Ujasusi, Yesu dhidi ya Katanga

PutinV

JF-Expert Member
Apr 17, 2017
1,046
1,643
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali (maandiko na mapokeo) Yesu alizaliwa Bethlehemu wakati wa utawala wa Kaisari Augusto na kukulia huko Nazareti katika familia ya Yosefu seremala. Yesu alianza kuhubiri na kuwafundisha watu alipokuwa na umri wa miaka 30 (Luka 3:23) na alifanya hivyo katika maeneo mbalimbali kama Galilaya, Samaria na Bethsaiada.

Yesu alizaliwa na kuishi wakati wa utawala wa Rumi katika Yudea, jimbo la Yudea halikuwa na faida sana bali lilikuwa na umuhimu kwa utawala wa Rumi kwa kipindi hicho kwani liliunganisha majimbo ya Syria na Misri, majimbo yenye faida kwa Rumi.

IMG_5796.JPG

Eneo lilokuwa chini ya Rumi.

Bila kujali ni namna gani watu walio mzunguka Yesu katika shughuli zake lakini haifichiki Yesu alizaliwa na kuishi katika kipindi ambapo eneo zima la Yudea lilikuwa katika shinikizo kubwa la kisiasa.

Utawala wa Rumi katika Yudea uliathiri mambo mengi katika utamaduni wa Wayahudi ikiwemo dini kwani magavana wa Kirumi ndio walio husika na uteuzi wa Kuhani mkuu. Mfano gavana Valerius Gratus aliyekuwa gavana wa Yudea kabla ya Pilato aliteua makuhani tofauti tofauti wakiwemo Anasi na Kayafa.

Wakati huu majukumu ya Kuhani mkuu yalikuwa ya kidiplomasia na kisiasa zaidi tofauti na majukumu yaliyotajwa na sheria ya Musa kwani Kuhani mkuu na baraza lake waliruhusiwa kukamata wahalifu na kuwahukumu kulingana na sheria za Kiyahudi mbele ya Baraza.
IMG_5907.JPG

Mafundisho na miujiza aliyotenda Yesu vilikuwa ni tishio kubwa kwa Kayafa na baraza lake la Mafarisayo kwani watu wengi walimuamini Yesu na kumfuata wakiamini kuwa ndiye Masiha aliyetabiriwa kuja kuwaokoa kutoka utawala wa Rumi. Wakati Yesu akiwa Galilaya na sehemu nyingine wakuu wa Wayahudi na Mafarisayo walituma wapelelezi waweze kumchunguza na kumtia hatiani kwa maswali yao ya mitego.

Pamoja na mipango yao haikuwa rahisi kumuingiza Yesu katika mitego kwani Yesu alijibu kwa ufanisi mkubwa. Mfano walipo muuliza kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari. (Mathayo 22:21)

Pia haikuwa rahisi kumtega Yesu kutokana na elimu yake kubwa katika maandiko na sheria za Kiyahudi.

Lakini pamoja na ubobezi wa Yesu katika mambo tajwa hapo juu, Yesu pia alikuwa na chembechembe za ujasusi.

Yesu alifahamu kuwa muda wote alikuwa chini ya uangalizi wa makuhani na wazee. Mambo aliyofanya huko Galilaya yaliwanyima usingizi na hivyo iliwabidi kumdhibiti kabla hajaingia Yerusalemu mji wenye watu wengi asije kuleta ghasia ambazo zingeweza kuonekana kama mapinduzi kwenye macho ya Warumi. Hivyo Yesu alifanya baadhi ya mambo kwa usiri na wakati mwingine bila hata wafuasi wake wa karibu kufahamu.

Wakati Yesu alipoukaribia mji wa Yerusalemu aliwatuma wanafunzi wake katika kijiji fulani wakamletee punda ambaye haifahamiki ni punda wa nani na kama mtu angewauliza walitakiwa wamjibu kuwa 'Bwana anamuhitaji'. Maneno 'bwana anamuhitaji' yalitosha kufanya wafuasi wa Yesu wapewe punda!. Kwa mujibu wa injili ya Marko wafuasi wa Yesu walipofika katika kijiji hicho walikuta punda amefungwa kama Yesu alivyoeleza lakini karibu na mahali hapo palikuwa na watu. Yaonyesha watu hao walikuwa hapo ili kuhakikisha punda huyo anamfikia Yesu. Kama Yesu angetafuta punda huyo bila tahadhari huenda viongozi wa Wayahudi wangepata habari na kupata namna ya kudhibiti Yesu asiingie Yerusalemu.

