Ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa (Osteoporosis).
-Ugonjwa huu hufanya mifupa iwe dhaifu, ipungue ujazo wake na iwe kwenye hatari kubwa ya kuvunjika kirahisi pasipo kuhitaji mgandamizo mkubwa.
Dalili muhimu za ugonjwa huu
-ni kupatwa na maumivu ya mara kwa mara ya mifupa, hasa sehemu ya mgongo, kupungua kwa urefu au kupinda kwa mwili pamoja na kuvunjika kirahisi kwa mifupa.
Sababu za ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa
Tatizo hili linaloonekana zaidi kwenye mifupa ya maungio ya mkono, miguu, uti wa mgongo na nyonga huchangiwa na uwepo wa sababu nyingi.
Baadhi yake ni-
▪️Mabadiliko ya homoni za mwili yanayochangiwa na kufikia umri wa ukomo wa hedhi.
▪️Uchache wa madini ya calcium na Vitamini D.
▪️Matumizi makubwa ya baadhi ya dawa, hasa zile za corticosteroid.
▪️Unywaji mkubwa wa pombe.
▪️Uvutaji wa sigara.
▪️Kutokufanya mazoezi.
▪️Matatizo kwenye tezi za thyroid.
-Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote, lakini wanawake wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata kuliko wanaume.
*Kinga ya Ugonjwa huu *
Unaweza kujikinga na Ugonjwa huu wa kudhoofu kwa mifupa kwa kufanya mambo yafuatayo-
-Kutumia walau miligrams 1000 za madini ya calcium kila siku.
-Kuongeza matumizi ya Vitamini D. Huusaidia mwili kwenye kufyonza vizuri madini ya calcium.
-Fanya mazoezi.
-Punguza unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara.