Ugonjwa wa Virusi vya Marburg: Historia, Uambukizwaji, Dalili na Matibabu

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
577
2,594
Ugonjwa wa virusi vya Marburg, au zamani ukijulikana kama Homa ya kutokwa na damu inayosababishwa na Virusi vya Marburg ni ugonjwa hatari sana unaoweza kuambukiza binadamu na wanyama wengine.

BD73146B-FE25-49CB-BB9B-C183A8A2B206.jpeg

Husababishwa na maambukizi ya Virusi vya Marburg vyenye sifa ya RNA kutoka familia ya Filoviridae.

Virusi vya ugonjwa huu hupatikana katika familia moja na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola.

HISTORIA
Milipuko miwili mikubwa iliyotokea kwa wakati mmoja Marburg na Frankfurt huko Ujerumani, na huko Belgrade, Serbia, mnamo mwaka 1967, ilisababisha utambuzi wa kwanza wa ugonjwa huo.

Mlipuko huo ulihusishwa na kazi ya maabara kwa kutumia nyani wa Kiafrika (Cercopithecus aethiops) walioagizwa kutoka Uganda.

Baadae, milipuko na visa vingine vimeripotiwa nchini Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Afrika Kusini na Uganda.

Mnamo mwaka 2008, visa vingine viwili vya ugonjwa huu viriripotiwa kwa wasafiri huru waliotembelea pango linalokaliwa na makoloni ya popo wa Rousettus nchini Uganda.

NJIA ZA MAAMBUKIZI
Kwa mara ya kwanza, binadamu hupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa huu kutoka kwa wanyama hasa popo, kwa kula au kugusa mzoga wake.

Mara mtu anapopata maambukizi hayo kutoka kwa mnyama, maambukizi ya virusi vya ugonjwa huu kati ya binadamu na binadamu mwingine huanza kutokea kupitia mguso wa moja kwa moja.

Virusi vya Marburg vinaweza kupenya na kuingia mwilini kupitia sehemu za wazi kama vile vidonda, au kupitia ngozi laini za sehemu ya macho, midomi na pua kutoka kwenye;
  • Damu au majimaji ya mwili kama vile Mkojo, mate, jasho, choo, matapishi, maziwa na shahawa.
  • Vifaa vilivyoguswa na majimaji kutoka kwenye mwili wa mgonjwa, au mtu aliyefariki kwa ugonjwa huu kama vile matambara, nguo, shuka, viwembe pamoja na sindano.
  • Kwa kushiriki tendo la ndoa kwa namna yoyote na mwanamme aliyeambukizwa ugonjwa huu. Taarifa za kina kuhusu njia hii hazipo wazi sana, lakini inafahamika kuwa virusi vya Marburg huwa na uwezo wa kubaki kwenye korodani za mwanamme kwa siku kadhaa baada ya kupona kama ilivyo kwa virusi vya Ebola.
Kutokana na njia ambayo ugonjwa huu huambukizwa, wahudumu wa afya na watu wengine wanaohudumia wagonjwa na marehemu wenye changamoto hii ikiwemo ndugu huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na maambukizi.

DALILI
Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Marburg huanza ghafla kwa homa kali, maumivu makali ya kichwa pamoja na maumivu ya Maumivu ya misuli. Dalili zingine ni
  • Kuhara
  • Maumivu makali ya tumbo
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu ya kifua
  • Kuwasha kwa koo
  • Upele usiowasha
Wagonjwa wengi hupata udhihirisho mkubwa wa kutokwa na damu ndani ya siku 7 kwenye sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo machoni, kwenye ngozi, fizi, macho, uke pamoja na kujisaidia choo na mkojo wenye damu.

Mwonekano wa wagonjwa katika awamu hii hufafanuliwa kuwa huonesha “sifa zinazofanana mzimu" huku macho yakirudi ndani, uso ukikosa nuru na mwili mzima ukiwa na uchovu mkubwa.