Haijulikani ni kwa namna gani Yesu aliandaa upatikanaji wa punda kwa ajili ya kuingilia Yerusalemu lakini kwa namna yoyote ilikuwa ni kwa lengo la kukwepa mamlaka za Kiyahudi kwa kufanya jambo ambalo halikuwa la kawaida kwani haikuwa kawaida kwa mtu yeyote maarufu kuingia Yerusalemu akiwa juu ya punda.

Kwanini?
Wakuu wa Wayahudi hawakutaka kumkamata Yesu akiwa katika umati wa watu lakini zaidi hawakutaka apate umaarufu Yerusalemu kama alivyo pata umaarufu katika Galilaya na miji mingine. Kama Yesu angeingia Yerusalemu akiwa na watu wachache huenda mamlaka za Kiyahudi zingemkamata kabla ya kufanya jambo lolote hivyo wafuasi wa Yesu waliandaa mapokezi ya Yesu huko Yerusalemu katika namna ambayo ingekuwa ni ngumu kwa viongozi wa Wayahudi kumkamata. Hivyo Yesu aliingia Yerusalemu kama alivyo eleza nabii Zakaria kuhusu Masiha wa Bwana, hivyo umati wa watu ulitoka kuja kumlaki.

Baada ya Yesu kufika Yerusalemu aliingia hekaluni na kuvuruga biashara za wavunja fedha na wauzaji wa njiwa. Lakini ilipofika jioni Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini na kwenda kusiko julikana.

Katika karne ya 20 shirika la FBI lilitumia kifupi cha MICE kuelezea mambo gani yanayoweza kuwafanya watu walioko upande wa adui wamsaliti adui. Kirefu cha MICE ni Money, Ideology, Compromise na Ego. Hivyo makuhani iliwabidi kutumia mbinu nyingine kumtia Yesu mbaroni. Makuhani waliamua kutumia tamaa ya Yuda katika fedha (Yohane 12: 4-6) ili waweze kupata taarifa za siri za Yesu.

Katika maandalizi ya Pasaka Yesu na wanafunzi wake walihitaji kusherehekea siku hiyo kama watu wengine na hivyo iliwapasa kutafuta sehemu watakayo kula Pasaka wakiwa na pamoja. Kutokana na Yesu kuwa chini ya upelelezi ilimpasa kutafuta sehemu ya siri ili kuwakwepa viongozi wa Kiyahudi hivyo Yesu hakuwaambia wanafunzi wake ni wapi watakapolia Pasaka yao hadi siku yenyewe ilipowadia. Siku hiyo Yesu aliwaagiza wanafunzi wake MJINI (kumaanisha alikuwa nje ya mji), humo watakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji wamfuate bila kuongea naye lolote hadi kwenye nyumba atakayo ingia kisha wamuulize mwenye nyumba kuhusu chumba alicho andaa Yesu kwa ajili ya Pasaka. Naye Yesu alifika jioni pamoja na wanafunzi wake kwa ajili ya kula Pasaka. Kamwe haikuwa rahisi kwa wakuu wa makuhani kufahamu ni wapi alipokuwa Yesu siku hiyo. Labda walidhani kama kawaida yake Yesu hakukuaa mjini wakati wa jioni hivyo isingekuwa rahisi kufahamu kama jioni hiyo angekuwa Yerusalemu. Hii ilikuwa ni nafasi ya Yuda kwenda kuwataarifu viongozi wa Wayahudi kuhusu nafasi hii adimu ya kumkamata Yesu kwani jioni ya siku hiyo alikuwa Yerusalemu!

