Uchaguzi 2020 Ufisadi uliobuliwa na CAG umeiondolea sifa (credibility) Serikali ya awamu ya 5. Wapinzani sasa mshindwe wenyewe!

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,027
Ni ukweli usiopingika sasa kuwa upigaji (ufisadi) ambao umekuwepo miaka nenda rudi serekalini bado kabisa haujapatiwa dawa, na serekali ya awamu ya 5 iliyojinasibu kama mkombozi katika eneo hili ni dhahiri imeshindwa kufurukuta kinyume cha matarajio ya sisi wananchi.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa ufisadi chini ya awamu hii ni mkubwa zaidi kuliko hata ilivyowahi kutokea kwenye awamu zilizotangulia huko nyuma.

Tofauti kubwa ni kwamba while kwenye awamu za huko nyuma madili yalikuwa yanapigwa kitimu miongoni mwa makada wa chama tawala, chini ya awamu hii inaonekana kuna wateule wachache (the chosen ones within the inner circle) ndiyo wanufaikaji wakubwa.

Kumekuwepo na viashiria vingi tu vya kifisadi chini ya awamu hii.… nitavitaja kwa uchache:

1) Manunuzi makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na serekali bila kuzingatia taratibu za manunuzi (mifano ipo mingi mnaijua)

2) Miradi ya pesa mabilioni kutengewa fedha kimyakimya bila idhini ya bunge (mifano ipo mnaijua)

3) Ukandamizaji wa watu kujieleza kupitia platforms mbalimbali ili kuficha maovu (mifano ipo mnaijua)

4) Kumekuwepo na wish-wash statements kutoka serekalini kuhusiana na zaidi ya 1.5tr zinazosemekana zilipigwa kwa mujibu wa taarifa ya CAG mstaafishwa Prof Assad. Jee, kuna mtu yeyote humu anaweza kutupatia leo final and credible statement ya serekali juu ya hili? Your guess is as good as mine!

5) CAG mstaafishwa Prof Assad alipigwa sana vita na mihimili ya Bunge & Executive hadi kupelekea kudhalilishwa mara kadhaa (mifano mnaikumbuka).
Hata kuondolewa kwake kwenye nafasi yake kunasemekana ni kinyume na katiba (kesi ipo mahakamani kwa hiyo sitaliongelea zaidi hili)

Watu wengi (wakiwemo waliomo ndani ya serekali kwenyewe, inawezekana pia na mamlaka ya uteuzi) wali misconceive kuwa kumuondoa Prof Assad kwenye nafasi ya CAG na kumleta mtu ambaye anaweza kuegemea upande wa serekali kungezuia kuibuliwa kwa haya madudu. Misconception hii ilitokana na kutotambua kuwa wanaofanya kazi ya ku audit huko field siyo CAG mwenyewe bali ni timu yake ambayo imesheheni vijana wengi wazalendo (tunawajua) ambao wanazingatia maadili ya kazi yao katikati ya mistari. Kwa hiyo, CAG, pamoja na kwamba ndiye signatory wa ripoti ya mwisho, hana ubavu wa kubadilisha audit findings hata afanyeje.

Wito wangu kwa kambi ya upinzani - mnahitaji kuya-compile haya madhaifu yote and you should make the most of it NOW - not tomorrow!

Acheni egos zenu za kila chama kujifanya ni bora kuliko chengine. Hakikisheni mnashinikiza tume huru inapatikana lakini wakati huo huo mlenge attacks zenu dhidi ya madhaifu haya ya awamu hii na kuendelea kuwaelimisha wananchi kuwa Maisha yao ni zaidi ya treni ya umeme au bwawa la umeme ambalo nalo linaweza kukumbwa na dhahma (natural hazards) wakati wowote na lisiwasaidie walengwa (wananchi) katika mustakabali wa maisha yao.

Wananchi wengi kwa kweli wamejikatia tamaa na ugumu wa maisha na hivyo wanahitaji sway kidogo tu ili waunge mkono ukombozi mpya wa taifa letu. Kukata tamaa kwa wananchi kunathibitishwa na jinsi wanavyofurahishwa kila wanapoona kiongozi fulani (waziri, mkurugenzi, nk) anatumbuliwa - kisaikolojia hii ni consolation tu kwao kwamba "ah bora naye awe anasota kama sisi! - wasotaji tuwe wengi".

The ball is in your court, dear opposition camp (cc Zitto, John Mnyika, etc).

Adios!
 
subiri tu....
Upinzani uchwara wa TZ kuchukua nchi may be baada ya miaka 50 ijayo lakini siyo sasa hivi.

Mwaka 2015 Mbowe na Lowassa aliwaambia kuwa mkishindwa kuiondoa CCM mwaka 2015 itachukua miaka 50 zaidi kuweza kufikiria kuondoa CCM madarakani au hamkuwaelewa viongozi wenu mkuu!!?
 
Upinzani uchwara wa TZ kuchukua nchi may be baada ya miaka 50 ijayo lakini siyo sasa hivi.

Mwaka 2015 Mbowe na Lowassa aliwaambia kuwa mkishindwa kuiondoa CCM mwaka 2015 itachukua miaka 50 zaidi kuweza kufikiria kuondoa CCM madarakani au hamkuwaelewa viongozi wenu mkuu!!?
tunaongelea ufisadi chini ya awamu ya 5 comrade!
 
Ufisadi huu umefanywa na awamu ya nne.

Serikali ya Magufuli inapambana kila siku kulisafisha hili taifa
 
tunaongelea ufisadi chini ya awamu ya 5 comrade!
Kuchambua ripoti tu ya CAG umeshindwa tutawezaje kuongelea ufisadi wakati umeshindwa kuchambua hiyo ripoti badala yake umetoa mapovu tuuu!
 
Tukiweka kando ukabila na udini uliotangazwa na gwajima ni nani kati ya wafuatao anaweza kupigia kura ccm?!?!.......zingatia zile factors...(economic, social and political factors)......
1. Wakulima
2. Wafanyakazi
3. Wafanyabiashara
4. Wanafunzi
 
Kwanza tungekuwa na Rais makini angekuwa ashatoa speech kali kwa taifa na kuwaambia wote waliofanya uzembe na wizi wapishe ofisini. lakini vile hatuna rais ndio hivyo.
 
CAG si alibadilishwa baada ya kuonyesha upuuzi wanaoufanya? Mpya naye ataondolewa? Haha serikali chafu ni chafu tu hata uweke mbwa atajua tu kua ni chafu.

Ngoja tuone huyu atakaa muda gani. Napenda kuona watu wanafata taaluma zao regardless ya wamepewa cheo na nani. Do what is right always
 
Kuchambua ripoti tu ya CAG umeshindwa tutawezaje kuongelea ufisadi wakati umeshindwa kuchambua hiyo ripoti badala yake umetoa mapovu tuuu!
weka uchambuzi wako halafu tanabaisha vs mapovu yangu!
 
Back
Top Bottom