Uingereza kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu

ze kokuyo

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
7,417
9,603
Waziri wa ulinzi wa Uingereza amethibitisha kwamba nchi yake itaipatia Ukraine makombora ya masafa marefu ili kuweza kupiga shabaha za mbali.

Makombora hayo ya Storm shadow yanaweza piga shabaha hadi 300km huku yakiruka karibu kabisa na ardhi ili kukwepa kuonwa na rada za adui.

Hapo awali Urusi iliionya Uingereza juu ya uamuzi wa kutaka kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu kwamba ingejibu vikali Jambo hilo.

Ben Wallace akithibisha UK kutoa makombora hayo

Mkuu ze kokuyo, sio "uingereza kuipatia" bali ni kwamba uingereza tayari ameshaikabidhi Ukraine hayo makombora!
1683802060269.jpg

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
 
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imepeleka makombora ya masafa marefu aina ya STORM SHADOW CRUISE MISSILES nchini Ukraine kwa mara ya kwanza. Makombora hayo yanashambulia umbali wa 300km ambayo ni sawa na umbali wote wa Jimbo la Crimea na yanaweza kushambulia mpaka maeneo mbalimbali ndani ya Urusi.

Awali, Ukraine ilitaka kupewa Makombora ya ATACMS kutoka Marekani yenye uwezo sawa na hayo ya Uingereza. Lakini Makombora ya STROM SHADOW hurushwa kupitia ndege za kivita wakati yale ya ATACMS hurushwa kutoka Ardhini kwa kutumia mifumo ya HIMARS.

Wachambuzi wa Masuala ya kijeshi wanasema kwamba Makombora hayo yataisaidia Jeshi la Ukraine kulipiga daraja la KERCH BRIDGE ambalo ndio njia pekee inayounganisha rasi ya Crimea na Urusi bara.

‘We simply will not stand back while Russia kills civilians,’ says UK defence chief Ben Wallace, announcing military aid UK sends Ukraine long-range cruise missiles to fight Russia
 
Alipoachia kiti Boris Warusi wa Mwananyamala wakasema UK itasitisha ufadhili kwa Ukraine.

Wakafika mbali wakasema hakuna mwanachama yoyote wa NATO atakayethubutu kupeleka silaha za masafa marefu.

Kama UK imeanza kupeleka, US anafuata bila shaka. Na huyu akipeleka hiko kifurushi cha masafa marefu patakuwa hapatoshi.
 
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imepeleka makombora ya masafa marefu aina ya STORM SHADOW CRUISE MISSILES nchini Ukraine kwa mara ya kwanza. Makombora hayo yanashambulia umbali wa 300km ambayo ni sawa na umbali wote wa Jimbo la Crimea na yanaweza kushambulia mpaka maeneo mbalimbali ndani ya Urusi.

Awali, Ukraine ilitaka kupewa Makombora ya ATACMS kutoka Marekani yenye uwezo sawa na hayo ya Uingereza. Lakini Makombora ya STROM SHADOW hurushwa kupitia ndege za kivita wakati yale ya ATACMS hurushwa kutoka Ardhini kwa kutumia mifumo ya HIMARS.

Wachambuzi wa Masuala ya kijeshi wanasema kwamba Makombora hayo yataisaidia Jeshi la Ukraine kulipiga daraja la KERCH BRIDGE ambalo ndio njia pekee inayounganisha rasi ya Crimea na Urusi bara.

‘We simply will not stand back while Russia kills civilians,’ says UK defence chief Ben Wallace, announcing military aid UK sends Ukraine long-range cruise missiles to fight Russia
Unafiki tu umewajaa, miaka na miaka Israeli anauwa nini kule palestina??
 
Back
Top Bottom