Tugepalu Jr
Member
- Oct 13, 2022
- 17
- 19
Suala la ubovu na uchakavu wa miundombinu katika taasisi za kielimu zimekuwa kilio kikubwa kwa Watanzania wengi Tangu kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 mpaka kufikia sasa, hasa katika maeneo ya vijijini.
Kwa asilimia zaidi ya 60% mpaka 70% maeneo ya vijijini yanakubwa na uhaba wa madarasa ya kisasa pamoja na waalimu wa kutosha hasa waalimu wa Tasnia ya Sayansi na Hesabu. Hivyo kufanya baadhi ya ndoto za wanafunzi kupotea kwani wakiamini Sayansi ni kwaajili ya wanaosoma Mijini na watu wenye Uwezo flani.
Kwa Mfano katika Wilaya Mojawapo ambayo mimi nilipata Elimu yangu ya Kidato cha tano na Sita, shule ile ilikuwa na jumla ya Waalimu Kumi na Tisa (19) pekee. Na hapo shule inatoa huduma kuanzia Kidato cha kwanza hadi cha Sita ikiwa na wanafunzi zaidi ya Elfu moja (1000+), licha ya idadi ndogo ya waalimu pia shule haikuwa na Maabara kwa ajili ya wanafunzi waliokuwa wakisoma masomo ya Sayansi hivyo kuwalazimu majaribio yao yaliyohitaji uwepo wa maabara kufanyika katika mazingira hatarishi na yenye kuweza kuwaletea madhara.
Jambo hili la uhaba wa waalimu pamoja na ubovu wa miundombinu linachangia kwa kiasi kikubwa utoro wa wanafunzi mashuleni kwani mazingira hayaonyeshi kuwapa morali ya kuendelea kuwepo pale, Hivyo kuwafanya wanafunzi wengi kujiingiza katika michezo ya Kamari pamoja na kuchangia ndio za Utotoni kwa kiasi kikubwa.
Serikali kupitia Wizara yake husika walitazame jambo hili kwa jicho la Tatu ili kuweza kutatua matatizo haya ili wanafunzi wanaotokea Vijijini na wao pia kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao kwa kuwajengea miundombinu iliyo rafiki kwao pamoja na kuongeza idadi ya Waalimu katika mazingira ya vijijini hasa waalimu wa Sayansi na Hesabu.