Ufugaji wa Bata: Aina za bata, ujuzi, gharama, changamoto, faida na masoko

Raia Mtata

JF-Expert Member
Feb 4, 2017
316
610
UTANGULIZI

Habari zenu wanajamvi, kwanza napenda kudeclare interest mimi ni mfugaji mchanga wa Bata, na nilifikia uamuzi wa kufuga bata baada ya maradhi kuwapiga kuku wangu na wakafa wote. Nimepitia threads nyingi sana za humu na sijaona special thread inayoongelea bata na bila hiyana nimemua kuileta ili wafugaji bata na wataalam tukutane hapa kupeana ujuzi. Bata ni ndege mtamu nadhani kushinda hata kuku, watu wengi wanapenda kumla bata ila hawataki kabisa kumfuga kutokana na mazingira yake. Ufugaji wa bata una faida na unaweza kukufanya ukawa Tajiri ndani ya kipindi kifupi.

MAGONJWA YA BATA
Lazima tuelewe magonjwa anayopata kuku na jamii ingine ya ndege bata pia hupata, tofauti ya bata na ndege wengine wana uwezo wa kuhimili magonjwa, yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya bata;

1. Duck Viral hepatitis
Ugonjwa huu unawashambulia vifaranga vya bata ambavyo vipo chini ya wiki 6, utakuta vifaranga wanakosa nguvu ya kusimama, kutembea na hatimaye vifo.

2. Aflatoxins Poisoning
Ugonjwa huu ni pale unapompa kifaranga pumba yenye madonge madonge ambayo ukiichunguza utakuta tayari imeanza kuweka kijani, hii ni sumu kabisa na haichelewi kumuondoa bata.

3. Cholera
Ugonjwa huu ni hatari kwa bata wadogo, utakuta bata wanajinyonga shingo na kuanguka.

4.Bata pia hushambuliwa na wadudu (parasites) mbalimbali ambao hupatikana ndani na nje ya mwili wake mfano viroboto, utitiri, chawa, ukurutu n.k ndani ya mwili anaweza kupata minyoo ya kwenye utumbo na maini.

5.Yapo magonjwa mengine hatari ya bata kama Duck viral enteritis, Aspergillosis, Collibasillosis n.k. kwa wale tunaofuga unaeza ambiwa bata ana matatizo ya mifupa, mafua, Typhoid au hata Pneomonia.

Magonjwa mengi ya bata husababishwa na ukosefu wa Vitamins, Madini na bila kusahau uchafu.

DAWA ZA KUWATIBU

Zipo dawa nyingi sana ambazo zinaweza kusaidia/kuokoa au kuimarisha hasa maisha ya vifaranga vya bata.

1. DCP
Dawa hii imeonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwakinga na kuwaimarisha bata katika miili yao hasa mifupa yao maana ina Calcium+Phosphorous. Matumizi yake unachanganya tu kwenye pumba.

2. Amin'total
Ni dawa moja nzuri sana inayosaidia absorption ya DCP ktk utumbo wa bata kwakuwa ina kiwango kikubwa cha D3. Dawa hii ni expensive kama una bata wachache si vema kuinunua kama unajiweza unaweza kuinunua.

3. Fluban (enrofloxaxin)
Imethibitika ni dawa nzuri sana hasa pale bata wanapopata typhoid. Ni dawa yenye nguvu na inatibu haraka.

4. Ivermectin
Ni dawa iliyoonyesha uwezo wa kuua wadudu wote wanaomdhuru bata ndani na nje kwa mkupuo.

5. Neoxychick
Ni dawa inayofanya vizuri hasa kukuzia bata wadogo, dawa hii ni antibiotics na ina Vitamins, na Minerals. Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama mbadala wa dawa hii ikiwa tu uchumi wako hauko vizuri, unamenya kitunguu swaumu, kitwange kisha changanya na maji, wape vifaranga siku3 za kwanza baada ya kuzaliwa.

