ufunguzi wa Kituo cha Afya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,091
727
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema, dhamira njema ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuipa kipaumbele Sekta ya Afya nchini ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uhakika za matibabu bila kuzifuata nje ya nchi.

"Vission yake ni kwamba wasitoke wagonjwa kutoka Zanzibar kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Watatibiwa hapa hapa, huo ndiyo muono wake;

Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Afya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

"Mbali ya kutoa neno moja kutoka Muungano, naomba nichukue fursa hii, Mheshimiwa kukujulisha kwamba mimi nilishirikishwa katika initiative hii ya Samia Foundation.

"Na ninaomba niwaambie wananchi na hasa kwa Wizara ya Afya kupitia Mheshimiwa Nassor Mazurui ambaye naye anaifahamu vission ya Mama Samia kwa Zanzibar na Sekta ya Afya na hapa Kizimkazi.

"Katika vission hiyo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete tulitumwa pia kwenda kuangalia pale Jakaya Kikwete Cardiac Institute kuangalia mifumo yao.

"Kwa hiyo naomba niseme hii ni asilimia ndogo sana ya Mama Samia Foundation na hiki Kituo cha Kizimkazi, muundo wake na vission yake ninaweza kusema ni kubwa zaidi.

"Ninaweza kusema ni chini ya asilimia ya asilimia 10 sasa hivi, lakini muundo na vission yake ni kubwa zaidi."

Pia, amempongeza Mhandisi ...kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Samia Foundation.

Amesema, uteuzi wake utamsaidia Rais Dkt. Samia kutafsri ndoto yake pana kama alivyoweza kufanya Dkt.Jakaya Kikwete na leo wagonjwa wengi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapata huduma zao Dar es Salaam bila kwenda nje ya nchi.

Pia, amempongeza Rais Dkt.Samia kwa kuweka msukumo mkubwa katika upatikanaji wa nishati ya uhakika, hatua ambayo imeungwa mkono na viongozi wengi ndani na nje ya Afrika.
 

Attachments

  • IMG-20250104-WA0098.jpg
    IMG-20250104-WA0098.jpg
    641.8 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0086.jpg
    IMG-20250104-WA0086.jpg
    936.2 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0099.jpg
    IMG-20250104-WA0099.jpg
    734.1 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0100.jpg
    IMG-20250104-WA0100.jpg
    953.6 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0101.jpg
    IMG-20250104-WA0101.jpg
    634.8 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0102.jpg
    IMG-20250104-WA0102.jpg
    1.1 MB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0103.jpg
    IMG-20250104-WA0103.jpg
    1 MB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0104.jpg
    IMG-20250104-WA0104.jpg
    918.1 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0105.jpg
    IMG-20250104-WA0105.jpg
    961.9 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0106.jpg
    IMG-20250104-WA0106.jpg
    997.5 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0087.jpg
    IMG-20250104-WA0087.jpg
    801.7 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0088.jpg
    IMG-20250104-WA0088.jpg
    856.6 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0097.jpg
    IMG-20250104-WA0097.jpg
    1.2 MB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0096.jpg
    IMG-20250104-WA0096.jpg
    414.3 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0095.jpg
    IMG-20250104-WA0095.jpg
    578.9 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0094.jpg
    IMG-20250104-WA0094.jpg
    448 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0093.jpg
    IMG-20250104-WA0093.jpg
    1.3 MB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0092.jpg
    IMG-20250104-WA0092.jpg
    1 MB · Views: 2
  • IMG-20250104-WA0091.jpg
    IMG-20250104-WA0091.jpg
    967.7 KB · Views: 2
  • IMG-20250104-WA0090.jpg
    IMG-20250104-WA0090.jpg
    773.6 KB · Views: 1
  • IMG-20250104-WA0089.jpg
    IMG-20250104-WA0089.jpg
    740.9 KB · Views: 1
Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Afya Kizimkazi Wilaya ya Kusini Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Hizi Kizmkazi ziko ngapi huko visiwani
 
Kituo cha afya, mtu kwao kila kiongozi kuanzia Chato na sasa Kizimkazi wanapeleka rasilimali nyingi kwao.

Tofauti na yule wa Bagamoyo, Masasi Mkuranga na Butiama.

Kituo hiki cha Kusini Unguja Kizimkazi kimejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, wakiwemo Samia Foundation, Foundation for Humanitarian Initiatives ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Benki ya NBC, pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1735999561837.jpeg

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, akikata utepe kuzindua Kituo kipya cha Afya Kizimkazi, katika Wilaya ya Kusini Unguja, January 4, 2025. Kushoto kwake ni Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahamoud na wa pili kushoto ni Mama Salma Kikwete
1735999391772.jpeg

Picha : Kituo cha Afya Kizimkazi Kusini Unguja Zanzibar.


Kutoka Maktaba :
27 Agosti 2023
Kizimkazi, Unguja Kusini
Zanzibar

SERA YA BENKI YA NBC KURUDISHA KWENYE JAMII YATIA MKONO WAKE KIZIMKAZI
Mradi huo wenye thamani ya sh bilioni 4.4 ambapo benki ya NBC imechangia kiasi cha Sh milioni 400, Rais Samia pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa hatua hiyo muhimu, alisema huo ni adhma ya serikali kuboresha huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya kwenye maeneo mbalimbali kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika maeneo hayo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=DFugy57bCh4
 
Back
Top Bottom