PANTHERA LEO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2019
- 2,307
- 3,437
Habari Wanajamvi.
Natumaini mko poa.
Naomba serekali iweze kuangalia upya hawa watumishi WA UHAMIAJI pale wilaya ya mwanga kabla hawajaathiri watu wengi.
Baada ya kuzungushwa mda mrefu katika mchakato wa kupata KITAMBULISHO CHA NIDA, Siku ya tarehe 18 niliweza kuelekezwa kwenda ofisi za uhamiaji kama sehemu ya mchakato .
Nilipofika tu mlangoni ilikuwa hivi
Mimi; Habari? Hapa ni ofisi za uhamiaji?
Afisa 2; Ndio umekuja kufanyaje?
Mimi; Nimekuja kufatilia KITAMBULISHO hivyo nimeelekezwa hapa.
Afisa 2; Kwaiyo hujui hapa umekuja kufanya nini?
Mimi; Nadhani ni kwaajili ya ku "verify" Hizi nyaraka
Afisa 1; Ni nani huyo hajui kilichomleta hapa. Emb sogea kwanza umetokea wapi?
Mimi; Nimetokea............
Afisa 1; Kwanza wewe una elimu gani?
Mimi; nikamtajia elimu
Afisa 2; Wewe inaonekana muongo tupe hivyo viambatanishi
Nikawapa( cheti Cha kuzaliwa,Tin, leseni, barua ya mtendaji nk)
Afisa1; Mbona hapa hamna cheti Cha darasa la saba, wala namba ya NIDA ya mama yako alafu inaonesha wewe sio mtanzania maana wilaya walizotoka wazazi wako ni mipakani kwaiyo yawezekana wewe sio mtanzania.
Mimi; Mbona sikuambiwa nilete cheti Cha la saba siku zote Kila siku natajiwa Kimoja kimoja.
(Nikaomba nipige simu nyumbani Ile nitumiwe picha ya cheti)
Afisa1; Uhakikishe na Namba ya NIDA ya mama yako tunataka
Mimi; Mbona kama mnaniwekea ugumu kwani nimekosea wapi
Afisa 1 akachukua Ile fomu akapiga muhuri Kisha akasema "Wewe yaonekana mjeuri sasa hapa nimekuwekea alama huwezi pata namba ya NIDA adi nitake Mimi"
Mimi; Naomba mnieleweshe natakiwa kufanyaje
Afisa 2; Wewe unajifanya huelewi, unadharau kazi yetu.....
Afisa 2; ila ofisi yetu inakupenda ila unashindwa kuelewa tunataka nini. Kwanza unajua majukumu ya uhamiaji?
Afisa1; Sijui kafikaje hapa inaonekana huyu mtu amekimbia wilaya A amekuja huku wilaya ya mwanga Kuna mambo anafanya. Kwanza unataka NIDA ya kazi gani
Mimi; Mimi nataka kitambulisho TU nadhani ni haki ya Kila mtu
Afisa; Basi inaonekana Huna haraka nacho kwaiyo nenda siku ukiwa na haraka utajua Cha kufanya.
Siwezi kuandika yote hapa ila kuna wadada waliingia wao walijaribu kumwambia yule Afisa1. Amalizane na Mimi ila jamaa akagoma kwasababu anazo zijua yeye binafsi.
Kiukweli nimekata tamaa Hadi Mimi mwenyewe nimeanza kujihoji au usikute Mimi sio mtanzania kweli. Nilikuwa sidhani kama kupata utambulisho kutakuwa na mambo mengi kiasi hicho.
Naomba serekali iweze kuangalia upya hili swala, Hawa watu walinishambulia kwa maneno kama vile Mimi ni muhalifu ili watengeneza mazingira ya RUSHWA.