6. Piperazine
Hapa wafugaji wa sungura watakuwa wamenielewa, hii ni dawa moja nzuri na inayoonyesha matokeo ya haraka. Ni dawa inayoua minyoo ya aina zote. Mimi binafsi napendelea kuitumia hii kwa bata wangu.

7. ESB3
Dawa moja makini sana pale bata anapoanza kuharisha, ukiona magonjwa ya tumbo yanamsumbua bata hasa kuharisha choo cheupe mpe hii dawa.

DAWA ZINGINE MUHIMU PALE UNAPOONA MABADILIKO YA BATA WAKO NI OTC, TYLOSIN, LIMOXIN, NA DOXCOL. Hizi zinatibu magonjwa mengi.

NADHARIA/IMANI/MISEMO
Kuna maneno mengi sana husemwa huko mitaani hasa kuhusiana na bata na kuna Imani zipo ktk jamii kwamba unapotaka kumchinja bata usimuonyeshe kisu kwani nyama yake itakuwa chungu sana, Wengine husema bata akitaga mayai yake anayahesabu na ukichukua mayai yake kila siku basi itafika kipindi atasusa kutaga na atapata stress ambazo zinaweza mfanya Asitage kwa muda mrefu, Wengine husema wakati wa kumnyonyoa bata haitakiwi kuongea maana mkiongea basi ataota tena manyoya mengine, Pia kuna wengine husema bata wa ukoo mmoja wakipandana inaweza kuwa chanzo hasa cha vifo vya bata wadogo, Yote kwa yote misemo ipo mingi tu inayoongelea bata japo mimi binafsi sitaki kusema lolote kuhusu hiyo misemo.

MUHIMU UNAPOFUGA BATA
1. Hakikisha maji wanayokunywa ni safi pia jitahidi kuwabadilishia maji mara kwa mara.
2. Hakikisha vyombo vya maji na chakula viwe safi muda wote.
3. Wape chakula safi na cha kutosha ili kuboresha ukuaji wao
4. Pia muhimu sana hasa kwa bata wadogo na wakubwa kuwachanganyia damu iliyokaushwa, chokaa, mifupa na mashudu ya alizeti ikiwezekana ili waweze kupata madini ya Calcium + phosphrus na trace Minerals. Pia itafanya bata wasiwe na hamu ya kula mayai. Na vilevile mchanganyiko huu unasaidia kupevusha mayai ya bata hivyo bata huwai kutaga mayai.
5. Vifaranga vikizaliwa unaweza kuvipa antibiotics kuzuia magonjwa na bacteria pia usiache kuwapa Vitamins ili kuwaongezea hamu ya kula na kinga ya magonjwa.
6. Unga wa sulphur umeonyesha matokeo mazuri hasa katika kuwalinda na bacteria.
7. Intensive System.. inashauriwa kama unajiweza ufanye ufugaji wa ndani wa bata hii itakupa matokeo mazuri na ya haraka.
8. Vifaranga vya bata havitakiwi kuoga au kunyeshewa na mvua kwa muda angalau wiki 10 za kwanza baada ya kuzaliwa.
9. Kipindi cha wiki 2 za kwanza vifaranga vya bata havitakiwi kupata baridi kama banda lako halina joto la kutosha unaweza kuwawekea majiko ya Mkaa ili kuwaongeza joto.
10. Hakikisha banda lako halina matundu yanayowawezesha panya kupita, Panya huwa wanawadhuru vifaranga wadogo hasa walio chini ya wiki mbili.
11. Changamoto kubwa ya bata ni chakula kwanza wanazaana kwa kasi, inabidi angalau uandae gunia la pumba pamoja na virutubisho vya kutosha. Pia bata wanakula sana majani hata kama unafugia ndani jitahidi siku moja moja uwe unawakatia majani hawa bata wa kienyeji ni sawa na kuku huwaga wanapenda kula majani.
12. Vifaranga wa bata hawatakiwi kula pumba iliyochanganywa na maji, kwa kufanya hivyo unawahatarishia maisha.

