Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
15,038
55,914
Kwa kweli aliyekuja na mpango wa kupanua ujenzi wa Mwendokasi sijui kama alizingatia mipango ya awali ya namna jiji lenyewe lilivyo.

Inaonekana kilichofanyika ni kujaribu kuleta plan mpya juu ya plan ya zamani kabla hata ya kufanya mabadiliko makubwa ktk plan ya zamani.

Leo barabara za zamani zinaminywa ukubwa ili kujenga mwendokasi. Matokeo yake ni kuwa unaminya flow ya magari binafsi ili kutoka nafasi kwa magari ya kampuni moja ya mwendokasi, maana magari binafsi hayaruhusiwi kutumia njia ya mwendokasi. Hii kamwe haitotatua tatizo la misongamano ya magari bali inaweza kuzidisha.

Kibaya zaidi ktk kuminya barabara za magari ya kawaida, hata space kwa ajili ya watembea kwa miguu inakosekana. Hii ni disasater.

Ukiachilia mbali hilo, unakuta mavituo ya mwendokasi ni makuuubwa kwelikweli, sasa sijui unatengeneza kituo kikubwa cha mwendokasi ili iweje. Haya ni matumizi mabaya ya pesa

Ukienda mjini huko Posta, mwendokasi eti mwendokasi nayo imepenyezwa kwenye kipande cha barabara ya Tanganyika library na Posta, halafu kuna likituo likuuubwa pale wakati tayari posta ya zamani kuna likituo lingine kwa magari yanayotokea Ferry. Hii ni ajabu sana.

Hebu sasa serikali ifikirie kujenga Subways na Metro jijini Dar. Hiyo inaweza kuwa effective zaidi kuliko haya mabarabara ya mwendokasi kila sehemu
 
Mwendokasi ikitumika effectively kukiwa na mabasi ya kutosha 100% inatoa tatizo la foleni.

Unakumbuka Foleni ya magomeni iliokuwa inafika hadi fire? Ilikufa ghafla tu ile foleni Mwendokasi ilipoanza na watu wakapaki magari binafsi nyumbani.

Cha muhimu kuwe na mabasi na watu wakae level seat na kama wanasimama wawe wachache, sio kurundikana kama mifugo.
 
Sidhani kama wanajua wanatakiwa kufanya nini hasa kupangilia mji wa Dar katika miondombinu, inawezekana mengi yanayofanyika ni trial and error tu, bahati mbaya kodi za raia ndio zinateketezwa.
 
Ebu acha kwanza zikamilike then ndio tuanze kukosoa kwa sasa bado mapema.
Husubiri nyumba ikamilike ndiyo upige plan. Una plan kwanza ndiyo unajenga. Nadhani jibu sahihi ungeelezea kwa undani kuwa hicho anachohofu hakiwezi kutokea.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hebu sasa serikali ifikirie kujenga Subways na Metro jijini Dar. Hiyo inaweza kuwa effective zaidi kuliko haya mabarabara ya mwendokasi kila sehemu
Hii ndio sukuhisho ya msongamano wa magari. Nadhani malengo ya BRT sio kupunguza msongamano wa magari bali ni kuondoa magari binafsi ya abiria.
Kwa jinsi jiji lilivyo busy, ni ngumu sana kuondoa magari binafsi yabakie magari ya mwendokasi.
 
Huu mradi ukiwa na magari mwengi na uhakika watu wengi watapaki magari nyumbani na utapunguza foleni kwa asilimia kubwa sana. Matatizo yanayo kwamisha huu mradi yanajulikana Rushwa na ufisadi,mtu akisema mradi huu unajiendesha kwa hasara na kataa.

Ila ndio hivyo nchi yetu inaongozwa na matukio ya kisiasa, huu mwaka ni wa uchaguzi magari yatanunuliwa kupooza kidogo, ila baada ya kubata lao mwakani msoto unaendelea kama kawa.Maana mminyano wa mwendokasi sio masihala.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hii ndio sukuhisho ya msongamano wa magari. Nadhani malengo ya BRT sio kupunguza msongamano wa magari bali ni kuondoa magari binafsi ya abiria.
Kwa jinsi jiji lilivyo busy, ni ngumu sana kuondoa magari binafsi yabakie magari ya mwendokasi.
Sasa huoni ukiondoa msongamano wa magari binafsi huoni kuwa umepunguza foleni?

Miradi ya Mwendokasi hata treni za mijini lengo ni kupunguza foleni. Sababu kukiwa na usafiri wa uhakika,watu hawa minyani na hawakai mda mrefu kituoni, hamna mtu atakaye tumia gari kwenda ofisini,yaani ktk watu kumi basi watu watakao tumia magari yao hawazidi watano.
 
Soma vizuri hoja yangu mkuu.
Kwa nature ya jiji la Dar na shughuli zake ni ngumu sana kumaliza msongamano wa magari. Hata hizo nchi ambazo zimeendekea na zinatumia metro bado barabara za pembeni zina magari mengi ingawa hakuna misongamano kwakuwa miundombunu yao iko vizuri gari zinatembea vizuri.
Mwendokasi kamwe haiwezi kuondoa msongamano wa magari. Kilichosaidia ni kuondoa vidaladala ndio maana unaona kuna unafuu. Magari binafsi bado yataendelea kuwepo hata zikiwekwa metro.
 
