Ugonjwa wa EBOLA: Asili, Dalili, Usambaaji na Kinga dhidi yake

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,278
UGONJWA WA EBOLA ULIANZA VIPI NA WAPI?

Ebola Virus Disease - EVD (Ugonjwa wa Virusi vya #Ebola) awali ulijulikana kama Ebola haemorrhagic Fever. Ni ugonjwa wenye madhara makubwa kwa Binadamu ikiwamo kusababisha kifo ikiwa haujatibiwa

Ebola kwa mara ya kwanza ilionekana mwaka 1976 katika milipuko miwili ya pamoja iliyotokea huko Nzara, Sudani Kusini na huko Yambuku, DRC katika Kijiji cha karibu na mto Ebola ambapo jina la Ugonjwa lilizaliwa

Mlipuko mkubwa wa Ebola tangu kugundulika kwake, ulitokea Afrika ya Magharibi mwaka 2014 - 2016. Ulianzia Guinea na kuvuka mipaka kusambaa hadi Sierra Leone na Liberia. Katika mlipuko huo kulikuwa na Wagonjwa na Vifo vingi kuliko jumla ya kwenye milipuko mingine yote kwa pamoja ya awali

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha Wastani cha vifo vya Wagonjwa wa #Ebola kinakaribia asilimia 50. Hata hivyo, viwango vya vifo vya Wagonjwa katika milipuko iliyopita vimetofautiana kutoka 25% hadi 90%

AINA YA VIRUSI VYA EBOLA

Virusi vya Ebola (EbolaVirus) vipo katika familia ya virusi ya Filoviridae. Familia hii pia ina Virusi vingine vya Cuevavirus na Marburgvirus

Virusi vya Ebola vipo vya aina 6 tofauti; Zaire, Bundibugyo, Sudan, Taï Forest, Reston na Bombali

DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA

Dalili za Ugonjwa wa Ebola zinaweza kuanza kuonekana kwa Binadamu katika kipindi cha siku 2 hadi 21 tangu kupata maambukizi. Dalili hizo zinaweza kuwa za ghafla na zinajumisha Homa, Uchovu, Maumivu ya Misuli, Maumivu ya Kichwa, na Kuwashwa Koo

Dalili hizo zinafuatiwa na Kutapika, Kuharisha, Upele, Dalili za Figo au Ini kushindwa kazi, na muda mwingine kuvuja damu ndani na nje ya mwili. Mtu aliyeambukizwa Virusi vya Ebola hawezi kueneza ugonjwa huo hadi apate dalili zake

Kitabibu inaweza kuwa ngumu kutofautisha #Ebola na magonjwa mengine ya kuambukiza kama Malaria, Homa ya Tumbo na Homa ya Uti wa Mgongo. Katika upimaji, Matokeo ya kimaabara yanajumuisha Kupungua kwa Chembechembe Nyeupe za Damu na Kuongezeka kwa vimeng'enya vya Ini

NAMNA VIRUSI VYA EBOLA VINAVYOSAMBAA

Kwa mujibu wa WHO, inadhaniwa Wanyama - 'Fruit Bats' wa familia ya 'Pteropodidae' wana asili ya kubeba EbolaVirus. Binadamu alipata Ebola kwa kugusana kwa karibu na Damu, Majimaji au Vimiminika vingine vya Wanyama wenye virusi hivyo

Ebola husambaa kutoka kwa Binadamu mmoja kwenda mwingine kupitia kugusana kwa karibu na Damu au majimaji ya mwili wa mtu mgonjwa au aliyefariki na Ebola. Njia nyingine ni kugusana na Vitu vilivyopata majimaji ya mwili (Kama vile Damu, Kinyesi, Matapishi) wa Mgonjwa au mtu aliyefariki na Ebola

Wajawazito wanaopata Ebola na kupona bado wanaweza kubeba EbolaVirus kwenye maziwa au vimiminika na tishu zinazohusiana na ujauzito. Ikiwa Mwanamke anayenyonyesha anapona Ebola na kutaka kuendelea kunyonyesha, inabidi maziwa yake yapimwe

