Ujenzi wa Hospital utaweka kumbukumbu ya Ndugu zetu wa Lucky Vincent

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
9,133
5,028
Ingawa kumekuwa na shutuma kuhusu matumizi au mgawanyo wa fedha za Rambirambi za ndugu zetu waliopoteza maisha katika ajali ya gari , lakini ni ukweli usiopingika kwamba kama hatutaweka kitu cha kudumu basi ni wazi tutawasahau na hakitakuwa na kumbukumbu la tukio lile.

Hivyo ujenzi wa ward au chumba kimoja katika hospital yeyote hapo Arusha na kuwekwa kwa chanzo cha fedha hizo na ikiwezekana list ya hao ndugu zetu waliopoteza maisha itawapa kumbukumbu ya kudumu kwa hao ndugu zetu.
 
machungu yako palepale... unapoahidi kusaka rambirambi afu unameza ungekuwa wewe ungeshangilia au ungefinyajee??
usituletee serikale ya rambirambi zombi weyeee
 

Rambirambi za Samwel Sitta,George Kahama,Stephen Kabwe zilipelekwa kujenga chumba gani cha hospitali??

Je zile gharama za mazishi,usafiri,chakula,jeneza na mengineyo zilikatwa kutoka kwenye Rambirambi??Kama hazikuguswa kwanini tuguse hizi za wanyonge au kwa sababu hawana sauti??

CCM acheni uhuni.
 
Si wazo baya.. lakin hoyo pesa mwanzon ilitakiwa iende kwa wafiwa.. kuhusu kujenga hospitali, serikal ilikuwa wapi mpaka watumie hilo fungu kujenga hospitali?

Inamasna maafa yasimgetokea, basi hilo wazo lidingekuwepo na hospital ingebaki vile vile?
 
Rambirambi haijengi kumbukumbu....
 
Si wazo baya.. lakin hoyo pesa mwanzon ilitakiwa iende kwa wafiwa.. kuhusu kujenga hospitali, serikal ilikuwa wapi mpaka watumie hilo fungu kujenga hospitali?

Inamasna maafa yasimgetokea, basi hilo wazo lidingekuwepo na hospital ingebaki vile vile?

Muulize, Je mfano zisopotosha serikali itaomba maafa mengine ili waweze kumalizia ujenzi? Au wataanza kuzunguka misibani wakiomba rambi rambi?
 
Hii comment aione RC wa Arusha &Co.

Mungu anawaona kwa hili la kula rambirambi.

 
Hospitali ijengwe na charities siyo rambirambi. Haya majitu yamekuwa mumiani kabisa. Manyonya damu kabisa. Laana ya hizi rambirambi nyie subirini tu mtaona. Naona mvua imerudi sijui imefata nini....
 

Rambi rambi ya mv bukoba imejenga chumba cha hospital gani?
 
Wanatumia ubabe tu, ila hawana mamlaka ya kubadilisha matumizi ya hizo hela.
 
Hata kuandika hujui, hiyo kumbukumbu unaihitaji kwa ajili gani? kwa faida ya nani? waliofiwa ndio wenye machungu wala hawahitaji kumbukumbu, makaburi na pengo la watoto wao kuondoka ni kumbukumbu ya kudumu.., Haya zile za kagera ziko wapi? zimeacha kumbukumbu gani unayohitaji iwepo Arusha? Nyie watu hamjawahi kufiwa?! Msiba usikie kwa jirani hivyo hivyo uuombee rambirambi usiombe yakufike.. Waacheni watoto wapumzike, wazazi tuwaombee faraja sio kujadili kila siku upuuzi wa matumizi ya rambirambi.
 
Kuna wakati nashangaa sana mawazo ya ajabu kama haya yako. Meya anajinufaishaje kisiasa? Kama ni kujulikana anajulikana zaidi ya huyo Gambo wako.
Halafu una rukia usio lijua. Meya aliombwa na wamiliki wa shule binafsi kwenda kuwakabidhi wafiwa rambirambi. Yaani yeye aalikwe nae aalike??
Mnacho shindwa kuelewa ni kwamba wateule wote wataondoka na mtaiacha Arusha na watu wake.
Haijalishi itachukua miaka mingapi lakini Arusha sio ya wateule itabaki kuwa ya Wakazi wa Arusha.
Msitulazimishe tugombane kwa kuhofia utawala usio na nidhamu hata kwenye mambo serious. Hivi hata misiba mnaifanya deal?? Aibuuu

Hata makaburi au kutokimuona mtoto mmoja kati ya ulio nao inatosha kuwa kumbukumbu sio mpaka pesa za pole zitumike kwa mambo ambayo ni ya serikali kufanya
 
Watu wafe Wao rambirambi za wafiwa ndio zijenge hospitali,Kama serekali inajenga hospitali kwa kutumia rambirambi za wafiwa,rambirambi ya serekali kwa wafiwa ni kitu gani?.
Tatizo mkuu wa Mkoa alidhani hapo anajijenga
Kumbe amejiporomosha na kujidharaulisha. Hii ni Arusha hakuna boya hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…