NB: MAGONJWA YOTE YA BATA YANAWEZA KUZUILIKA KWA USAFI TU. NA LAZIMA TUKUMBUKE BATA SIO MCHAFU ILA WEWE MFUGAJI NDIO MCHAFU.

AINA ZA BATA

Wapo bata wa aina mbalimbali ila hapa nitataja chache tu. Tukianza na bata wa kienyeji (Muscovy Duck) ambao kila mtu anawajua. Bata wengi wa kienyeji wanataga mayai 10 hadi 12 na mara nyingi wanataga alfajiri, bata hawa hutotoa watoto kuanzia 8+, wafugaji wengine wamebahatika kupata mbegu tofauti za hawa bata hivyo wanasema bata hawa wana uwezo wa kutaga mayai hadi 30.

Pia kuna bata wanaitwa Pekin, hawa asili yao ni china hapa Tanzania wapo ila sio wengi sana. Aina ingine ya bata ni Bukini hawa sasa watu wengi wanawafuga kibiashara, na pia wana gharama hata kuwanunua kwake. Chakula Chao kikubwa majani.

Aina ingine ya Bata ni bata mzinga hawa ni gharama sana kuwafuga, tena wakiwa wanakua ndio balaa inatakiwa uwe na chakula cha kutosha ndani kwani wanakula mno, asilimia kubwa ya waliojaribu kuwafuga hawakufikia malengo yao kutokana na gharama ya chakula na magonjwa, bata mzinga hutaga mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza, akitaga kwa mara ya pili hutaga mayai 25 hadi 30, na analalia kwa siku 28, siku ya 29 hadi 31 ni siku ambazo mayai hutotolewa, ikifika siku ya 32 kama mayai yamebaki basi hayo ni ya kutupa.
Aina ingine ya bata ni mchovya hawa wana midomo ya njano, Tabia zao hazitofautiani sana na bata wengine.

MASOKO NA BEI
Maneno mengi husemwa kwamba bata mchafu wengine husema sio mtamu, basi tu ili mradi kila mtu anasema yake, bata wana masoko sana hasa wageni wanapenda sana bata, shida ya upatikanaji wake ndio imesababisha bata waonekane wana bei sana na kama chakula cha anasa, tufuge bata kwa wingi ili upatikanaji wake usiwe wa kusua sua. Na pia bata wakiwa wengi na bei ikiwa ya kawaida itafanya watu wale bata kwa wingi.

CHANJO ZA BATA
Bata wakiwa ni ndege kama kuku nao wanastahili kupewa kinga. Bata unaweza kuwakinga na maradhi kwa kuwaweka sehemu safi. Ila kama unataka uhakika wa asilimia 200 bata wako wasife wape chanjo kwa mtiririko ufuatao.

-Bata wako wakifika siku saba yani wiki ya kwanza (baada ya kumaliza kutumia Neoxychick) wape chanjo ya Newcastle
  • Bata wako wakifika siku Kumi na nne yaani wiki ya pili wape chanjo ya Kideri
  • Bata wako wakifika siku ya Ishirini ya moja yani wiki ya tatu wape chanjo ya Newcastle tena.
  • Bata wako wakifika siku ya Ishirini na nne yaani wiki ya 4, wape chanjo ya Gumboro. Hapo utakuwa umekata mzizi wa fitina, ila usafi lazima pamoja na lishe bora. Na inashauriwa kila unapowapa chanjo wape Vitamin kabla hujawapa chanjo ingine, na Vitamin nzuri inaitwa IntroVit A ina vitamin nyingi nyingi sana. Baada ya hapo unaweza kuwapa vifaranga wapo Growers Mash bila chanjo tena na watakuwa vizuri bila tatizo.

HITIMISHO
Kupitia thread hii wale wote wanaofuga au wanaotarajia kufuga bata tukutane kushea mambo mbalimbali yahusuyo bata. Pia natoa wito Kwa moderators wa JF waweke PIN hii posti iwe juu kwa ajili ya sisi wapenzi wa kula na kufuga bata. Wataalam wa mifugo wanakaribishwa kutoa mawazo yao mbali mbali yahusuyo mfugo huu adhimu.

NYONGEZA

Bata wamekuwa wakifugwa miaka mingi katika ardhi ya Tanzania, na njia za ufugaji ni tofauti. Bata hasa wakiwa wadogo inashauriwa wale starter kwa angalau mwezi na wawekewe Glucose ile ya kuku kwenye Maji pamoja na Vitamin, ila kuna ambao hawafuati haya masharti. Kùna ambao wanawanyoosha shingo bata wakiwa wadogo na bata hukua bila tatizo lolote. Pia kuna ambao hawawapi bata dawa yoyote zaidi ya muarobaini, alovera na majani ya Mpapai. Well kila mtu ana njia yake ya ufugaji ili mradi malengo yafikiwe.

NAWASILISHA.
 
Asante mkuu kwa jinsi ninavyofahamu hawa bata wametofautiana, kuna bata wanaitwa bata bukini ni wazuri kimuonekano na hata bei yake imechangamka. Ukifuga hao wanazaliana kwa wingi vilevile utauza kwa bei ya juu, hata hawa bata wetu wa kienyeji pia wanazaliana kwa wingi mno, kibongobongo hawa unaweza kupata masoko yake humuhumu uswahilini kwetu. Wale bukini ukitaka kuuza inabidi usogee mjini kidogo huko utapiga ela ndefu.
Hongera mkuu kwa chapisho bora kabisa, mkuu nikuulize hivi ushawahi kutafiti na kujua aina gani ya bata ni nzuri na yenye uzalishaji wa haraka ambao unaweza kukuingizia kipato faster?
 
UTANGULIZI

Habari zenu wanajamvi, kwanza napenda kudeclare interest mimi ni mfugaji mchanga wa Bata, na nilifikia uamuzi wa kufuga bata baada ya maradhi kuwapiga kuku wangu na wakafa wote. Nimepitia threads nyingi sana za humu na sijaona special thread inayoongelea bata na bila hiyana nimemua kuileta ili wafugaji bata na wataalam tukutane hapa kupeana ujuzi. Bata ni ndege mtamu nadhani kushinda hata kuku, watu wengi wanapenda kumla bata ila hawataki kabisa kumfuga kutokana na mazingira yake. Ufugaji wa bata una faida na unaweza kukufanya ukawa Tajiri ndani ya kipindi kifupi.

MAGONJWA YA BATA
Lazima tuelewe magonjwa anayopata kuku na jamii ingine ya ndege bata pia hupata, tofauti ya bata na ndege wengine wana uwezo wa kuhimili magonjwa, yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya bata;

1. Duck Viral hepatitis.
Ugonjwa huu unawashambulia vifaranga vya bata ambavyo vipo chini ya wiki 6, utakuta vifaranga wanakosa nguvu ya kusimama, kutembea na hatimaye vifo.

2. Aflatoxins Poisoning
Ugonjwa huu ni pale unapompa kifaranga pumba yenye madonge madonge ambayo ukiichunguza utakuta tayari imeanza kuweka kijani, hii ni sumu kabisa na haichelewi kumuondoa bata.

3. Cholera
Ugonjwa huu ni hatari kwa bata wadogo, utakuta bata wanajinyonga shingo na kuanguka.

4.Bata pia hushambuliwa na wadudu (parasites) mbalimbali ambao hupatikana ndani na nje ya mwili wake mfano viroboto, utitiri, chawa, ukurutu n.k ndani ya mwili anaweza kupata minyoo ya kwenye utumbo na maini.

