sasa mkuu..! mchana unaanzaje kulala masaa mengi, wakati nje kuna kelele za watu, Jua nje limewaka hadi mwisho, kelele za milango huyu anatoka yule anaingia..
Ukitaka ulale sana mchana, Subiri ule wakati, nje kuwe na kimvua fulani kaubaridi kwa mbali kiasi kwamba hata nje harakati za watu hakuna, halafu hakuna usumbufu wowote ule kutoka kwa mtu yeyote yaani kila mtu awe ametulia chumbani kwake, uone kama hujaunganisha hadi usingizi wa usiku, halafu unakuja kuamshwa na njaa tu!