Ufisadi UDA: Madiwani na wabunge wa UKAWA waliohongwa kushtakiwa kamati kuu ya CHADEMA

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
924
1,096
  • Meya wa UKAWAUbungo athibitisha kuzifahamu tuhuma za Rushwa
  • asema atakiomba chama chake kuwafanyia uchunguzi madiwani na wabunge wote wanahusika.


Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiwa na Mbunge wa Kibamba John John Mnyika katika Picha ya Maktaba.

Na Mwandishi wetu:

wakati kukiwa na taarifa za mameya wote wa UKAWA wanaongoza katika halimashauri za manispaa mbali mbali zilizopo jijini Dar es salaam kuitwa Dodoma kwenda kujadili kwa mapana tuhuma zilizoibuliwa kuhusu uuzwaji wa shirika la UDA, mameya hao ni wale wa Ubungo, Ilala na emya wa jiji la Dar es salaam.

mjumbe wa kamati kuu wa CHADEMA ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob amekiri kuzipata na kuzifahamu hizo taarifa za wajumbe wa halimashauri ya jiji kupokea rushwa ya kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu kwa madiwani wa vyama vyote na shilingi milioni tano tano kwa wabunge wa vyama vyote kutoka kwa wamiliki wapya wa shirika la usafiri Dar es salaam UDA ili kuhalalisha uuzwaji usiofuata misingi ya kisheria wa shirika hilo na kupokea shilingi bilioni 5.8 kama mgao wao wa asilimia 51% na kuahidi kuzifikisha rasmi katika vikao halali vya chama chake cha chadema ili chama hicho kiwachukulie hatua stahiki wajumbe wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo haviendani na misingi ya chama chao ya kupambana na Rushwa.

''nimezisikia na zimesambaa sana hizo taarifa hata kabla hujaniuliza, na kwa kweli zinatuvunjia heshima sisi kama wawakilishi wa wananchi na wana chadema, kwa hiyo nimeamua kukiandikia barua chama changu kupitia katibu mkuu kiitishe uchunguzi rasmi ili kujiridhisha juu ya tuhuma hizo ambazo si nyepesi'' alisema Boniface alipoulizwa na JAMVI LA HABARI kwa njia ya Simu .

''mimi binafsi na mjumbe wa kamati kuu ya chama, hivyo nina nafasi ya kuliiingiza hilo kwenye kikao muhimu ili lichukuliwe hatua, lakini kwa madiwani wa vyama vingine sina uamuzi nalo maana wao pia wana utaratibu wao katika vyama vyao, lakini kwa CHADEMA hatutamwangalia mtu usoni, chama kitachunguza na atakayebainika kuchukua rushwa hiyo atawajibika ipasavyo''. aliongeza mstahiki meya Boniface.

hivi karibuni JAMVI LA HABARI lilipoti juu ya kuwepo kwa tuhuma za wawakilishi hao wa wananchi wa jiji la Dar es salaam kuhongwa ili kuridhia utakatishwaji wa matumizi ya fedha hizo.

taarifa za uhakika zinasema upande wa vigogo wa UDA sasa wanahaha kuhakikisha kuwa taarifa za wao kugawa fedha kwa madiwani na wabunge ili kuhalalisha mradi wao hazimfikii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa wanafahamu zikimfikia na akifanya uchunguzi na akajiridhisha hawezi kuhalalisha biashara hiyo kutokana na msimamo wake uliojizolea umaarufu kwa wananchi wa kupambana na Rushwa na kuchukia aina yote ya ufisadi.

''jamaa wanahaha kuhakikisha namba moja hazipati hizi taarifa za chini ya carpet, unajua walijitahidi sana kuficha na kuwarubuni wasaidizi wa rais kuwa hakuna shida kwenye mradi ule na kwamba kutokuunga mkono ni kuchelewesha juhudi za maendeleo, sasa lilipoibuka hili wamepagawa, wanajua kabisa Rais hawezi kubali''. kilisema chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na wamiliki hao wa UDA
source : JAMVI LA HABARI
 
Hata aliyewapa green light naye wakuchunguza.Issue imeshapigiwa kelele kwamba ina ufisadi na Rushwa kwanini alibariki matumizi ya hiyo B5.8??
 
