Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,638
- 4,239
Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya viongozi wa Afrika dhidi ya kutegemea sana misaada ya kigeni kufuatia uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump, wa kusitisha msaada wa shirikisho duniani kote.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Usalama wa Afya wa Kanda ya Afrika Mashariki 2025, Kenyatta alisisitiza kuwa nchi za Afrika zinapaswa kushirikiana kuunda mifumo ya kujitegemea ya kukusanya fedha kwa ajili ya kukabiliana na majanga.
Alibainisha kuwa utegemezi mkubwa mara nyingi huzuia maendeleo ya kiuchumi ya muda mrefu ya nchi, akisema kuwa huu ni ujumbe wa tahadhari kwa viongozi wa Afrika.
"Niliwaona baadhi ya watu juzi wakilia kwamba Trump ameondoa misaada. Hiyo siyo serikali yenu, wala nchi yenu, mnalia nini?" alihoji.
Halazimiki kuwapa chochote, nyie sio walipa kodi Marekani. Hii ni tahadhari tosha ili mjue mtajifanyia nini ili kujitegemea. Tushirikiane tumalizane na utegemezi."