DOKEZO Ufisadi mwingine wa Kutisha Halmashauri ya Rorya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Obwere Kabwana

New Member
Sep 20, 2023
3
5
Ufisadi wa Kutisha Halmashauri ya (W) Rorya

Waziri wa Tamisemi Mhe Mchengerwa

Kamanda Mkuu wa kupambana na Kuzuhia Rushwa (PCCB)

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa

Tunawaomba mtume wataalam waje wachunguze ufisadi unaoendelea katika Halmashauri ya Rorya

Kuna kiasi cha Tzs 661,000,000 za Ujenzi wa Shule ya Secondary Koryo Zimeamishwa na Ofisi ya DED bila kupitishwa na Kamati ya Fedha na Mipango

Kiasi cha TZs 331,000,000 zimepelekwa katika ujenzi wa Shule ya Secondary Nyamagaro wakati Shule imeshajengwa ( Doule allocation)

Barabara zinajengwa chini ya kiwango Madiwani wakioji wanaambiwa wakae kimya ni mradi wa Viongozi wa Chama Wilayani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ameojiwa na kikao cha Kamati ya Fedha na Mipango ameshindwa kutoa Majibu ya Kuridhisha

Tuna imani na ofisi zenu tunaomba mtume kikosi kazi kije kuchunguza Ufisadi unaoendelea katika Halmashauri ya Rorya.
 
Pale Rorya kuna mitifuano sana!
Majengo ya halmashauri ya wilaya yamepelekwa maporini huku ofisi za watendaji zikisambazwa Utegi na Shirati!
Kuna barabara ya lami kila mwaka inajengwa na haijawahi kuisha!
Kuna madaraja yamejengwa mto Mori.
Funga kazi ni mradi wa kufunga taa za solar barabarani... Kuna taa chache zimefungwa pale Utegi barabara ya kwenda Kowaki.
Kimsingi serikali kuu na wizara husika ziingilie kati! Rorya kuna upigaji mkubwa sana!
 
Ufisadi wa Kutisha Halmashauri ya (W) Rorya

Waziri wa Tamisemi Mhe Mchengerwa

Kamanda Mkuu wa kupambana na Kuzuhia Rushwa (PCCB)

Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa

Tunawaomba mtume wataalam waje wachunguze ufisadi unaoendelea katika Halmashauri ya Rorya

Kuna kiasi cha Tzs 661,000,000 za Ujenzi wa Shule ya Secondary Koryo Zimeamishwa na Ofisi ya DED bila kupitishwa na Kamati ya Fedha na Mipango

Kiasi cha TZs 331,000,000 zimepelekwa katika ujenzi wa Shule ya Secondary Nyamagaro wakati Shule imeshajengwa ( Doule allocation)

Barabara zinajengwa chini ya kiwango Madiwani wakioji wanaambiwa wakae kimya ni mradi wa Viongozi wa Chama Wilayani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ameojiwa na kikao cha Kamati ya Fedha na Mipango ameshindwa kutoa Majibu ya Kuridhisha

Tuna imani na ofisi zenu tunaomba mtume kikosi kazi kije kuchunguza Ufisadi unaoendelea katika Halmashauri ya Rorya.
Barabara zinajengwa chini ya kiwango Madiwani wakioji wanaambiwa wakae kimya ni mradi wa Viongozi wa Chama Wilayani.🥺🥺🥺Duh
 
Wanakula kwa urefu wa kamba yao.
Tz watu wengi wanataka pesa bila jasho - watu wenye nafasi wanawaza wizi tu - Nani atamfunga paka kengere - wote tuko kaa panya tu
 
Back
Top Bottom