5.Yapo magonjwa mengine hatari ya bata kama Duck viral enteritis, Aspergillosis, Collibasillosis n.k. kwa wale tunaofuga unaeza ambiwa bata ana matatizo ya mifupa, mafua, Typhoid au hata Pneomonia.

Magonjwa mengi ya bata husababishwa na ukosefu wa Vitamins, Madini na bila kusahau uchafu.

DAWA ZA KUWATIBU

Zipo dawa nyingi sana ambazo zinaweza kusaidia/kuokoa au kuimarisha hasa maisha ya vifaranga vya bata.

1. DCP
Dawa hii imeonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwakinga na kuwaimarisha bata katika miili yao hasa mifupa yao maana ina Calcium+Phosphorous. Matumizi yake unachanganya tu kwenye pumba.

2. Amin'total
Ni dawa moja nzuri sana inayosaidia absorption ya DCP ktk utumbo wa bata kwakuwa ina kiwango kikubwa cha D3. Dawa hii ni expensive kama una bata wachache si vema kuinunua kama unajiweza unaweza kuinunua.

3. Fluban (enrofloxaxin)
Imethibitika ni dawa nzuri sana hasa pale bata wanapopata typhoid. Ni dawa yenye nguvu na inatibu haraka.

4. Ivermectin
Ni dawa iliyoonyesha uwezo wa kuua wadudu wote wanaomdhuru bata ndani na nje kwa mkupuo.

5. Neoxychick
Ni dawa inayofanya vizuri hasa kukuzia bata wadogo, dawa hii ni antibiotics na ina Vitamins, na Minerals. Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama mbadala wa dawa hii ikiwa tu uchumi wako hauko vizuri, unamenya kitunguu swaumu, kitwange kisha changanya na maji, wape vifaranga siku3 za kwanza baada ya kuzaliwa.

6.Piperazine
Hapa wafugaji wa sungura watakuwa wamenielewa, hii ni dawa moja nzuri na inayoonyesha matokeo ya haraka. Ni dawa inayoua minyoo ya aina zote. Mimi binafsi napendelea kuitumia hii kwa bata wangu.

NADHARIA/IMANI/MISEMO
Kuna maneno mengi sana husemwa huko mitaani hasa kuhusiana na bata na kuna Imani zipo ktk jamii kwamba unapotaka kumchinja bata usimuonyeshe kisu kwani nyama yake itakuwa chungu sana, Wengine husema bata akitaga mayai yake anayahesabu na ukichukua mayai yake kila siku basi itafika kipindi atasusa kutaga na atapata stress ambazo zinaweza mfanya Asitage kwa muda mrefu, Wengine husema wakati wa kumnyonyoa bata haitakiwi kuongea maana mkiongea basi ataota tena manyoya mengine, Pia kuna wengine husema bata wa ukoo mmoja wakipandana inaweza kuwa chanzo hasa cha vifo vya bata wadogo, Yote kwa yote misemo ipo mingi tu inayoongelea bata japo mimi binafsi sitaki kusema lolote kuhusu hiyo misemo.

MUHIMU UNAPOFUGA BATA

1. Hakikisha maji wanayokunywa ni safi pia jitahidi kuwabadilishia maji mara kwa mara.
2. Hakikisha vyombo vya maji na chakula viwe safi muda wote.
3.Wape chakula safi na cha kutosha ili kuboresha ukuaji wao
4.Pia muhimu sana hasa kwa bata wadogo na wakubwa kuwachanganyia damu iliyokaushwa, chokaa, mifupa na mashudu ya alizeti ikiwezekana ili waweze kupata madini ya Calcium + phosphrus na trace Minerals.
5.Vifaranga vikizaliwa unaweza kuvipa antibiotics kuzuia magonjwa na bacteria pia usiache kuwapa Vitamins ili kuwaongezea hamu ya kula na kinga ya magonjwa.
6. Unga wa sulphur umeonyesha matokeo mazuri hasa katika kuwalinda na bacteria.
7. Intensive System.. inashauriwa kama unajiweza ufanye ufugaji wa ndani wa bata hii itakupa matokeo mazuri na ya haraka.
8.Vifaranga vya bata havitakiwi kuoga au kunyeshewa na mvua kwa muda angalau wiki 10 za kwanza baada ya kuzaliwa.
9. Kipindi cha wiki 2 za kwanza vifaranga vya bata havitakiwi kupata baridi kama banda lako halina joto la kutosha unaweza kuwawekea majiko ya Mkaa ili kuwaongeza joto.

