A
Anonymous
Guest
Wakuu,
Nane-Nane ya Mwaka huu imegubwikwa na ufisadi wa hali ya juu hususani katikamaandalizi yake. Hii yangu inakuja kama muendelezo wa kile amba ho kiliwekwa wazi kwamba kuna vyoo viwili tu katika eneo lote kitu ambacho kimesababisha kero kubwa kwa washiriki.
Ukienda mbele zaidi haya ndio mambo ambayo yamefanyika yaliyopelekea kusema kwamba kuna ubadhilifu mkubwa katika maandalizi ya sherehe hizi:
1. Ni kampuni moja tu ambayo imepewa kazi ya kuandaa na kujenga mabanda kwa ajili ya maonyesho ya Nane Nane. Kampuni hiyo, FNM MARKETING ilipewa kazi hiyo bila kujali utaalam katika sekta husika na uwezo wake wa kuweza kamilisha kazi kwa wakati ili maonyesho yaende vizuri.
2. Katika mapnyesho hayo kuna Pavilions 16 ambapo kila Pavilion moja imelipiwa shilingi za Kitanzania 105,500,000 ambapo waandaaji walikuwa na jukumu la kuzitengeneza na kuweka kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maonyesho. Hata hivyo mpaka asubuhi hii sio Pavilion zote zilizokamilika ujenzi wake na washiriki wamelazimika kuingia gharama za ziada kuweza zitengeneza ili maonyesho yaendelee. Jumla ya TZS 1.6B zimekusanywa kwenye malipo ya Pavilion.
3. Katika bajeti ilitengwa pesa kwa anili ya ujenzi wa miundombinu na barabara ambapo mpaka kufikia jana, zaidi ya TZS Bilioni 7 zimeshatumika kwenye miundombinu ilhi uwanja wa maonyesho bado una hali mbaya na vumbi kila sehemu.
4. Hakuna maandalizi yake ofisi ya mawasiliano hivyo kupelekea washiriki kuhangaika kuweza kufahamu nani ni muhusika mkuu na nani ataweza watatulia matatizo yao.
5. Card zitolewazo kwa wamiliki wa Pavilion baada ya kulipa milioni 105 zimekuwa hazipatikani hali inayopelekea kuwalazimu kulipa pesa zaidi ili kuweza zipata kadi hizo na kuwapatia washiriki wataokuwa katika Pavilions zao.
6. TV ambazo zilianishwa kwamba zitawekwa katika kila booth hazijawekwa hivyo kupelekea washiriki kuanza kuhangaika kutafuta TV mbadala ambazo wanazitumia katika maonyesho.
7. Washiriki wamekuwa wanashinikizwa na Wizara kushiriki huku wakipangiwa nini wanatakiwa weka katika mabanda yao bila kujali mipango ambayo washiriki wamekuwa nayo kuhusu ushiriki wao katika Nane Nane. Waziri amekuwa akitumia mabavu na vitisho kulazimisha ushiriki wao katika watu.
Mwisho, pamoja na nia njema ya kutaka maonyesho kuwa ni makubwa na yenye ufanisi, pamoja na bajeti kubwa iliyopangwa kwa ajili ya maandalizi; ubadhirifu mkubwa umefanyika na unaendelea kufanyika.
NOTE: Angalia Mockup design na linganisha na kilichotokea
Tuangalie hili…
Nimeambatanisha picha za vyoo vya Nane Nane vikiwa vinajengwa leo kwa kasi baada ya habari yake kuibuliwa jana na JamiiForums.
Hivi ni vyoo vilivyokamilika kwa ajili ya matumizi.
Hii ndio hali halisi asubuhi hii ambayo ndio siku ya kilele cha sherehe za Nane Nane Dodoma ambapo tunashuhudia wakandarasi wakiendelea na kazi ya Zima Moto kumalizia maandalizi ya viwanja kwa ajili ya maonyesho, ikiwa ni pamoja na kuweka pavements na kutengeneza bara bara (tukitegemea kupambana na vumbi).
Ikumbukwe kwamba Nane Nane ni Sikukuu ya Kitaifa ambayo inasheherekewa kila mwaka, na ilikuwa na bajeti yake. Sasa je, kulikuwa na ulazima gani wa kufanya kazi ya Zimamoto wakati tulikuwa na miezi nane ya maandalizi toka January 2024?
Hii ni sikukuu kubwa sana kwa Mkulima wa Tanzania, sasa kama Wizara husikawanashindwa kuifanyakazi hii kwa ufasaha na kuacha UFISADI uharibu shughuli, tunadhani nini ndio njia sahihi kumuokoa Mkulima wa Tanzania?