Ndugu watanzania na serikali yetu kwa ujumla,
Mwaka jana kuliibuka ugonjwa ulioathiri baadhi ya mazao sehemu mbali mbali mbali nchini( Arusha Morogoro, Tanga, Iringa na njombe) na uliathiri zaidi mahindi na mboga mboga (nyanya, Hoho, Vitunguu). Ugonjwa huu uliwashtua wengi maana inasadikika ni Viral disease (virus) na kwa kawaida ugonjwa wa virus hauna tiba zaidi ya kung'oa mmea. Ugonjwa huu kwa sababu ulikua ni mgeni ulipewa jina KANTANGAZE.
Uchunguzi wangu mdogo nilioufanya unasema ugonjwa huu ni matokeo ya vita ya kimasoko ya mbegu nchini. Kuna kampuni tayari inayombegu inakinzana na ugonjwa huu na inalengo la kutaka kuyanunua makampuni mengine makubwa yaliyopo nchini ili aweze kudominate soko.
Kampuni inayohusishwa ni kampuni kubwa inayojihusisha na uuzaji wa mbegu za GMO (Genetically modified Organism) duniani na Kuna baadhi ya nchi imeshapigwa marufuku.
Lengo la uzi huu ni kutaka kutoa taarifa kwa mamlaka husika kufuatilia ukweli maana nimepata taarifa kwa makampuni pinzani, baadhi ya watalaamu wa kilimo na wadau kwenye sector ya kilimo. Hivyo serikali kupitia kitengo chake cha ufuatiliaji wa mbegu mbali mbali kufanya utafiti kubaini ukweli na mwisho kuwatoa wananchi hofu.