Watu wana uwezo wa kuendelea kuambukiza Ebola mradi tu damu yao bado ina #EbolaVirus. Sherehe za maziko zinazohusisha ugusaji wa moja kwa moja wa mwili wa Marehemu aliyefariki kwa Ebola zinaweza pia kuchangia katika maambukizi

NAMNA YA KUJIKINGA NA KUDHIBITI EBOLA

Udhibiti wa Ebola unategemea Usimamizi wa Maambukizi, Ufuatiliaji wa Waliogusana na wenye virusi vya Ebola, Huduma nzuri ya Maabara na Mazishi Salama. Ushirikiano wa Jamii ni muhimu katika kudhibiti kwa mafanikio #EbolaOutbreak

Mazishi salama, Kutambua watu wanaoweza kuwa wamegusana na Mtu mwenye virus vya Ebola na kufuatilia afya zao kwa siku 21 ni hatua za kuzuia mlipuko wa Ugonjwa huo. Pia, Muhimu kutenganisha Watu wazima na Wagonjwa na kudumisha usafi na mazingira safi ili kuzuia kuenea zaidi

Jamii yatakiwa kupunguza hatari ya maambukizi ya Ebola kutoka kwa Wanyamapori (Kama Nyani, Tumbili na 'Fruit Bat') hadi kwa binadamu kwa kugusana. Unapobeba Wanyama tumia 'glove' na nguo nyingine zinazofaa za kinga. Damu na nyama zinapaswa kupikwa vema kabla ya matumizi

Jamii inatakiwa kuacha mgusano wa moja kwa moja au wa karibu na Watu wenye dalili za Ebola. Wakati wa kutunza Wagonjwa 'gloves' na vifaa vya kinga vinafaa kuvaliwa. Pia, muhimu kunawa mikono mara baada ya kutembelea Wagonjwa hospitalini au baada ya kuwahudumia nyumbani

UHUSIANO WA EBOLA NA KUJAMIIANA

WHO yapendekeza Wanaume wanaopona Ebola kufanya ngono salama na kwa usafi kwa miezi 12 tangu waoneshe dalili au hadi shahawa zao zitakapopimwa mara 2 kuwa hazina Virus vya Ebola. Wanaume waliopona wanapaswa kupimwa shahawa kila miezi 3 baada ya dalili za Ebola kuonekana. Zikiwa na Virusi hivyo zitapima kila mwezi hadi zitakapothibitika hazina virusi mara mbili

Baada ya tendo, mnapaswa kujisafisha na kunawa mikono mara moja kwa maji tiririka baada ya kugusana na majimaji yoyote yaliyotokwa kwa mwenzako

USAMBAAJI WA EBOLA KWA WAJAWAZITO NA WANAONYONYESHA

Wajawazito wanaopata #Ebola na kupona bado wanaweza kubeba #EbolaVirus kwenye maziwa au vimiminika na tishu zinazohusiana na ujauzito. Ikiwa mama mwenye mtoto atahisiwa au kuthibitika kuwa Ebola anapaswa kuacha kunyonyesha mara moja

Mtoto anapaswa kutengwa kutoka kwa mama yake na kupewa mbadala wa maziwa ya mama kama inahitajika. Ikiwa Mwanamke anayenyonyesha anapona Ebola na kutaka kuendelea kunyonyesha, inabidi maziwa yake yapimwe kwanza

ATHARI ANAZOWEZA KUPATA MTU ALIYEPONA EBOLA

Matatizo kadhaa ya kiafya yameripotiwa kwa watu waliopona #Ebola yakiwemo ya afya ya akili. Waliopona ugonjwa huu wanahitaji usaidizi mzuri wa Kiafya na Kisaikolojia, pia katika kupunguza hatari ya maambukizi ya #EbolaVirus
 
UGONJWA WA EBOLA ULIANZA VIPI NA WAPI?

Ebola Virus Disease - EVD (Ugonjwa wa Virusi vya #Ebola) awali ulijulikana kama Ebola haemorrhagic Fever. Ni ugonjwa wenye madhara makubwa kwa Binadamu ikiwamo kuababisha kifo ikiwa haujatibiwa

Akuna kitu ni propaganda tu
 
Hii story ya ebola sijui iliishiaga wapi? 😁 😁
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom