Obwere Kabwana
New Member
- Sep 20, 2023
- 3
- 5
Waziri wa TAMISEMI na Taasizi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) tumeni kikosi kazi kuchunguza Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kuna ufisadi wa kutisha.
Kampuni ya Ongujo Invesment inayomilikiwa na Ndg. Ongujo Wakibara (OWAN) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya imepewa zabuni ya kununua Bolt na Nut kwa bei ya kutupwa Tsh. 31,539,340 badala ya bei iliyopo sokoni ambayo ni Tsh. 50,000. Zabuni hii haikutangazwa kama Sheria ya Manunuzi inavyotaka zabuni zote zenye thamani zaidi ya Tsh. Milioni Tano (5,000,000) lazima zitangazwe.
Mkataba kati ya Ongujo Investment kutopitishwa na Bodi ya Zabuni (Tender Board) kinyume na Sheria ya Manunuzi PPA, 2011 Section 35(1), (2) & (3). Zabuni kutofuata sheria ya Manunuzi (The Public Procurement (Ammendment) Regulation, 2016-Section 91-Method of tendering.
Kampuni hii imekuwa na rekodi mbovu ya utekelezaji wa zabuni katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
Mwaka 2021 Kampuni ya Ongujo Investment ilipewa zabuni ya Shilingi Milioni Mia Saba (700,000,000) Fedha za Covid 2019 kusambaza vifaa vya ujenzi hadi leo hajakabidhi Floor Tiles zenye thamani ya Tzs Milioni mia Mmoja na hamsini (150,000,000) na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake
Mwaka wa Fedha 2023/2024 Kampuni hii imepewa kandarasi ya kujenga Madarasa Shule ya Sekondari Rabuor, matofali yanayotumika katika ujenzi yapo chini ya kiwango na ukuta tayari umeweka ufa na kuhatarisha uhai wa wanafunzi wanaosoma katika shule hii.
Mheshimwa Waziri Mchengerwa na Kamanda wa TAKUKURU Inspekta Jenerali Hamduni Watanzania wana imani kubwa sana na kazi mnazofanya, changamoto mnayopata ni mnaangushwa na wasaidizi waliopo katika ngazi za Wilaya na Mikoa. Ni aibu ufisadi unafanyika na kuna DC, Kamamnda wa TAKUKURU (W), DSO na kamati za ulinzi na usalama Wilaya chini ya DC.
Pitia attachment soma namba 2301503
,