Uhai wa CHADEMA unategemea wa CCM

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
37,141
46,411
Ni jambo lililodhahiri kabisa kuwa Chadema haiwezi kusimama bila CCM kwakua uhai wake unautegemezi kwa asilimi nyingi uwepo wa CCM.

Hayo yanaonekana katika Maeneo yafuatayo;

Wanachama;

Mpaka sasa Chadema imekua ikiendelea kujipatia wanachama wake kwa kuwachukua toka CCM. Ni mara chache sana kuona wanachama wapya wakichukua kadi bila kuwa wanachama wa ccm kwanza.

Viongozi;

Viongozi wengi wa Chadema either walikuwa wanachama wa ccm au walikuwa viongozi ccm.

Hoja;

Hoja nyingi za Chadema zinatokana na mambo wanayoyafanya ccm, Chadema mpaka sasa wameshindwa kuibua hoja zisizotokana na maswala yaliyofanywa na ccm.

Kwakuwa maeneo yote muhimu katika uhai wa chama yanatokana na utegemezi basi ni wazi kabisa kwamba chama tegemezi kitaendelea kuwa hai kutegemea uhai wa kile inachokitegemea.

Kama Chadema haitajipambanua toka utegemezi wa CCM, bila shaka yoyote kitakufa tu kwakua hakitakua na mbinu za kujilinda endapo lolote litatokea.

Ni kichekesho pia kwa Chadema kuendelea kuota kuiondoa CCM wakati chenyewe kinaishi kwa kutegemea uhai wa CCM, Chadema ikiiondoa CCM na yenyewe inaondoka iko hivyo.
 
Nasubiri muandamane kumuunga mkono makonda kama kawaida yenu!

Ili tujue uvccm yote ni zero
 
Watalia na Kugaragara wakidhani Kuna Miujiza ya lowasa kuwa rais. Hilo hakiwezekani. Rais wa taifa letu ni John pombe Joseph magufuli 2015 - 2020. Subirini uchaguzi mkuu bado Muda kidogo.
 
Hebu kifuteni kwenye ramani ya dunia hiko chama chenu cha kijani muone kama CDM haiwezi kusimama na kuleta mabadiliko kwenye sector za maendeleo ya nchi na wananchi wake.

Ila Sizonje nahisi yeye ameleta mabadiliko ya utawala wa kimabavu na kusigina katiba ya JMT mengine ni wajibu hastahiki kusifiwa.
 
Umekaa kuanzia asubuhi mpaka saahizi ndo ulichoandika hiki.mzazi wako anahasara
 

Akili yako kama Debe tupu lisilo na mvumo.
 
Watalia na Kugaragara wakidhani Kuna Miujiza ya lowasa kuwa rais. Hilo hakiwezekani. Rais wa taifa letu ni John pombe Joseph magufuli 2015 - 2020. Subirini uchaguzi mkuu bado Muda kidogo.
Wanasahau kwamba uchaguzi umeshakwisha.
 
Kwa upinzani huu ambao unegeuza watu kama ajenda zao sidhani kama kinauwezo wa kusimama muda mrefu.
 

Tutolee kifaduro chako hapa.
 
Wewe hiyo biku unayolipwa huitendei haki. Ndo umepost nini sasa. Dah uvccm mmeishiwa thinking capacity
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…