Ujasusi wa elimu Tanzania

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
10,878
26,106
Baada ya matokeo kutangazwa Leo Tarehe 29.01.2023 , na mie kama Mwl Mzoefu nimeona nitoe mtazamo wangu unaobezi katika Matokeo...Kama nimekosea ni ruhusa nikosolewe...

1. Ukionaa shule ina div I zote ni za point 7 na A kwa masomo yote ujue hao ni majasusi wa elimu, kifupi shule hizi zinahatarisha Maendeleo ya nchi kiujumla na zinafundisha wizi wa hali ya juu...hata ofisini ukiajiri mwanafumzi aliyetoka shule hizi jiandae kulia na kupata hasara ( Binafsi hawa huwa sishughuliki nao kwanza ni wabaguzi hata kwa wanafunzi wenye uwezo mdogo, japo katika tafiti zangu wazazi wengi wengi wanazipenda shule hizi...hasa wazazi ambao hawajasoma)

2. Ukionaa shule ina div I nyingi na div II chache ujue walimu na wanafunzi kwa pamoja wanapambana sana ila nao wanatamani siku moja wapate matokeo kama ya majasusi wa Elimu.

3. Ukiona shule ina div I,II, na III ujue walimu na wanafunzi wanajitahidi kwa uwezo wao waliopewa na Mwenyezi Mungu ila nature imewakatalia..(Kiasili binadamu hatuwezi lingana kiuwezo hasa katika dhana ya kufikiria na matumizi ya ubongo ndio maana umeona madaraja hayo matatu yametokea)

4. Ukiona shule ina div I, II , III, IV na div 0 ujue hiyo shule haina wizi hata kidogo yaana kila mwanafunzi amebebwa na juhudi zake..( Mtu aliyesoma kwenye shule hizi anafaa sana kuajiriwa maana anafahamu binadamu Kwa asili yetu hatulingani kiuwezo )

5. Ukiona shule haina div I Wala div II ila ina div IV na 0 nyingi sana na div III chache sana au hakuna kabisa div III ujue hiyo shule wamekutana mabaharia wote yaani walimu na Wanafunzi wote ni masela..., Ndio maana wakuu wa shule hizo uwa wanaondolewa chini wote....

NOTE: Kikawaida na kihalali shule inatakiwa iwe na division I na 0 chache Kwa sababu mstari unaotenganisha mtu mwenye akili nyingi na mjinga ni mwembamba sana....japo mnaweza msinielewa na maanisha nini hapa ..!! Jitihadi za makusudi ndo zinaweza kuvunja uwiano huu...yaani ukakuta shule ina div I nyingi (ila zisiwe div I za point Saba zote) au div 0 nyingi zaidi.

Ukiona shule ina div I zote za point 7 (na wana A zote) au ina div O zote..nakushauri omba ushauri kwanza kabla kufanya maamuzi ya kumpeleka mwanao kusoma*

*Mtazamo wa Mwl Kabola, Shija F.___Bwiru Boyz Technical Sec School_Mwanza..


C&P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ww ni mwalimu na una akili hii basi naanza kuelewa kwanini mnawekwa kwenye kundi la wasio jielewa wasio na akili na wapumbavu fulani tu. Huwezi kua mjinga kiasi hiki mleta mada ww ni mwalimu useless.

Kuna shule wanapambana usiku na mchana na wana mazingira mazuri ya kufunsishia kwanini wasipate A zote?.
 
Kama ww ni mwalimu na una akili hii basi naanza kuelewa kwanini mnawekwa kwenye kundi la wasio jielewa wasio na akili na wapumbavu fulani tu. Huwezi kua mjinga kiasi hiki mleta mada ww ni mwalimu useless.

Kuna shule wanapambana usiku na mchana na wana mazingira mazuri ya kufunsishia kwanini wasipate A zote?.
Unakili kisoda hujui tu ungejua ungelia sana


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii analysis tena kutoka kwa mtu anayejiita mwalimu naona ndio kioo cha shule zilizofunika kwa zero zinazofundishwa na aina ya huyu jamaa aliyeleta uzi, wewe kama kweli ni mwalimu siwezi kukupa mwanangu umfundishe
 
Uzuri amejitenga na mawazo ya Mwalimu kutoka Bwiru kwa kutuambia ame copy na ku paste, leo mleta mada naona anachafua hali ya hewa tuu.
 
Wewe utakuwa ni mwalimumhuni na usie na exposure yoyote. Ungekuwa na taaluma nzuri na ujuzi wa kutosha kuweza kufundisha katika shule zenye kufaulisha kwa daraja la kwanza wanafunzi wote ningekushauri uende huko ukajifunze.Lkn kwa uandishi na mawazo yako duni Kama haya sikushauri.


Mazingira ya shule hizo, usimamizi wa nidhamu, ubora wa walimu, masurufu, commitment ya walimu na na recruitment ya wanafunzi wao ndiyo vinawabeba.

Nenda St. Francis, nenda Kemobos, nenda Marian schools, nenda Mazinde Juu, nenda Canosa ulinganishe na hiyo kambi (unayoita shule) ambapo wewe upo utaona tofauti
 
Mwalimu mjinga kama huyu hawezi fundisha shule za vipaji ndio maana analalamika akiona wenzake wanapasua. Imagine shule inapokea watoto wenye A na B kwenye wastani wa ufaulu shule ya msingi unataka kuniambia hao wakifundishwa vyema hawapasui A form four.

Acheni kujidhalilisha waalimu mapopoma
 
Back
Top Bottom