UFISADI: Mpina aibua tuhuma za upigaji wa Sh. Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
609
1,420
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameibua tuhuma nzito bungeni kuhusiana malipo ya shilingi triliioni 1.5 ambazo hazijulikani zilipo alizotakiwa kulipa Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kama malipo ya CSR na faini kuchelewesha mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa miaka miwili kinyume cha mkataba.

Mpina alikuwa akichangia bungeni Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2022/23 bungeni Novemba 9,2022 ambapo aliomba Bunge kuiagiza Wizara ya Nishati na TANESCO kuhakikisha fedha hizo zinalipwa ili ziende zikatumike kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya watanzania.

Mpina alisema kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya BAJETI muda ulioongezwa katika mkataba baina ya TANESCO na Mkandarasi Arab Contractors haujulikani hadi sasa kwamba ni miezi 12 au miezi 24 kwani Taarifa ya TANESCO kwenye kamati ilionyesha mkandarasi ameongezewa muda hadi 15 Juni, 2023 kukamilisha mradi lakini Wizara ya Nishati inasema muda ulioongezwa miaka miwili hadi hadi Julai, 2024 hivyo kuwepo mkanganyiko mkubwa.

Pia Mpina aliomba kuundwa Kamati Teule ya Bunge ili kubaini ukweli na chanzo cha mkanganyiko wa taarifa zinazotolewa na Wizara ya Nishati kuhusiana na ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere na kupendekeza hatua za kuchukua.



PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
Back
Top Bottom