Nyakati zile tuliwaeleza tabia za hawa mafisadi ziko damuni, haziko CCM wala CDM wala ACT, katika vyama hivi vyote kuna wasafi na wachafu

CCM kinalaumiwa kwa kutochukua hatua husika kwa wakati sahihi wakati wana nguvu zote

CDM na vyama vingine onyesheni njia kwa kuwachukulia hatua hao madiwani waliokula rushwa, is another opportunity to come out clean

Kisiasa mtakuwa mnamuaibisha bossi mkubwa kuwa alichobariki bado--juzi kwa wale jamaa kununua UDA ni kichafu na mtamuweka kwenye wakati mgumu sana...na mtamshusha confidence!

mtaua ndege wawili kwa jiwe moja, yet mtajisogeza karibu na wananchi
 
Hii ni Aibu kubwa sana kwa UKAWA.

Wote ambao watapatikana kujihusisha na kadhia hii hatua zichukuliwe dhidi yao.

Madiwani na Wabunge wa UKAWA lazima wajitofautishe na wale wa CCM ambao wao kuchukua rushwa/hongo ni jambo la kawaida kabisa.
 
I agree with your advice 100%
 
Hii ni Aibu kubwa sana kwa UKAWA.

Wote ambao watapatikana kujihusisha na kadhia hii hatua zichukuliwe dhidi yao.

Madiwani na Wabunge wa UKAWA lazima wajitofautishe na wale wa CCM ambao wao kuchukua rushwa/hongo ni jambo la kawaida kabisa.
ndio maana MEYA WA UBUNGO amelisemea hilo
 
Kwa upande wangu bado sijaamini kwamba kuna madiwani wamepokea RUSHWA zaidi ya tuhuma za kuishushia heshima ukawa na hususan Chadema.
 
Hivi wewe unayehonga watu ni kwa faida gani unayoipata kama sio wizi mtupu?....

Yaani kununua umenunua 5.8 billion halafu bado unaonga nini kama umenunua kihalali?.........

Ifike muda Sasa tufukue makaburi magufuli mafisadi wamemushinda haiwezekani mtu ameshastaafu karibu miaka miwili Sasa lakini bado anahujumu uchumi tunamchekea tu.......

We are all planing to fail again as always we fail as a nation?

Ukawa kama wameshiriki kwenye ufisadi wajitasimini wajiuzulu wizi ni nembo ya Ccm hata Dr Slaa aliwatimua wezi wote baada ya kugundua walitumiwa na ccm kwa namna moja hama nyingine..........

This is sensitive issue but watu wanachukulia jambo la kawaida kwa sababu ya mfumo mbovu uliowekwa na Ccm Takukuru wanafanya kazi gani kwenye Rushwa wakati wanapoteza kodi zetu kulipwa mishahara wakati ni wafanyakazi wa hovyo hovyo wameshindwa kupambana na ufisadi?...
.
 
msome vizuri meya Boni utapata picha

Nimemsoma amesema amesikia TUHUMA na yeye,mara ya kwanza hao JAMUHURI walisema na Boniphace ,Mnyika na Kubenea wamepokea,ndiyo sababu siamini hizo tuhuma kama zinaukweli,ila kwa sababu ni tuhuma wameamua kuzifanyia kazi ni kitu cha msingi
 
Chadema tokea wamsafishe fisadi Lowasa, nikajua hamna kitu hapo.

Chadema ni majizi mara 10000000 ya ccm
 
Chadema tokea wamsafishe fisadi Lowasa, nikajua hamna kitu hapo.

Chadema ni majizi mara 10000000 ya ccm

Tupatie jamaa wa Bilioni nane,ndipo uwe na haki ya kuituhumu Chadema au Lowassa.Tuambie kwanini Mkullu alitoa green light kwa UDA wakati anajua UDA ni JIPU??AU sababu ni HOME BOY??

Safisheni nyumba yenu muone uchafu wa nyumba ya jirani
 
Asante mkuu kwa mawazo yasiyo na mgando wala kutenganisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…