Son of the universe
New Member
- May 29, 2024
- 3
- 6
Kwanza nitumie fursa hii kuipongeza serikali kupitia wizara ya ujenzi, TANROADS na TARURA kwa miradi yote ya ujenzi wa barabara iliyokwisha kamilika, inayoendelea kukamilishwa na itakayokamilishwa nchini kote.
Napenda kuzungumzia barabara kuu zinazopatikana ndani ya majiji katika nchi yetu ya Tanzania hususani jiji la Dar es salaam.
Kabla hakujaanza miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi yaani BRT barabara za Nyerere, kawawa, kilwa na nyinginezo zilikuwa na nafasi iliyoachwa na kupandwa miti na maua ndani yake.
Faida za miti na maua hayo yaliyokuwepo ndani ya hifadhi za barabara zetu hizo sio tu ilikuwa ni kupendezesha barabara hizo bali pia zilikuwa zinatoa vivuli kwa abiria na watumiaji wa barabara hizo wasiumizwe na jua kali linalochoma sana katika jiji la Dar es salaam.
Pia mimea hiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika upunguzaji wa kelele zitokanazo na vyombo vya usafiri vinavyopita katika barabara hizo kwa kukaribisha ndege wanaochangia milio inayonyonya kelele hizo.
Aidha mimea hiyo ilikuwa ni sehemu muhimu ya kupunguza gesi ya ukaa inayotolewa na vyombo vya moto vinavyopita katika barabara hizo pamoja na zile zitokazo katika viwanda vinavyopatikana pembezoni mwa barabara hizo hasa barabara ya nyerere na hivyo kupunguza athari hasi za kimazingira ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la joto ndani ya jiji letu.
Kwa kuongezea mimea hiyo husaidia kuongeza gesi safi ya oksijeni kwa abiria na watumiaji wa barabara hizo hasa ikilinganishwa na namna magari ya abiria maarufu kama daladala yanavyojaza watu na hivyo kushindwa kupumua vyema lakini uwepo wa miti na maua mengi husaidia kuongeza kiasi cha gesi muhimu ya oksijeni kwa watumiaji hao wa barabara.
Tangu ilipoanza miradi ya ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi basi miti na maua hayo yote yameondolewa katika barabara za Kawawa, Kilwa na sasa Nyerere na badala yake zimewekwa zege na pavings mahali pote kwenye barabara na hivyo kukosekana hata chembe ya nafasi kwa ajili ya miti na maua.
Na kuna kila dalili kuwa hata barabara zilizosalia pia basi jambo hilo hilo litakuja kufanyika wakati wa ujenzi wa barabara za Mandela, Ali Hassan Mwinyi, Sam Nujoma na zingine ambazo kwa wakati huu bado zina bustani nzuri za kuvutia za miti na maua.
Ninashauri wabunifu na wajenzi wa barabara zote hizo ambazo ni bora na muhimu kwa matumizi yetu wakumbuke pia na umuhimu wa miti na maua katika barabara hizo kama nilivyoeleza hapo juu. Naziona barabara hizo zikipendeza zaidi kuliko zilivyo sasa kama zikiweza kubuniwa sehemu kwa ajili ya upandaji wa maua ya kisasa na yanayovutia kama ilivyo katika miji ya wenzetu katika nchi zilizoendelea.
Na ikiwezekana badala tu ya kupanda miti basi ipandwe hata miti ya matunda ambayo itakuwa chakula kwa wapita njia na wanyama wengine wanaoishi katika miti hiyo.
Nashauri pia uwekwe utaratibu kama huo kwa barabara zote nchi nzima kupanda miti na maua pembezoni mwa hizo barabara ili iwe hatua muhimu katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuongezeka kwa joto kwa sababu ya uwepo wa rangi nyeusi katika lami pamoja na misuguano inayosababishwa na matairi ya vyombo hivyo vya moto vipitapo katika barabara hizo pamoja na gesi ya ukaa ambayo hutolewa kwa wingi na vyombo hivyo vya moto.
Inaweza kubuniwa pia upandaji wa mimea hasa maua katika nguzo za barabara za juu katika makutano ya barabara kama TAZARA, UBUNGO, UHASIBU, pamoja na zile za reli ya kisasa zinazokatiza katikati ya jiji na nyingine zitakazo ongezwa hii itaongeza zaidi mvuto wa barabara hizo kwa watumiaji na utunzaji wa mazingira pamoja na ulinzi wa viumbe hai wengine ambao wanategemea mimea hiyo kwa makazi na chakula.
Suala hili la utunzaji wa mazingira linapaswa kwenda sambamba kabisa na shughuli zetu za kimaendeleo kama taifa kwa sababu tusipozingatia leo basi ifikapo kesho tutatumia gharama kubwa zaidi kutafuta suluhisho la changamoto ambazo tunazisababisha leo kwa kutozingatia ulinzi wa mazingira na hata miundombinu yetu.
Hili pia linaweza kwenda sambamba na uwekaji wa utaratibu kwa wamiliki wote wa maeneo yanayopakana na barabara kupanda maua na miti katika maeneo hayo ili kuyafanya yavutie na kuleta faida zinazoambatana na zoezi hilo.
Pia nashauri utaalamu uzingatiwe katika uchaguzi wa aina ya miti na maua inayofaa kupandwa katika maeneo hayo pamoja na ubunifu wa namna itakavyopandwa pamoja na kuhudumiwa.
Ninafuraha kubwa kuona wazo hili likitekelezwa na kutimia ndani ya kipindi kifupi cha miaka 5 na kuifanya nchi yetu hasa barabara za majiji yake kuzidi kuvutia kwa watumiaji wake huku tukiendelea kulinda mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika miji na majiji yetu kote Tanzania.
Natamani kuiona Tanzania ya kijani inayovutia machoni mwa kila anayepita njiani katika barabara zake zilizopambwa vizuri kwa miti na maua ya kuvutia pamoja na ndege wazuri wanaoburudisha masikio ya wapita njia kwa milio murua wakifurahia kuishi katika nchi nzuri yenye utajiri mwingi wa amani na utulivu.