Wakati wa chakula Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa mmoja wao atamsaliti lakini haijulikani ni kwa namna gani Yesu alitambua hilo. Labda ni kwa sababu Yesu aliwafahamu wanafunzi wake sana na alijua upande dhaifu wa Yuda katika pesa (Yohane 12: 4-6) hivyo makuhani wangemtumia katika kumkamata Yesu. Ni kweli safari hii Yesu alikuwa amefeli katika ujasusi na mmoja kati ya wafuasi wake amemsaliti.

Yuda Iskarioti aliondoka mapema na kwenda kuwataarifu wakuu wa makuhani kuwa Yesu alikuwa Yerusalemu jioni ya siku hiyo. Bila shaka taarifa hizo ziliwashtua sana lakini ilikuwa ni nafasi ya pekee kwao kuweza kumkamata Yesu ili kulikomboa taifa lao.

Kama nilivyoandika mwanzo, Kuhani mkuu alikuwa kiungo kati ya utawala wa Rumi na Wayahudi wote, kama Yesu ambaye alichukuliwa kama mwanamapinduzi na mwanafalsafa angesababisha ghasia Yerusalemu ingemaanisha kuwa Kuhani mkuu ameshindwa kazi yake hiyo ya ukuhani mkuu. Kayafa ni Kuhani aliyedumu muda mrefu zaidi akidumu katika ofisi kwa muda wa miaka 18. Bila shaka aliweza kudumu muda wote huo kwa sababu ya umahiri wake kwa Warumi akishirikiana vyema na gavana wa wakati huo yaani Pilato (ikumbukwe kuwa baada uteuzi wa Pilato kutenguliwa na mfalme Caligula Kayafa naye uteuzi wake ulitenguliwa). Kwa hiyo Kayafa asingekubali mtu mmoja amuharibie sifa yake kwa Warumi hivyo alichukua hatua haraka sana na kutuma askari kwenda kumkamata Yesu.

Yesu baadaye anatajwa akiwa katika bustani ya Gethsemane ambayo iko nje kidogo mji wa Yerusalemu ambapo alikamatwa baada ya Yuda kufika na askari. Hii inamaanisha Yesu aliondoka Yerusalemu mara tu baada chakula hivyo huenda Yuda alifika kwenye nyumba Ile lakini Yesu hakuwepo tena lakini kwa namna yoyote ile ilikuwa Yesu akamatwe usiku huo. Huenda Yuda alifahamu Yesu alipenda kusali katika bustani ya Gethsemane hivyo alipokwenda na askari wakamkuta hapo.

Kwanini Yesu alitakiwa kukamatwa haraka hivi?
Kwa sababu haijulikani ni lini tena wangeweza kumkamata kwa sababu ya uwezo wa kijasusi wa Yesu.

Baada ya Yesu kukamatwa iliwapasa viongozi wa Kiyahudi wamfunge katika chumba cha hekalu hadi asubuhi kama walivyo fanya kwa wanafunzi wake (Matendo ya mitume 4:3, 5:17) ili asubuhi aweze kuhukumiwa na baraza zima la wazee.

Lakini kinyume na taratibu Yesu alipelekwa nyumbani kwa Anasi baba mkwe Kayafa na kisha baadaye kwa Kayafa aliyekuwa Kuhani mkuu.
Usiku ule ilimpasa Kuhani mkuu kama Myahudi yoyote yule, asheherekee siku ya mikate akiwa na familia yake lakini yeye alitaka kumaliza kesi ya Yesu mapema zaidi hivyo kesi hiyo ilisikilizwa nyumbani kwake wakati wa usiku bila uwepo wa wajumbe 72 wa baraza la Wayahudi.

Kwanini Kayafa alifanya hivi?
Mbali na sababu ya uhusiano na Rumi sababu nyingine iliyomfanya Kayafa aharakishe kesi ya Yesu.

Huenda Kayafa aliogopa kupata upinzani kwani baadhi ya wajumbe wa baraza la Wayahudi kama Yosefu wa Arimathaya, Nikodemo na Gamalliel walikuwa wafuasi wa Yesu japo kwa siri.

Kayafa alimuuliza Yesu kama yeye ndiye Masiha.
Yesu alijibu kuwa yeye ndiye, kwa mujibu wa Kayafa aliyekasirika kiasi cha kuchana mavazi yake jibu hilo lilitosha kumhukumu Yesu kufa lakini iliwapasa kupata ruhusa kutoka kwa Pilato.

Kayafa alihitaji Yesu auwawe haraka zaidi lakini hakuwa na mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo bila uwepo wa baraza la wazee. Hivyo ilimbidi atumie mbinu nyingine ambayo itamuhusisha Pilato ambaye ndiye mtu mwingine aliyekuwa na mamlaka ya kuhukumu kifo. Kayafa alihitaji msaada usiokuwa wa moja kwa moja kutoka kwa Pilato hivyo pia alihitaji shitaka jipya litakalo mvutia Pilato kutoa hukumu kwa Yesu kwani shitaka la 'Yeye amesema ni Masiha mwana wa Mungu' lisingemshawishi Pilato na hivyo asingetoa hukumu. Hivyo Yesu aliundiwa shitaka jingine la kujiita mfalme wa Wayahudi jambo ambalo lilikuwa ni kosa la uhaini dhidi ya Kaisari na hivyo Pilato kama muwakilishi wa Kaisari Yudea hakupaswa kufumbia jambo hilo macho.

Pilato alitakiwa kutoa adhabu kali ili liwe onyo kwa watu wengine watakao jaribu kupinga utawala wa Rumi lakini Pilato alipo gundua kuwa Yesu hakuwa na hatia bali alikuwa kwenye mgogoro wa kifalsafa na viongozi wake wa dini alijaribu kumuachia lakini Wayahudi walimkumbusha urafiki wake na Kaisari Tiberio. Pilato akihofia mashitaka ya kufumbia macho uhaini kumfikia Kaisari, hakuona faida wala hasara ya kuuawa mtu mmoja katika Yudea yote hivyo akamuhukumu Yesu kifo cha msalabani kama wahalifu wengine wa kipindi hicho.

Uhasama kati ya Yesu na viongozi wa Wayahudi haukuhusisha utaalamu wa sheria ya dini ya Kiyahudi tu hata mbinu za kijasusi zilitumika kumnyamazisha Yesu. Yesu naye alienenda nyendo zake kwa umakini wa hali ya juu na hii inaonyesha alitumia ujasusi kukwepa mbinu za kijasusi za makuhani katika kumkamata. Mwisho makuhani walifanikiwa kwa kuweza kumrubuni mmoja wa wafuasi wake naye akamsaliti.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali (maandiko na mapokeo) Yesu alizaliwa Bethlehemu wakati wa utawala wa Kaisari Augusto na kukulia huko Nazareti katika familia ya Yosefu seremala. Yesu alianza kuhubiri na kuwafundisha watu alipokuwa na umri wa miaka 30 (Luka 3:23) na alifanya hivyo katika maeneo mbalimbali kama Galilaya, Samaria na Bethsaiada.

Yesu alizaliwa na kuishi wakati wa utawala wa Rumi katika Yudea, jimbo la Yudea halikuwa na faida sana bali lilikuwa na umuhimu kwa utawala wa Rumi kwa kipindi hicho kwani liliunganisha majimbo ya Syria na Misri, majimbo yenye faida kwa Rumi.

Bila kujali ni namna gani watu walio mzunguka Yesu katika shughuli zake lakini haifichiki Yesu alizaliwa na kuishi katika kipindi ambapo eneo zima la Yudea lilikuwa katika shinikizo kubwa la kisiasa.

Utawala wa Rumi katika Yudea uliathiri mambo mengi katika utamaduni wa Wayahudi ikiwemo dini kwani magavana wa Kirumi ndio walio husika na uteuzi wa Kuhani mkuu. Mfano gavana Valerius Gratus aliyekuwa gavana wa Yudea kabla ya Pilato aliteua makuhani tofauti tofauti wakiwemo Anasi na Kayafa.

Wakati huu majukumu ya Kuhani mkuu yalikuwa ya kidiplomasia na kisiasa zaidi tofauti na majukumu yaliyotajwa na sheria ya Musa kwani Kuhani mkuu na baraza lake waliruhusiwa kukamata wahalifu na kuwahukumu kulingana na sheria za Kiyahudi mbele ya baraza.

