Uimara wa CCM utategemea upepo wa kisiasa ndani ya Chadema

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
9,469
13,549
Huu ndiyo ukweli kuwa Chadema ikisambaratika CCM itakuwa imara kuliko wakati wo wote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

Ikitokea Mbowe akajitoa katika kinyang'anyiro cha kuwania tena kiti cha uenyekiti Taifa Chadema basi CCM itakuwa tumbo moto. Hii itawapa nguvu baadhi ya makada wa CCM kushinikiza fomu zaidi ya moja zitolewe kugombea uenyekiti wa Taifa CCM, kitendo ambacho kitatikisa umoja bandia unaoonekana hivi sasa.

Tundu Lissu akishinda nafasi ya uenyekiti wa Taifa Chadema, hakika CCM itakuwa hoi bin taaban kiasi vijana wengi wanaweza kuanzisha uasi na kupelekea CCM kudhoofika.

Endapo Mbowe atagombea uenyekiti wa Taifa Chadema na akashinda, CCM itapata hoja za kuibeza Chadema na wale machawa wa Samia watapata nguvu na kuwapiku wote wanaotaka mabadiliko ndani ya CCM!
 
Ikitokea Mbowe akajitoa katika kinyang'anyiro cha kuwania tena kiti cha uenyekiti Taifa Chadema basi CCM itakuwa tumbo moto. Hii itawapa baadhi ya makada wa CCM kushinikiza fomu zaidi ya moja zitolewe kugombea uenyekiti wa Taifa CCM, kitendo ambacho kitatikisa umoja bandia unaoonekana hivi sasa.

Tundu Lissu akishinda nafasi ya uenyekiti wa Taifa Chadema, hakika CCM itakuwa hoi bin taaban kiasi vijana wengi wanaweza kuanzisha uasi na kupelekea CCM kudhoofika.

Endapo Mbowe atagombea uenyekiti wa Taifa Chadema na akashinda, CCM itapata hoja za kuibeza Chadema na wale machawa wa Samia watapata nguvu na kuwapiku wote wanaotaka mabadiliko ndani ya CCM!
Chadema ni imara kuliko ccm. Uimara ni kupendwa na raia
 
CCM haijawahi kuwa imara! Bila nafasi hii ya kushika dola na kuwa na Rais ingekwisha sambaratika zamani!
 
Upepo wa siasa ubadirika badirika ,wakati mwingine anayedhani yupo salama upepo wa kisulisuli cha siasa unaweza kumkumba.
 
Huu ndiyo ukweli kuwa Chadema ikisambaratika CCM itakuwa imara kuliko wakati wo wote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

Ikitokea Mbowe akajitoa katika kinyang'anyiro cha kuwania tena kiti cha uenyekiti Taifa Chadema basi CCM itakuwa tumbo moto. Hii itawapa nguvu baadhi ya makada wa CCM kushinikiza fomu zaidi ya moja zitolewe kugombea uenyekiti wa Taifa CCM, kitendo ambacho kitatikisa umoja bandia unaoonekana hivi sasa.

Tundu Lissu akishinda nafasi ya uenyekiti wa Taifa Chadema, hakika CCM itakuwa hoi bin taaban kiasi vijana wengi wanaweza kuanzisha uasi na kupelekea CCM kudhoofika.

Endapo Mbowe atagombea uenyekiti wa Taifa Chadema na akashinda, CCM itapata hoja za kuibeza Chadema na wale machawa wa Samia watapata nguvu na kuwapiku wote wanaotaka mabadiliko ndani ya CCM!
Lissu akiwa m/kiti CDM itasambaratika.
 
Baada ya Mbowe kuamua kugombea uenyekiti wa Taifa Chadema sasa wale waliokuwa wanamtaka kutoka CCM wameanza kuhoji umoja ndani ya Chadema!
 
Chadema ni moja kuliko vile mahasimu wao walitegemea kabla ya Uchaguzi.

CCM ni vipande vipande baada ya Samia kujiteua kuwania Urais. Hivi sasa inabidi vikundi vya kuhamasisha viingie kazini ili Samia akubalike. Uvccm, UWT, Wenyeviti wa mikoa na Wajumbe wa Halmashauri kuu wako kazini kushawishi Samia akubalike! Ikishindikana mabavu yatatumika ili mradi tu Samia apeperushe bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Kazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom