Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,361
- 63,976
Tumeshuhudia kanisa la mfalme Zumaridi, Word of Reconciliation Ministries (WRM) la anayejiita Nabii Suguye na Spirit Word Ministry la Ceasar Masisi yakifungiwa kwa sababu mbalimbali ambazo hasa zinahusu viongozi wake.
Kwanza, sikubaliani na utaratibu wa serikali kufungia makanisa bila amri ya mahakama.Imani ni kitu subjective sana, kuwapa watu wachache nguvu kubwa ya kufunga na kufungilia taasisi za kidini bila mchakato wa mahakama wa wazi sio sahihi kabisa.
Pili, kama makosa yanawahusu mfano viongozi wa kanisa kwa nini linafungiwa kanisa zima badala ya kushughulika na wahusika binafsi tu? Kama utaratibu huu utatumika sawa bila upendeleo kwa dini na madhehebu yote kuna ambalo halitafungiwa?
Kama tunataka taifa la haki kwa wote tuishi na maneno ya mwanafalsafa wa kale Voltaire aliyesema "Naweza nisikubaliane na yale unayosema ila nitaitetea hata kwa kifo haki yako ya kusema"