Mafundisho na miujiza aliyotenda Yesu vilikuwa ni tishio kubwa kwa Kayafa na baraza lake la Mafarisayo kwani watu wengi walimuamini Yesu na kumfuata wakiamini kuwa ndiye Masiha aliyetabiriwa kuja kuwaokoa kutoka utawala wa Rumi. Wakati Yesu akiwa Galilaya na sehemu nyingine wakuu wa Wayahudi na Mafarisayo walituma wapelelezi waweze kumchunguza na kumtia hatiani kwa maswali yao ya mitego.

Pamoja na mipango yao haikuwa rahisi kumuingiza Yesu katika mitego kwani Yesu alijibu kwa ufanisi mkubwa. Mfano walipo muuliza kuhusu kulipa kodi kwa Kaisari. (Mathayo 22:21)
IMG_5902.JPG

Pia haikuwa rahisi kumtega Yesu kutokana na elimu yake kubwa katika maandiko na sheria za Kiyahudi.

Lakini pamoja na ubobezi wa Yesu katika mambo tajwa hapo juu, Yesu pia alikuwa na chembechembe za ujasusi.

Yesu alifahamu kuwa muda wote alikuwa chini ya uangalizi wa makuhani na wazee. Mambo aliyofanya huko Galilaya yaliwanyima usingizi na hivyo iliwabidi kumdhibiti kabla hajaingia Yerusalemu mji wenye watu wengi asije kuleta ghasia ambazo zingeweza kuonekana kama mapinduzi kwenye macho ya Warumi. Hivyo Yesu alifanya baadhi ya mambo kwa usiri na wakati mwingine bila hata wafuasi wake wa karibu kufahamu.

Wakati Yesu alipoukaribia mji wa Yerusalemu aliwatuma wanafunzi wake katika kijiji fulani wakamletee punda ambaye haifahamiki ni punda wa nani na kama mtu angewauliza walitakiwa wamjibu kuwa 'Bwana anamuhitaji'. Maneno 'bwana anamuhitaji' yalitosha kufanya wafuasi wa Yesu wapewe punda!. Kwa mujibu wa injili ya Marko wafuasi wa Yesu walipofika katika kijiji hicho walikuta punda amefungwa kama Yesu alivyoeleza lakini karibu na mahali hapo palikuwa na watu. Yaonyesha watu hao walikuwa hapo ili kuhakikisha punda huyo anamfikia Yesu. Kama Yesu angetafuta punda huyo bila tahadhari huenda viongozi wa Wayahudi wangepata habari na kupata namna ya kudhibiti Yesu asiingie Yerusalemu.

IMG_5912.JPG

Haijulikani ni kwa namna gani Yesu aliandaa upatikanaji wa punda kwa ajili ya kuingilia Yerusalemu lakini kwa namna yoyote ilikuwa ni kwa lengo la kukwepa mamlaka za Kiyahudi kwa kufanya jambo ambalo halikuwa la kawaida kwani haikuwa kawaida kwa mtu yeyote maarufu kuingia Yerusalemu akiwa juu ya punda.

Kwanini?
Wakuu wa Wayahudi hawakutaka kumkamata Yesu akiwa katika umati wa watu lakini zaidi hawakutaka apate umaarufu Yerusalemu kama alivyo pata umaarufu katika Galilaya na miji mingine. Kama Yesu angeingia Yerusalemu akiwa na watu wachache huenda mamlaka za Kiyahudi zingemkamata kabla ya kufanya jambo lolote hivyo wafuasi wa Yesu waliandaa mapokezi ya Yesu huko Yerusalemu katika namna ambayo ingekuwa ni ngumu kwa viongozi wa Wayahudi kumkamata. Hivyo Yesu aliingia Yerusalemu kama alivyo eleza nabii Zakaria kuhusu Masiha wa Bwana, hivyo umati wa watu ulitoka kuja kumlaki.

Baada ya Yesu kufika Yerusalemu aliingia hekaluni na kuvuruga biashara za wavunja fedha na wauzaji wa njiwa. Lakini ilipofika jioni Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini na kwenda kusiko julikana.

Katika karne ya 20 shirika la FBI lilitumia kifupi cha MICE kuelezea mambo gani yanayoweza kuwafanya watu walioko upande wa adui wamsaliti adui. Kirefu cha MICE ni Money, Ideology, Compromise na Ego. Hivyo makuhani iliwabidi kutumia mbinu nyingine kumtia Yesu mbaroni. Makuhani waliamua kutumia tamaa ya Yuda katika fedha (Yohane 12: 4-6) ili waweze kupata taarifa za siri za Yesu.

Katika maandalizi ya Pasaka Yesu na wanafunzi wake walihitaji kusherehekea siku hiyo kama watu wengine na hivyo iliwapasa kutafuta sehemu watakayo kula Pasaka wakiwa na pamoja. Kutokana na Yesu kuwa chini ya upelelezi ilimpasa kutafuta sehemu ya siri ili kuwakwepa viongozi wa Kiyahudi hivyo Yesu hakuwaambia wanafunzi wake ni wapi watakapolia Pasaka yao hadi siku yenyewe ilipowadia. Siku hiyo Yesu aliwaagiza wanafunzi wake MJINI (kumaanisha alikuwa nje ya mji), humo watakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji wamfuate bila kuongea naye lolote hadi kwenye nyumba atakayo ingia kisha wamuulize mwenye nyumba kuhusu chumba alicho andaa Yesu kwa ajili ya Pasaka. Naye Yesu alifika jioni pamoja na wanafunzi wake kwa ajili ya kula Pasaka. Kamwe haikuwa rahisi kwa wakuu wa makuhani kufahamu ni wapi alipokuwa Yesu siku hiyo. Labda walidhani kama kawaida yake Yesu hakukuaa mjini wakati wa jioni hivyo isingekuwa rahisi kufahamu kama jioni hiyo angekuwa Yerusalemu. Hii ilikuwa ni nafasi ya Yuda kwenda kuwataarifu viongozi wa Wayahudi kuhusu nafasi hii adimu ya kumkamata Yesu kwani jioni ya siku hiyo alikuwa Yerusalemu!

IMG_5797.JPG

Wakati wa chakula Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa mmoja wao atamsaliti lakini haijulikani ni kwa namna gani Yesu alitambua hilo. Labda ni kwa sababu Yesu aliwafahamu wanafunzi wake sana na alijua upande dhaifu wa Yuda katika pesa (Yohane 12: 4-6) hivyo makuhani wangemtumia katika kumkamata Yesu. Ni kweli safari hii Yesu alikuwa amefeli katika ujasusi na mmoja kati ya wafuasi wake amemsaliti.

Yuda Iskarioti aliondoka mapema na kwenda kuwataarifu wakuu wa makuhani kuwa Yesu alikuwa Yerusalemu jioni ya siku hiyo. Bila shaka taarifa hizo ziliwashtua sana lakini ilikuwa ni nafasi ya pekee kwao kuweza kumkamata Yesu ili kulikomboa taifa lao.

IMG_5805.JPG

Kama nilivyoandika mwanzo, Kuhani mkuu alikuwa kiungo kati ya utawala wa Rumi na Wayahudi wote, kama Yesu ambaye alichukuliwa kama mwanamapinduzi na mwanafalsafa angesababisha ghasia Yerusalemu ingemaanisha kuwa Kuhani mkuu ameshindwa kazi yake hiyo ya ukuhani mkuu. Kayafa ni Kuhani aliyedumu muda mrefu zaidi akidumu katika ofisi kwa muda wa miaka 18. Bila shaka aliweza kudumu muda wote huo kwa sababu ya umahiri wake kwa Warumi akishirikiana vyema na gavana wa wakati huo yaani Pilato (ikumbukwe kuwa baada uteuzi wa Pilato kutenguliwa na mfalme Caligula Kayafa naye uteuzi wake ulitenguliwa). Kwa hiyo Kayafa asingekubali mtu mmoja amuharibie sifa yake kwa Warumi hivyo alichukua hatua haraka sana na kutuma askari kwenda kumkamata Yesu.

Yesu baadaye anatajwa akiwa katika bustani ya Gethsemane ambayo iko nje kidogo mji wa Yerusalemu ambapo alikamatwa baada ya Yuda kufika na askari. Hii inamaanisha Yesu aliondoka Yerusalemu mara tu baada chakula hivyo huenda Yuda alifika kwenye nyumba Ile lakini Yesu hakuwepo tena lakini kwa namna yoyote ile ilikuwa Yesu akamatwe usiku huo. Huenda Yuda alifahamu Yesu alipenda kusali katika bustani ya Gethsemane hivyo alipokwenda na askari wakamkuta hapo.

IMG_5908.JPG

Kwanini Yesu alitakiwa kukamatwa haraka hivi?
Kwa sababu haijulikani ni lini tena wangeweza kumkamata kwa sababu ya uwezo wa kijasusi wa Yesu.

Baada ya Yesu kukamatwa iliwapasa viongozi wa Kiyahudi wamfunge katika chumba cha hekalu hadi asubuhi kama walivyo fanya kwa wanafunzi wake (Matendo ya mitume 4:3, 5:17) ili asubuhi aweze kuhukumiwa na baraza zima la wazee.

Lakini kinyume na taratibu Yesu alipelekwa nyumbani kwa Anasi baba mkwe Kayafa na kisha baadaye kwa Kayafa aliyekuwa Kuhani mkuu.
Usiku ule ilimpasa Kuhani mkuu kama Myahudi yoyote yule, asheherekee siku ya mikate akiwa na familia yake lakini yeye alitaka kumaliza kesi ya Yesu mapema zaidi hivyo kesi hiyo ilisikilizwa nyumbani kwake wakati wa usiku bila uwepo wa wajumbe 72 wa baraza la Wayahudi.

Kwanini Kayafa alifanya hivi?
Mbali na sababu ya uhusiano na Rumi sababu nyingine iliyomfanya Kayafa aharakishe kesi ya Yesu.

Huenda Kayafa aliogopa kupata upinzani kwani baadhi ya wajumbe wa baraza la Wayahudi kama Yosefu wa Arimathaya, Nikodemo na Gamalliel walikuwa wafuasi wa Yesu japo kwa siri.

Kayafa alimuuliza Yesu kama yeye ndiye Masiha.
Yesu alijibu kuwa yeye ndiye, kwa mujibu wa Kayafa aliyekasirika kiasi cha kuchana mavazi yake jibu hilo lilitosha kumhukumu Yesu kufa.

IMG_5799.JPG

Kayafa alihitaji Yesu auwawe haraka zaidi lakini hakuwa na mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo bila uwepo wa baraza la wazee. Hivyo ilimbidi atumie mbinu nyingine ambayo itamuhusisha Pilato ambaye ndiye mtu mwingine aliyekuwa na mamlaka ya kuhukumu kifo. Kayafa alihitaji msaada usiokuwa wa moja kwa moja kutoka kwa Pilato hivyo pia alihitaji shitaka jipya litakalo mvutia Pilato kutoa hukumu kwa Yesu kwani shitaka la 'Yeye amesema ni Masiha mwana wa Mungu' lisingemshawishi Pilato na hivyo asingetoa hukumu. Hivyo Yesu aliundiwa shitaka jingine la kujiita mfalme wa Wayahudi jambo ambalo lilikuwa ni kosa la uhaini dhidi ya Kaisari na hivyo Pilato kama muwakilishi wa Kaisari Yudea hakupaswa kufumbia jambo hilo macho.

Pilato alitakiwa kutoa adhabu kali ili liwe onyo kwa watu wengine watakao jaribu kupinga utawala wa Rumi lakini Pilato alipo gundua kuwa Yesu hakuwa na hatia bali alikuwa kwenye mgogoro wa kifalsafa na viongozi wake wa dini alijaribu kumuachia lakini Wayahudi walimkumbusha urafiki wake na Kaisari Tiberio. Pilato akihofia mashitaka ya kufumbia macho uhaini kumfikia Kaisari, hakuona faida wala hasara ya kuuawa mtu mmoja katika Yudea yote hivyo akamuhukumu Yesu kifo cha msalabani kama wahalifu wengine wa kipindi hicho.

IMG_5911.JPG

Pilato.

Uhasama kati ya Yesu na viongozi wa Wayahudi haukuhusisha utaalamu wa sheria ya dini ya Kiyahudi tu hata mbinu za kijasusi zilitumika kumnyamazisha Yesu. Yesu naye alienenda nyendo zake kwa umakini wa hali ya juu na hii inaonyesha alitumia ujasusi kukwepa mbinu za kijasusi za makuhani katika kumkamata. Mwisho makuhani walifanikiwa kwa kuweza kumrubuni mmoja wa wafuasi wake naye akamsaliti.
___________________________________

Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza, “Kwa nini mnamfungua huyo mwanapunda?”
Wao wakajibu “bwana anamuhitaji”.
 
Jaribu kutoka nje ya box
Well, nje ya box tayari mimi nipo nje ,Namtazama Yesu kama nabii wa Kiroho zaidi,
Ama Muhammad alikuwa Nabii wa Kiutawala mfano wa Muses na Daudi,
hawa walikuwa na Vikosi vya kijeshi na majasusi wa kuchunguza harakati za watesi wao.
Sasa nakushauri wewe utoke ndani ya Box na utazame kwa kulinganisha hawa watumishi wa Mungu Aliye Juu.
 
Umeandika ujasusi ili kuondoa imani na spritual matter ilio ndani ya maandiko.Sayansi na mawazo mengine (wishful thinking) yapo kwenye vitabu vingine eg Da vinc code, moral & dogma Cha Pike nk nk sio biblia. Yesu alikuwa mtu mwenye kuijua kesho.Kingine usichokijua Yesu hakusoma maana hakuwa binadamu 100 % na hii elimu isingemfit maana yeye sio wa Level ya kufundishwa chochote katika umri wowote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well, nje ya box tayari mimi nipo nje ,Namtazama Yesu kama nabii wa Kiroho zaidi,
Ama Muhammad alikuwa Nabii wa Kiutawala mfano wa Muses na Daudi,
hawa walikuwa na Vikosi vya kijeshi na majasusi wa kuchunguza harakati za watesi wao.
Sasa nakushauri wewe utoke ndani ya Box na utazame kwa kulinganisha hawa watumishi wa Mungu Aliye Juu.
Yesu alikuwa jeshi la mtu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu alikuwa jeshi la mtu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
15 Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake. 16 Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu. 17 Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

YOH:11: 39 Yesu akasema, “Ondoeni hilo jiwe!” Martha, dada yake huyo aliyekufa, akamwambia, “Bwana, amekwishaanza kunuka; amekaa kaburini siku nne!” 40 Yesu akamwambia, “Je, sikukwambia kwamba ukiamini utaona utukufu wa Mungu?” 41 Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema, “Nakushukuru Baba kwa kuwa wewe wanisikiliza. 42 Najua kwamba unanisikiliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watu hawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” 43 Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: “Lazaro! Toka nje!” 44 Huyo aliyekuwa amekufa akatoka nje, huku amefungwa sanda miguu na mikono, na uso wake umefunikwa. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mkamwache aende zake.” 45 Basi, Wayahudi wengi waliokuwa wamefika kwa Maria walipoona kitendo hicho alichokifanya Yesu wakamwamini. 46 Lakini baadhi yao walikwenda kwa Mafarisayo wakatoa taarifa ya jambo hilo alilofanya Yesu. 47 kwa hiyo makuhani wakuu na Mafarisayo wakafanya kikao cha Baraza kuu, wakasema, “Tufanye nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi mno. 48 Tukimwacha tu watu wote watamwamini, nao Waroma watakuja kuliharibu Hekalu letu na taifa letu!” 49 Hapo, mmoja wao aitwaye Kayafa, ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo, akawaambia, “Ninyi hamjui kitu! 50 Je, hamwoni kwamba ni afadhali kwenu mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa zima liangamizwe?”

Nauona ujasusi hapa ,lakini Mayahudi nao walikuwa Majasusi si wadogo,kwa Jeshi la Mtu huyu mmoja pekeyake .
Kweli 'He was fighting Man alone'
 
Back
Top Bottom