Katika hatua mbaya za ugonjwa, homa huwa kubwa kiasi cha kuathiri mfumo wa kati a fahamu hivyo kusababisha kuchanganyikiwa, kuweweseka na ukorofi. Kwa wanaume, korodani zinaweza kuvimba.

Hatua ya mwisho inayoelekea kifo kawaida hutokea kati ya siku 8 na 9 baada kuambukizwa. Husababishwa na upotevu wa damu nyingi, kufeli wa ini pamoja na kusimama kufanya kazi kwa viungo muhimu vya mwili.

UCHUNGUZI WA KIMAABARA
Ni ngumu kutambua kirahisi pamoja na kutofautisha maambukizi ya ugonjwa huu na magonjwa mengine ya kuambukiza mfano Malaria, homa ya Matumbo (Typhoid), homa ya uti wa mgongo pamoja na homa zingine zinazosababishwa na virusi.

Njia zifuatazo zinaweza kufanyika kwenye maabara ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huu;
  • Antibody enzyme-linked immunosorbent assay (ELISA)
  • Antigen detection tests
  • Serum neutralization tests
  • Reverse-transcriptase polymerase chain reaction (RT-PCR) assay
  • Virus isolation by cell culture
KINGA
Pamoja na kuonekana mara chache sana kwa binadamu, ugonjwa huu unaweza kuambukiza kirahisi hasa kwa watumishi wa afya wanaohudumia wagonjwa pamoja na ndugu wa karibu wanaoishi na kutoa huduma kwa mtu mwenye ugonjwa huu.

Hivyo, namna nzuri ya kujikinga ni kuepuka ulaji/kukaa karibu na wanyama waliopo kwenye kundi la primates (Wanyama jamii ya nyani na sokwe) na popo ambao ndio hubeba sifa kubwa ya kuishi na virusi vya Marburg.

Aidha, watu wanaotoa huduma kwa mgonjwa wanapaswa kuvaa vifaa maalum vya kujikinga mfano gloves, gauni maalum na barakoa, kumtenga mgonjwa kwenye eneo lililodhibitiwa pamoja na kutakasa au kuangamiza kikamilifu masalia ya vifaa alivyotumia mgonjwa vyenye sifa ya kubeba vimelea ya ugonjwa.

MATIBABU
Ugonjwa huu hauna tiba ya moja kwa moja isipokuwa kushughulikia dalili zinazoonekana kwa wakati huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa virusi vya Marburg huwa na hadi 88% ya uwezekano wa kusababisha kifo.
 
Wana Jamii wenzangu,poleni na majukumu ya kila siku na muumba atupe nguvu ya kuendelea kupambana ya kila iitwayo leo.

Chukua tahadhari hizi zifuatazo juu ya kujikinga na kuepuka kueneza ugonjwa wa Malburg.View attachment 2561733View attachment 2561734View attachment 2561735

Sent using Jamii Forums mobile app

Huu ugonjwa wana udogosha kisiasa. Huu si covid. Mortality rate ya ya covid ilikuwa 2% huu ni above 90%.

Huu si wa kuamua wa kufa wafe na kuishi waishi. Huu si wa kufanyia usanii na ghiliba za vita vya kiuchumi.
 
Huu ugonjwa wana udogosha kisiasa. Huu si
covid. Morality rate ya ya covid ilikuwa 2% huu ni above 90%.

Huu si wa kuamua wa kufa wafe na kuishi waishi. Huu si wa kufanyia usanii na ghiliba za vita vya kiuchumi.
Mortality rather.
 
Wana Jamii wenzangu,poleni na majukumu ya kila siku na muumba atupe nguvu ya kuendelea kupambana ya kila iitwayo leo.

Chukua tahadhari hizi zifuatazo juu ya kujikinga na kuepuka kueneza ugonjwa wa Malburg.View attachment 2561733View attachment 2561734View attachment 2561735

Sent using Jamii Forums mobile app
HIyo title ungeandika hivi "Hakuna namna ya kujikinga na Marburg".
Hizo mamna ambazo huu ugonjwa unaambukizwa ndiyo maisha yetu ya kila siku, tusipokulana mate basi tutagusana kwenye mwendo kasi na daladala tu, bado tabia nyingine nyingi za mazoea na kipuuzi huko bara, kwenye betting na kuangalia mipira.
 
