Uganda yazuia wafanyakazi kwenda Saudi Arabia

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,314
Serikali ya Kampala imesema kuwa itaacha kupeleka raia wake kufanya kazi za ndani nchini humo kutokana na ripoti za karibuni za wafanyakazi kunyanyaswa nchini humo.

Marufuku hiyo itadumu hadi pale Serikali ya Uganda itakapojiridhisha kuwa mazingira ya kufanya kazi nchini ni salama na yanayofaa, hivyo kusitisha makubaliano ya Julai mwaka jana kati ya Serikali za Saudia na Uganda za kubadilishana wafanyakazi.

Ripoti za wafanyakazi wa mbari zingine kutoka mataifa tofauti kunyanyaswa, kufungwa na wakati mwingine kuuwawa wakiwa chini ya uangalizi wa polisi nchini Saudia na mataifa mengine ya Ghuba zimekuwa nyingi siku za karibuni hivyo kupelekea mataifa mengine kama Ufilipino na Indonesia kuweka marufuku kama hiyo.
Chanzo: Reuters
 
Naona wasaudia weusi wako bize kupangua thread kuhusu ubaguzi wa nchi yao. Ngoja wagundue umeleta na uzi huu tena, utaogaje matusi!? Utadhani wewe ndiye serikali ya Uganda, subiri uone!!
 
Dahhhh
Kuna story moja nilisoma wa dada mmoja Mkenya alikuwa mfanya Kazi wa ndani huko Saudi .

Ilinisisimua mno na kumuonea huruma sana.
Bora mtu uishi kwenye umaskini kuliko vile.

Yaani cha kwanza kabisa alipofika akanyang'anywa passport.

Dahhhh Mungu atusaidie Waafrica.
 
kuna wadada kutoka Kondoa na kwingineko inasemekana walipelekwa huko na mbunge mmoja wa nchi hii mwenye tamaa ya utajiri , hebu tujulisheni hali zao .
 
Ndugu kuna dada wawili wenyeji wa Dodoma walikuwa huku maeneo ya Kahama mmoja alikuwa na ameolewa na mwingine single. Huyu mwenye mme wakakorofishana na mmewe na kuvunja ndoa. Miezi kama mitatu imepita ndugu yao akaja dukani mke wangu akamuuliza mbona wateja wangu siwaoni? Akamjibu wako Oman kufanya kazi za ndani walitafutiwa na Agent aliyeko Dar. Walipofika tu wakawapigia simu na tangia siku hiyo hakuna mawasiliano tena. Uzi huu umenikumbusha namna gani jinsi mwanamme alivyokuwa anampenda yule dada pamoja na vituko vyake kwenye ndoa. Kaenda Oman na kuacha mtoto wa mwaka mmoja na miezi minne kwa mama yake. Nawaombea mungu yasiwafike matatizo yoyote huko.
 
Mmoja wa ma-agent alikuwa Mtemvu!
 
Ondoa hofu ubalozi wetu OMAN upo active Sana,umeshawarudisha wengi tuu waliotaka kurudi
Kisha Omani kiswahili na Waswahili nje nje
 
Tetesi:Kabla ya kuondoka unafanyiwa vipimo vya afya,ikiwemo ukimwi, hep b,blood grouping,nk. Wengi wanapotea,kuwa cadaveric organ donors kama moyo,figo,ini. Wengine kama guinea pigs,kutumika kwa utafiti wa tiba.
 

Kwa kweli story zinazotoka huko si njema kabisa.
Na wengine wanakuja na evidence kabisa.
Ni kuwaombea tu kwakweli.

Tukae tukijua si kila mtu duniani ni mwema.
Na uhakika huko kuna watu wema na wanawatunza wafanyakzi wao .
Na kuna wengine ni hivyo tena.
 
Miaka yote mwarabu anaamini mswahili ni mtu wa wake
Saudi Arabia na nchi zingine as ghuba wananyanyasa sana wafanyakazi hasa weusi na hauna pa kwenda kushtaki mana police wao bora mara10 ya wale wa India
 
Kila sehemu ina watu wabaya na wazuri.

Hata tanzania pia tunashuhudia sana wafanya kazi wakinyanyaswa hadi kufikia kuchomwa na pasi!
 
Wewe umechokoza matusi kutoka kwa wasaudia waliozaliwa bongo na kukulia bongo .watafia bongo ila wanaifaham saudi arabia kuliko aliyeishi huko. hawa ni weusi kama mkaaa ila wanaamini wana uraia na ni wazalendo sana wa saudi arabia. watakutukana hapa na kukwambia "MBONA SIJUI WAPI NAKO WANABAGUA" kana kwamba ubaguzi ni jambo jema kabisa kufanyika hapa duniani.
 
kuna wadada kutoka Kondoa na kwingineko inasemekana walipelekwa huko na mbunge mmoja wa nchi hii mwenye tamaa ya utajiri , hebu tujulisheni hali zao .

Sita wamesharudi, mmoja ana kovu la kuunguzwa na pasi kwenye paja. Hao watano wamefanyiwa mambo ya kinyama kabisa ikiwemo kuingiliwa sehemu ya haja kubwa.
Muda si mrefu nitaleta uzi hapa mara baada ya kupata idhini ya wahusika.
Kazi walizokuwa wanafanya ni kuhudumia wazeee wasiojiweza, hii inahusisha hata kuwasafisha wanapojisaidia.
Kutimiza tamaa za ndugu na jamaa wa bosi ikiwemo ngono ya lazima(kubakwa) na kuwekwa mahali pachafu na kuzuiwa kutembea na kuwasiliana na watanzania wenzako.
Wengi wanakufa na kuzikwa huko huko.
Uarabuni kwa wafanyakazi wa ndani ni Jehana ndogo.
 
yupo muangalie kule fb mi nachat nae sana tu, ila ana majina mawili sijui jina lake halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…