NB; MAGONJWA YOTE YA BATA YANAWEZA KUZUILIKA KWA USAFI TU.

MASOKO NA BEI
Maneno mengi husemwa kwamba bata mchafu wengine husema sio mtamu, basi tu ili mradi kila mtu anasema yake, bata wana masoko sana hasa wageni wanapenda sana bata, shida ya upatikanaji wake ndio imesababisha bata waonekane wana bei sana na kama chakula cha anasa, tufuge bata kwa wingi ili upatikanaji wake usiwe wa kusua sua. Na pia bata wakiwa wengi na bei ikiwa ya kawaida itafanya watu wale bata kwa wingi.

HITIMISHO
Kupitia thread hii wale wote wanaofuga au wanaotarajia kufuga bata tukutane kushea mambo mbalimbali yahusuyo bata. Pia natoa wito Kwa moderators wa JF waweke PIN hii posti iwe juu kwa ajili ya sisi wapenzi wa kula na kufuga bata. Wataalam wa mifugo wanakaribishwa kutoa mawazo yao mbali mbali yahusuyo mfugo huu adhimu.

NAWASILISHA.
Hongera sana kwa kutushirikisha hilo, samahani ww unafuga Bata wa aina ipi?
 
Safi sana mkuu tungeomba utupe changamoto za ufugaji wa bata bukini.

Hawana changamoto kubwa, chakula chao 90% ni majani lakini lazima wapate lishe yenye virutubisho Kama growers pumba za kuku na watoto wapate starter.

Kwenye soko naona ndio pagumu nadhani kwasababu ya Bei. Na jamii bado haijaipa kipaumbele Sana nyama ya Bata na ufugaji wake kwa ujumla.
 
Umeongea jambo kubwa sana, jamii inabidi ibadilike, kinachofanya watu kuchukia bata ukiwauliza wanakwambia wanajisaidia ovyo. Ila ukichinja kwenye kula wanapenda tena wanajilamba na kuisifia ni tamu. Bata anayelalia ndio kinyesi chake kinanuka. Ila hawa wa kawaida choo chao ni kama cha kuku tu.
Hawana changamoto kubwa, chakula chao 90% ni majani lakini lazima wapate lishe yenye virutubisho Kama growers pumba za kuku na watoto wapate starter....

Kwenye soko naona ndio pagumu nadhani kwasababu ya Bei..... Na jamii bado haijaipa kipaumbele Sana nyama ya Bata na ufugaji wake kwa ujumla....
 
Umeongea jambo kubwa sana, jamii inabidi ibadilike, kinachofanya watu kuchukia bata ukiwauliza wanakwambia wanajisaidia ovyo. Ila ukichinja kwenye kula wanapenda tena wanajilamba na kuisifia ni tamu. Bata anayelalia ndio kinyesi chake kinanuka. Ila hawa wa kawaida choo chao ni kama cha kuku tu.
Kwa wafugaji hatuoni kinyesi kama kinanuka tunajionea sawa kabisaa, ufugujai unaraha yake hasa ukiufuga kwa kutoka moyoni sio kulazimishwa au kufwata mkumbo, nimeshakutana na hii changamoto ya watu wanafuga lakini ni kwasababu alisikia kuku au Bata au Mbwa wanalipa.
 
