Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,051
Imetolewa taarifa na wizara ya Afya na Profesa Tumaini Nagu kuwa huko Bukoba vijijini, katika Kata ya Maruku na Kanyangereko, kumetokea ugonjwa usiojulikana, ambao dalili zake ni kutoka damu mfululizo, kwenye sehemu mbalimbali, ikiwemo puani, hadi Figo zinazshindwa kufanya kazi, uliosababisha raia 5 kupoteza maisha.
Dalili hizo zilizotajwa ni kama dalili za ugonjwa wa Ebola.
Swali ninalojiuliza ni hili, hivi inawezskanaje wizara ya Afya, ituambie ni ugonjwa usiojulikana, ilihali wanajua kuwa ni ugonjwa wa Ebola?
Nchi jirani za Jamhuri ya Congo na Uganda, ulipolipuka ugonjwa huo na kuua watu kadhaa, hawakuficha na kueleza kuwa nchi hizo zimekumbwa na ugonjwa wa Ebola.
Ni sababu zipi zinazosababisha nchi yetu isitaje kuwa ugonjwa huo inaodai ni ugonjwa usiojulikana ni Ebola?
Lazima wizara ya Afya watambue kuwa ugonjwa huo wa Ebola ni ugonjwa hatari Sana unaoweza kuchukua maisha ya watu wengi Sana.
Niwatahadhirishe wizara ya Afya kuwa Kuna msemo wa kiswahili unaosema, MFICHA MARADHI, MWISHO KILIO KITAMWUBUA.
Je, wizara yetu ya Afya, imeamua kuficha ugonjwa huo ulioingia nchini, Ili KILIO KIJE KUTUUMBUA?