Kufuatia zoezi la utumbuaji vipere,majipu na matezi imebainika kuwa Shirika la Viwango Tanzania kuna majipu yaliokomaa na kugeuka kansa rushwa ..Tuhuma husika za ufisadi zinayohusisha utolewaji wa shehena za mizigo zisizokidhi viwango kimataifa vya ubora katika uzalishaji wake.
Nini kinafanyika,Waagizaji hasa wa bidhaa hafifu kiviwango hufanya uagizaji pasipo bidhaa husika kuthibitishwa na mashirika ya viwango ya kitaifa {TBS} na kimataifa.
Baada ya bidhaa husika kufika bandarini Dar es salaam,wafanyabiashara kwa kushirikiana na Mwakala wa forodha {clearing and Forwarding agents} huwaonga maafisa viwango waliopo bandarini au katika ofisi zao zilizopo jengo la Diplomat-Mkwepu ili kupata approval au barua za kughushi ubora wa bidhaa pasipo hata kukagua n.k.
Malipo ya rushwa husika hufanywa kwa siri {fedha taslimu,Tigo pesa,Mpesa} na uwa kwa viwango vya TZS1,000,000 ,TZS 1,200,000 mpaka TZS 5,000,000.Maafisa viwango wengi ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na kuomba na kupokea rushwa wameweza kujilimbikizia mali nyingi sana .
Tuhuma hizi zinakuja wakati ambapo makampuni mengi ya forodha yapo kwenye sakata ya ukwepaji wa ulipaji wa tozo za utoaji mizigo bandarini.