Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Chuo kikuu cha Oxford kimekamilisha jaribio la kwanza la uchunguzi wa kitabibu kuhusu ufanisi wa chanjo mpya ya ugonjwa wa Malaria iliyopewa jina la R21/Matrix-M.
Kwa mujibu wa chapisho la uchunguzi huu lilolotolewa kwenye Jarida la The Lancet, chanjo hii inaweza kutengeneza kingamwili zenye uwezo wa kuzuia mashambulizi ya vimelea vya ugonjwa wa Malaria kwa hadi asilimia 80.
Ikiwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) litajiridhisha kuwa chanjo hii ni salama na inao ufanisi wa kutosha kupambana na ugonjwa wa Malaria, litaiidhinisha hapo baadae mwaka kesho baada ya kukamilika kwa jaribio la mwisho la ufanisi wake.
R21/Matrix-M inatajwa kuwa na gharama nafuu, itapunguza vifo kwa asilimia 70 ifikiapo mwaka 2030 na itaufuta kabisa ugonjwa huu ifikiapo mwaka 2040.
Mwishoni mwa mwaka 2021, WHO iliidhinisha matumizi ya chanjo ya RTS,S/AS01 kusini mwa Jangwa la Sahara ili kuleta ahueni ya ugonjwa wa Malaria ambao zaidi ya asilimia 75 ya visa vyote duniani hutokea huko.