Maigizo yanaendelea

Daah, hakuna kupumzika yaanii!!!

Likiisha igizo moja linaingia igizo la pilii, ni bandika bandua

Episode ijayo : OMICRON OUTBREAK
 
Huu uzi ulitakiwa uwe juu pale uonekane ili watu wachukue tahadhari
 
Huu ugonjwa wana udogosha kisiasa. Huu si covid. Mortality rate ya ya covid ilikuwa 2% huu ni above 90%.

Huu si wa kuamua wa kufa wafe na kuishi waishi. Huu si wa kufanyia usanii na ghiliba za vita vya kiuchumi.
Serikali imejitahidi. Ile tu ku-acknowledge upo ni hatua sahihi. Kazi kwetu wananchi kuchukua tahadhari ili kupunguza kusambaa kwa ugonjwa
 
TIME LINE YA UGONJWA WA MARBURG DUNIANI
MwakaNchiUgonjwa ulipotokeaRipoti ya idadi ya wagonjwaIdadi ya vifo(%)Kilichotokea
2023TanzaniaMkoa wa Kagera
8​
5(63%)March 21, 2023, Maofisa wa serikali ya Tanzania watangaza mlipuko kwa mara ya kwanza nchini wa ugonjwa wa Marburg.Tukio hili limetangazwa sehemu ya Kagera ambapo ni kaskazini magharibi mwa nchi.Habari za kupatikana au kusambaa kwa ugonjwa bado hazijatolewa.
2023Equatorial GuineaJimbo la Kie-Ntem
9​
7(78%)February 13, 2023,maofisa wa serikali ya Equatorial Guinea watangaza mlipuko wa Maburg.Wizara ya afya mwanzoni ilithibitisha kesi moja na kesi nyingine ikaongezeka kutoka jimbo la Kie-Ntem kaskazini mashariki mwa nchi hiyo hadi sasa hakuna taarifa zaidi
2022GhanaMkoa wa Ashanti
3​
2(67%)Tuko la kutisha la Maburg lilitokea mkoa wa Ashanti July 2022.Lakini mwanzoni ugonjwa huu ulionekana kwenye maabara ya taifa na ukathibitishwa zaidi kwenye taasisi ya Pasteur mjini Dakar Senegal na kufanya ugonjwa huu kuonekana Ghana kwa mara ya kwanza.Muda mfupi tu baadae watu wawili wa familia moja walionekana na ugonjwa huo hakukuwa na tukio lingine tena lilitokea nje ya familia hiyo.Ugonjwa huo ulitangazwa kutoweka September mwezi huo huo.
2021GuineaGuéckédou
1​
1(50%)Kesi moja iliripotiwa na kuthibitishwa na wizara ya afya ya Guinea kwa mgonjwa ambayo aligundulika nao baada ya kufariki.Hakuna kesi nyingine iliyothibitishwa baada ya cases 170 zilizoonekana zilikuwa karibu na ugonjwa kufuatiliwa kwa siku 21
2017UgandaKween
4​
3(75%)Sampuli ya damu kutoka wilaya ya Kween mashariki mwa Uganda iliionyesha positive virusi vya Marburg.Ndani ya masaa 24 ya uthibitisho mpasuko wa ugonjwa wa haraka ukatokea.
2014UgandaKampala1*
1​
Kwa ujumla wake,case moja ilithibitishwa(mbaya) na watu waliokaribu na ugonjwa 197 walifuatiliwa kwa wiki 3.Kati ya hawa 197, 8 walionyesha dalili zinazofanana na Marburg, lakini wote walionekana negative
2012UgandaKabale
15​
4(27%)Majaribio katika CDC/UVRI yalionyesha mpasuko wa ugonjwa katika wilaya za Kabale, Ibanda, Mbarara, na Kampala katika kipindi cha zaidi ya wiki 3
2008Raia wa Uhonzi aliyekuwa UgandaPango la msitu wa Maramagambo huko Uganda, kwenye ukingo wa mbuga za wanyama za malkia Elizabeth
