wa kikwete. huyu nape ndye aliyekuwa akiwashughulikia wana CCM wenzake ambao walikuwa wanaonekana kuwa na fikra za kimapinduzi ndani ya chama. akiwaita wapinzani ndani ya ccm.

bahati mbaya kwa awamu hii hakupata kupakatwa kama ilivyokuwa awamu iliyopita ambayo ilimbeba sababu ya ugomvi wake na lowassa. ni wazi kuwa nape aliibuka sana awamu iliyopita mara baada ya kuanza kufanyika juhudi za kumzima lowassa baada ya kuwa amejiuzulu kwa kashfa ya richmond. nape huyu wa sasa si nape wa miaka ile ambayo naye alikuwa akipakakatwa na babaye na kupetiwa petiwa mgongoni. nafasi ilealiyokuwa nayo imechukuliwa na makonda katika awamu hii. hivyo nape amegeuka kuwa mpinzani wa makonda kwa sababu ya tofaut zao za kisiasa ndani ya chama. si kweli kuwa nape amekuwa mtu mwema. huyu ambaye ni mapema tu alipitisha miswada mibaya ya kuwabana waandishi na kuzuia bunge kuwa live.

tabia mbaya za wanasiasa wamekuwa wanapogombana wao kwa wao ugomvi wao huufanya kuwa ni public. huamua kutafuta ushawishi toka kwa wananchi na wananchi bila kujua au kwa kujua lakini kwa kupoteza umakini hujikuta wameingia kwenye ugomvi huo.

makonda amekuwa na tabia ya kujipendekeza sana kwa wakubwa zake. tunakumbuka katika suala la bunge la katiba na alivyotumika mpaka kuharibu mkutano wa mzee warioba na polepole akiwepo. huyu kijana alijipatia ujira wake akatimiza lengo lake na akaja kupewa zawadi ya ukuu wa wilaya. tukumbuke huyu pia alitumika sana na wapinzani wa lowassa kipindi kile kumtukana lowassa katika vyombo vya habari. miaka hiyo akitumika na samweli sitta. mpaka alipokuja kuwa mtumikaji wa kikwete na ridhiwani.

kama ana degree basi aliipata katika taaluma ya kujipendekeza sana kwa wakubwa.bahati mbaya sana mwanasiasa mmoja mtu mzima siku kadhaa zilizopita alikuja humu ndani akatapika mavyakula yake kuwa vijana wana mengi ya kujifunza toka kwa makonda. nadhani naye alikuwa akitaka aonekane kuwa yupo upande wake maana wanajua kwa sasa kama ukimpendeza makonda umempendeza baba yake.

kuweni makini na nape si kwamba sasa akili yake imefunguka. hapana ni vita tu vya kisiasa baada ya mwenzake kuwa amelamba dume yeye akalamba garasa. lakini siku zake zikifika mtamiminika humu pia kumponda kwa maneno mabaya mabaya. swali. alishaomba msamaha kwa kutufunga goal la kono lililopelekea majanga haya?

waacheni waparurane. ndugu wakigombana chukua jembe ukalime after all haya wameyaleta ketu wakidhan wao wangekuwa salama. wakasahau
"mchuma janga hula na wakwao "
 
You have a point ndugu GuDume. Kuna msemo wa busara unasema "Unapoandaa kitanda cha kokoto kwa mwenzako kumbuka kuwa siku moja utakilalia wewe mwenyewe".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…