Hahaha mkuu umeongea ukweli mtupu kuna kipindi lilivuma wimbi la watu kufuga sungura wakawa wanaambiwa wafuge halafu wakiwa wengi kuna jamaa wanatoka kenya kuja kuwanunua bwana bwana watu wakafuga matokeo yake wakenya wakaingia mitini watu wakabaki na sungura wao. Walifuga kwakuwa waliambiwa kuna ela na sio passion. Mimi nafuga kama passion. Ninao na sungura pia lakini sifugi ili nije kukuuzia. Ukija kununua nitakuuzia ila kipaumbele changu ni mboga kwa ajili ya familia.
Kwa wafugaji hatuoni kinyesi kama kinanuka tunajionea sawa kabisaa, ufugujai unaraha yake hasa ukiufuga kwa kutoka moyoni sio kulazimishwa au kufwata mkumbo, nimeshakutana na hii changamoto ya watu wanafuga lakini ni kwasababu alisikia kuku au Bata au Mbwa wanalipa.
 
Hahaha mkuu umeongea ukweli mtupu kuna kipindi lilivuma wimbi la watu kufuga sungura wakawa wanaambiwa wafuge halafu wakiwa wengi kuna jamaa wanatoka kenya kuja kuwanunua bwana bwana watu wakafuga matokeo yake wakenya wakaingia mitini watu wakabaki na sungura wao.
Walifuga kwakuwa waliambiwa kuna ela na sio passion.
Mimi nafuga kama passion. Ninao
na sungura pia lakini sifugi ili nije kukuuzia. Ukija kununua nitakuuzia ila kipaumbele changu ni mboga kwa ajili ya familia.
Huo sasa ndio ufugaji wakutoka ktika uvungu wa Moyo wa mfugaji, Passion, Mungu akubariki sana.
Kwakweli hata mimi ninabaadhi ya bata Pekini nawafuga kwa mapenzi tu ya ufugaji inaleta Raha,Amani,Chakula kwa familia, kwa ufugaji wa mradi nawekeza zaidi kwenye Mbuzi,Mbwa,Bukuni,na bata hawa wakawaida ndio naanza sasa.
 
Mkuu hata hawa bata wa kienyeji imagine ukafuga ukawa nao kama 200, huo ni mradi tosha.
Na ndio maana kuna sehemu ktk hili chapisho nimeandika unaweza jikuta umeamka tajiri kupitia ufugaji. Mfano bata wa kienyeji wanauzwa 20,000x200= 4,000,000 pesa kama hiyo haitoshi kuanza biashara ingine?
Huo sasa ndio ufugaji wakutoka ktika uvungu wa Moyo wa mfugaji, Passion, Mungu akubariki sana.
Kwakweli hata mimi ninabaadhi ya bata Pekini nawafuga kwa mapenzi tu ya ufugaji inaleta Raha,Amani,Chakula kwa familia, kwa ufugaji wa mradi nawekeza zaidi kwenye Mbuzi,Mbwa,Bukuni,na bata hawa wakawaida ndio naanza sasa.
 
Hao Bata wa kienyeji hawajawahi kunivutia ! Mtaani tunawaita Bata maji !!!

Bata bukini wazuri , ninao wawili ndo nimeanza! Hawa nafuga Kama kivutio na mboga tu !

Bata mzinga nao wazuri pia soko lake Zuri, tatzo Ni wanakufa Sana.,,,hasa vifaranga, pia wanashambuliwa Sana na magonjwa !!! Niliwahi kufuga kipindi fulani , waliteketea karibia wote ! Ufugaji wangu sio mkubwa wa kibiashara !!!
 
Kweli mkuu bata mzinga ufugaji wake unahitaji uwe kwanza umejiandaa,halafu kadri anavyokua ndio anazidi kula sana.
Bata maji hawavutii sema hawa ni mboga na wanafaa kwa kuuza, kwa sababu bei ni ndogo kila mtu anaweza kuimudu.
Hao bata bukini bei yake imesimama

Back
Top Bottom