1​
1 (100%)Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 wa kidachi ambaye alikuwa na historia za kusafiri Uganda alilazwa hospitali huko kwao Uholanzi.Siku 3 baada ya kulazwa akasikia dalili za homa na kutetemeaka,ikifuatiwa na kudhoofika kiafya.Mwanamke huyo alifariki siku 10 baada ya kulazwa.
2008Raia wa Marekani aliyekuwa UgandaPango la msitu wa Maramagambo huko Uganda, kwenye ukingo wa mbuga za wanyama za malkia Elizabeth
1​
0 (0)Msafiri wa Marekani alirudi kwao akitokea Uganda January 2008. Mgonjwa alionyesha ugonjwa kwa siku 4 baada ya kurudi,alilazwa,na kuruhusiwa kuhakika alionekana kuwa na ugonjwa wa Marburg.
2007UgandaMgodi wa madini ya risasi na dhahabu katika wilaya ya Kamwenge
4​
1 (25%)Mpasuko mdogo wa ugonjwa ulitokea kwa matukio ma 4 ya vijana wa kiume waliokuwa wanafanya kazi mgodini,hadi leo hakuna tukio lingine limetokea
2004 hadi 2005AngolaJimbo la Uige, Angola
252​
227 (90%)Mpasuko ulitokea jimbo la UIGE October 2004.Matukio mengine yaligunduliwa yakiunganishwa na ugonjwa huo moja kwa moja
1998 hadi 2000Democratic Republic of Congo (DRC)Durba, DRC
154​
128 (83%)Matukio mengi yalionekana kwa vijana wakiume katika mgodi wa dhahabu wa Durba,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo,ambapo ndio palionekana ugonjwa huo umeshamiri.Matukio mengine yaliionekana kijiji jirani cha Watsa
1990UrusiUrusi
1​
1 (100%)Maambukizi yalitokea maabara yakaua mfanyakazi mmoja
1987KenyaKenya
1​
1 (100%)Kijana wa Denmark mwenye umri wa miaka15 alilazwa akiwa na historia ya siku tatu ya kuumwa kichwa, uchovu,homa na kutapika.Siku 9 kabala ya dalili,alitembelea mapango ya Kitum mlima Elgon mbuga za wanyama.Pamoja na juhudi kubwa za kumsaidia mgonjwa alifariki siku ya 5 hakuna matukio mengine tena yaliendelea.
1980KenyaKenya
2​
1 (50%)Katika pango la Kitum mbuga za wanyama za mlima Elgon.Pamoja na uangalizi maalum akiwa Nairobi mgonjwa alifariki daktari aliyekuwa anampa huduma ya kupumua naye alipata dalili siku9 baadae lakini akapona siku 4 baadae
1975Johannesburg, South AfricaZimbabwe
3​
1 (33%)Msafiri alikuwa amesafiri muda si mrefu kwenda Zimbabwe na akalazwa hospitali nchini Afrika kusini.Maambukizi yalikwenda kwa abira mwenzake na nurse aliyekuwa anamhudumia.Msafiri huyo alifariki lakini huyu msafiri jirani yake na nurse walipona baada ya kupatiwa matibabu ya hali ya juu.
1967Germany and YugoslaviaUganda
31​
7 (23%)Matukio ya pamoja yalitokea kwa wafanyakazi wa maabara ambao walikuwa wanafanya kazi kuwahudumia nyani wa kijani walioingizwa kutoka Uganda.Kwa nyongeza zaidi pamoja na matukio 31 kutangazwa kuna cases nyingine ziligunduliwa kwenye vipimo vya damu kwa wanyama wanyama hao.
* maana yake ni tukio lililothibitishwa na maabara peke yake
 
Back
Top Bottom