Ujenzi Ofisi Mpya ya Mkuu wa Wilaya Chunya Kupangiwa Bajeti 2025/2026

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,781
1,279

UJENZI OFISI MPYA YA MKUU WA WILAYA CHUNYA KUPANGIWA BAJETI 2025/26

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Dkt. Festo Dugange amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuweka kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 maombi ya fedha kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.

Mhe. Dkt. Dugange ametoa maelekezo hayo bungeni jijini Dodoma Februari 14, 2025 kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lupa, Mhe. Masache Kasaka aliyetaka kujua lini serikali itatoa maelekezo kwa ofisi ya mkuu wa Mbeya kufanya maombi maalum ya fedha kwaajili ya ujenzi wa Ofisi hiyo.

Akijibu swali hilo, Mhe. Dkt. Dugange amesema “Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeshawasiliana na mkuu wa mkoa wa Mbeya na kumpa maelekezo kupitia katibu Tawala wa mkoa kuleta bajeti kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chunya nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI kusisitiza maelekezo hayo kwa mkuu wa mkoa wa Mbeya ili wakati wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2025/26 walete maombi hayo.”

Mhe. Dkt. Dugange amesema Serikali imeandaa michoro na gharama za ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya ambapo kiasi cha Sh.Bilioni 3.5. kinahitajika.

“Kwa kuwa kipindi cha maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2025/26 kimefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya itawasilisha maombi hayo katika mpango na bajeti Mkuu wa Wilaya ya Chunya,” amesisitiza

Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya lililopo kwa sasa lilijengwa mwaka 1937 na sasa jengo hilo ni chakavu na kumekuwapo na juhudi za ukarabati kufanyika mara kwa mara.
 

Attachments

  • GjwzLdwWgAA9_MF.jpg
    GjwzLdwWgAA9_MF.jpg
    62.3 KB · Views: 1
  • IMG-20220526-WA0054.jpg
    IMG-20220526-WA0054.jpg
    196 KB · Views: 1
Back
Top Bottom