Kuna mwanasiasa mmoja kule Russia anaitwa Zhirinovsky, ni mbaguzi wa rangi, miaka ya 90 aliwahi kusema "sayansi inapiga hatua wakati mtu mweusi anaendelea kucheza muziki". Ilikuwa ni kejeli iliyowakera waafrika wengi lakini ujumbe ulifika. Napozitazama akili za kitanzania najikuta nikiuona kweli fulani ndani ya kauli za kibaguzi za mrusi yule. Unapolilia uonyeshwe live bunge muda wa mchana maana yake ni kwamba kama wewe ni muajiriwa basi unamuibia muda wa kazi yule aliyekuajiri kwa kufuatilia bunge wakati akili yako ilipaswa kufikiria kazi. Cha kushangaza ni kwamba baadhi ya mambo yanayoonekana live ni ule utambulisho wa ndugu za wabunge wanaokwenda Dodoma, mimi kama mlipa kodi nafaidika vipi kwa kumjua mtoto, housegirl, houseboy wa mbunge fulani?. Tuna safari ndefu sana.