Husubiri nyumba ikamilike ndiyo upige plan. Una plan kwanza ndiyo unajenga. Nadhani jibu sahihi ungeelezea kwa undani kuwa hicho anachohofu hakiwezi kutokea.

Tayari zipo mwendokasi zilizokamilika na hazijatatua shida ya usafiri Dar, bali ni kama tatizo limezidi!
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hakuna kitu wanafanya.
Wanapaka rangi machuma ya kuingia vituo vya mwendokasi lakini mabasi mabovu 🤣🤣🤣.
Yani bora hata vituo visingejengwa lakini mabasi yakawepo.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Kwa kweli aliyekuja na mpango wa kupanua ujenzi wa Mwendokasi sijui kama alizingatia mipango ya awali ya namna jiji lenyewe lilivyo.

Inaonekana kilichofanyika ni kujaribu kuleta plan mpya juu ya plan ya zamani kabla hata ya kufanya mabadiliko makubwa ktk plan ya zamani.

Leo barabara za zamani zinaminywa ukubwa ili kujenga mwendokasi. Matokeo yake ni kuwa unaminya flow ya magari binafsi ili kutoka nafasi kwa magari ya kampuni moja ya mwendokasi, maana magari binafsi hayaruhusiwi kutumia njia ya mwendokasi. Hii kamwe haitotatua tatizo la misongamano ya magari bali inaweza kuzidisha.

Kibaya zaidi ktk kuminya barabara za magari ya kawaida, hata space kwa ajili ya watembea kwa miguu inakosekana. Hii ni disasater.

Ukiachilia mbali hilo, unakuta mavituo ya mwendokasi ni makuuubwa kwelikweli, sasa sijui unatengeneza kituo kikubwa cha mwendokasi ili iweje. Haya ni matumizi mabaya ya pesa

Ukienda mjini huko Posta, mwendokasi eti mwendokasi nayo imepenyezwa kwenye kipande cha barabara ya Tanganyika library na Posta, halafu kuna likituo likuuubwa pale wakati tayari posta ya zamani kuna likituo lingine kwa magari yanayotokea Ferry. Hii ni ajabu sana.

Hebu sasa serikali ifikirie kujenga Subways na Metro jijini Dar. Hiyo inaweza kuwa effective zaidi kuliko haya mabarabara ya mwendokasi kila sehemu
Mkuu

Vuta pumzi

Chuki inaua kuliko ukimwi
 
Hakuna kitu wanafanya.
Wanapaka rangi machuma ya kuingia vituo vya mwendokasi lakini mabasi mabovu 🤣🤣🤣.
Yani bora hata vituo visingejengwa lakini mabasi yakawepo.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

Siku hizi unaweza kukaa kituo cha mwendokasi saa nzima kusubiri basi.

Very poor!
 
Soma vizuri hoja yangu mkuu.
Kwa nature ya jiji la Dar na shughuli zake ni ngumu sana kumaliza msongamano wa magari. Hata hizo nchi ambazo zimeendekea na zinatumia metro bado barabara za pembeni zina magari mengi ingawa hakuna misongamano kwakuwa miundombunu yao iko vizuri gari zinatembea vizuri.
Mwendokasi kamwe haiwezi kuondoa msongamano wa magari. Kilichosaidia ni kuondoa vidaladala ndio maana unaona kuna unafuu. Magari binafsi bado yataendelea kuwepo hata zikiwekwa metro.
Kupunguza unapunguza ndio najua mji unakuwa, magari yataongezeka na ndio maana serikaini kuna watu wa planning ndio kazi yao kudeal na future ya jiji, ila foleni unaipunguza hata kwa asilimia thelathini.

Mfano nchi kama China,US au India hivyi bila hizi mwendokasi,treni zao mjini we unazani foleni yake ingekuwaje, pamoja na kuwa na mtandao mkubwa wa barabara still bado foleni wanazo,ila foleni zingekuwa kubwa mnoo kama wasingekuwa na mwendokasi na hizi metro za mijini.
 
Ukirejea comment yangu ya awali utaona alichomaanisha mtoa mada na nilicho support ndio hiki umekieleza hapa. Mwendokasi inapunguza au kuondoa aina zingine za usafiri wa umma ila haziondoi msongamano wa magari. Hivyo njia zote zinapaswa kupewa kupaumbele sawa.
Umesema wafanyakazi wataacha magari, ni sawa ila wafanyakazi hapo Dar wenye magari ni wangapi, na kama msongamano unasababishwa na wafanyakazi, kwa nini muda wote barabara ziko busy. Ina maana wafanyakazi muda wote wako barabarani?
Tukubaliane tu kwamba mwendokasi inaondoa aina zingine za usafiri wa umma ila haziondoi msongamano wa magari.
 
Nimekuulizwa swali simple pata picha China,India,US kama wasingekuwa na Mwendokasi au Metro hivi kwa sasa hali yao ingekuwaje?

Kwani mimi nimesema muda wote kuna foleni?, foleni zipo asubuhi na jioni sababu watu wanawahi makazini na jioni wanarudi majumbani. Kwa kupaki magari kwa mda wa jioni na asubuhi utakuwa umepunguza magari mengi tu barabarani.

Kwani neno mfanyakazi ww unalielewaje?au unazani walio ajiriwa......?

Maana ni ngumu kukihudumia chombo cha usafiri kama huna kazi ya kukuingizia kipato tena cha uhakika.
 
Usilinganishe mabarabara mapana ya kule na vibarabara vidogodogo vya huku.
 
Back
Top Bottom