A
Anonymous
Guest
Nimepenyezewa taarifa zenye uhakika kwamba tarehe 10 Desemba 2024 kumefanyika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi almaarufu TAFCA ambalo ofisi zake zipo Magomeni Kagera
Narudi nyuma kidogo. Mnyetishaji amenielezea kuwa Mkutano Mkuu wa TAFCA uliofanyika mnamo tarehe 18 Desemba 2023 uligubikwa na malalamiko mengi yanayohusu utaratibu wa wadau wa sanaa kupata mkwamo mkubwa kwenye maombi ya mikopo kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.
Katika Mkutano huo ulioendeshwa na rais wa Shirikisho ulikosa majibu kwa sababu hakukuwepo na mwakilishi kutoka Mfuko huo, hivyo Mkutano huo uliazimia kuunda Kamati itakayokusanya changamoto na maoni ya wadau ili kuyakabidhi kwenye shirikisho hilo wayapeleke mamlaka husika na majibu yatoke.
Kamati inasemekana ilimaliza kazi yake mapema Januari 2024. Lakini kutokana na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuwa ni chawa wa Rais wa TAFCA walimfikishia taarifa za siri kuwa miongoni mwa kero walizokusanya ni tuhuma dhidi ya rais wa shirikisho kushinikiza, kuomba na kupokea rushwa ya Tzs 3,000,000 ili wahusika wapate mkopo ndani ya siku tatu.
Taarifa zaidi zipo kwenye attached document ya taarifa ya Kamati iliyosomwa. Hivyo baada ya danadana ndefu hatimaye Kamati ilikabidhi taarifa yake mnamo Aprili 2024 kwa Bodi ya TAFCA. Inasemwa na mnyetishaji ndani ya shirikisho kwamba Bodi ya TAFCA waliamua kumkingia kifua rais wa Shirikisho kwa kuificha taarifa isitoke kwa umma wala mamlaka husika.
Bodi ya TAFCA walifanya attempt moja kuizima hoja kwa kuwaita waliotoa tuhuma ili kuwaambia madai yao hayana mashiko.. lakini siku waliokaa nao ndipo mapya yakaibuka. Walalamikaji walitoa ushahidi wa mawasiliano ya simu yaani sauti na SMS zote alizowasiliana rais kushinikiza apewe pesa hizo ili awakatie watu wa benki watoe fedha haraka.
Inasemekana, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo anazo taarifa hizi na ushahidi wote tangu August 2024 lakini hajachukua hatua yeyote. Pia katika Mkutano Mkuu wa TAFCA hapo jana ulihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa BASATA ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Kwa kuwa walalamikaji ni wajumbe wa mkutano mkuu, walipata nafasi kikaoni kumkumbusha wametapeliwa pia wamepewa rushwa na rais wa TAFCA walimfikishia malalamiko lakini mpaka jana wanaona kimya. Katibu Mtendaji alikiri suala hilo wanalo na akawaomba wasiende kokote kwa kuwa amewaagiza wanasheria wake wawaite ili kuwapatanisha na mtuhumiwa.
Inasemwa alimpigia simu mkuu wa kitengo cha sheria BASATA palepale ambapo alimjibu hajaanza kulishughilikia jambo hilo.....
Taarifa zaidi inasema kwamba, baadhi ya vyama vinavyounda TAFCA walipata fununu ya kukaliwa kwa taarifa ya kamati na uozo uliomo. Walijiorodhesha kuomba Mkutano Mkuu wa Dharura mnamo Oktoba 2024 ambapo Kifungu cha 6 A (iv) cha katiba ya TAFCA kimenukuliwa hapa;
iv. Kama ilivyoelezwa katika kifungu cha 6, A (i) Pia kutakuwepo
Mkutano Mkuu maalumu au wa dharura, iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo
Lakini Bodi ya TAFCA chini ya raiswa shirikisho iligoma kuitisha mkutano wa dharura kupokea na kujadili taarifa ya kamati.
Mkutano mkuu wa jana ulipaswa kufanyika tarehe 05 Desemba 2024 kwa mujibu wa ratiba na wajumne walitumiwa mwaliko. Lakini Bodi ya TAFCA chini ya rais wake ilifuta na kuhamishia tarehe 10 ambayo ni jana. Mtoa taarifa anasema agenda za mkutano wa jana hakukuwepo na agenda ya kupokea taarifa ya Kamati. Lakini baadhi ya wajumbe walishinikiza taarifa isomwe na ikasomwa, mwishoni mwa taarifa rais wa TAFCA alizuia usikilizwaji wa voice notes huku akidai kuwa Katibu Mtendaji wa BASATA amezuia taarifa isijadiliwe na mkutano huo kwani wanalifanyia kazi suala la tuhuma dhidi yake.
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la sanaa za Ufundi Tanzania (TAFCA), kiongozi akivunja Kifungu cha 9 (i), (ii) kama kilivyonukuliwa hapa:
KIFUNGU CHA 9
Miiko ya Kiongozi/Mjumbe
Kiongozi au Mjumbe wa Bodi atapoteza sifa na kusimamishwa au kupewa
hadhabu endapo atakiuka miiko ya Shirikisho ikiwepo ifuatayo.
I. Kulitumia jina la TAFCA ikiwemo kukusanya na kupokea michango ya
fedha na mali kwa Manufaa yake Binafsi.
II. Kutoa ama kupokea rushwa.
Kumbe Mkutano Mkuu wa Shirikisho ulikuwa ni sehemu sahihi kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kaatiba yao, lakini mamlaka ya usajili (BASATA) iliingilia kuzuia hatua zisichukuliwe huku ikiacha hewani muda uliojiwekea kufikia hatma ya sakata hili.
Inasemekana Rais huyo wa Shirikisho bwana Adrian Nyangamale amekuwa akilindwa dhidi ya ubadhirifu mwingi ndani na nje ya Shirikisho hilo. Kwenye sakata hili inaleta mashaka ukimya wa Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni, Michezo na Habari.
MY TAKE:
Tunaiomba Serikali kuwachukulia hatua watu wote wanaohujumu juhudiza kukwamua sekta ya sanaa wanaoweka maslahi binafsi mbele badala ya kutimiza wajibu wao muhimu.
Serikali iwamulike na kuwachukilia hatua viongozi ambao wanatumia nafasi na mamlaka walizopewa kutetea maovu na ufisadi ndani ya sekta
TAKUKURU ichukue hatua ya kuchunguza yanayojiri kwenye mchakato wa utoaji mikopo ya Sanaa na Utamaduni kwani katika taarifa ya kamati, kuna rushwa na uozo unaokwamisha utoaji wa mikopo
Nawasilisha