UENDESHAJI KAMPUNI: KUMTOA MWANAHISA.

Bexb

JF-Expert Member
Oct 24, 2016
690
1,503
Habari ya majukumu wakuu. leo nataka tuzungumzie suala hili kidogo kwani nimekua nikipata maswali juu ya suala hili kwa watu kadhaa kutoka hapa JF. Wengi wamekua wakiuliza namna ya kuwatoa baadhi ya wanahisa katika kampuni lakini wamekua wakikwama katika hilo kutokana na sababu mbalimbali hivyo, si vibaya leo tukaangazia mawili matatu.
Kimsingi kuna namna mbili kuu za kumtoa mwanahisa kutoka kwenye kampuni na njia hizi mbili ndio kuu na zilizozoeleka kutumika njia hizo ni kaa ifuatavyo;
1. KUNYANG'ANYA HISA AMBAZO HAZIJALIPIWA(FORFEITURE OF UNPAID SHARES).
Hii hutokea mara nyingi pale ambapo mwanahisa hajalipia hisa zake kutokana na sababu mbalimbali. wakati wa usajili wa kampuni huwa kuna kipengele cha kugawanya hisa kwa wanahisa wote kulingana na makubaliano yao ama uwezo wao kwa vile walivyoamua. hivyo, kila mmoja atatakiwa kulipia hisa zake kwani hutambulika kuwa ndio mtaji wa kampuni husika. Sasa ikitokea mmoja ama baadhi ya wanahisa hajalipia hisa zake basi humaanisha kuwakwamisha wenzake katika kuendeleza kampuni hivyo kutakiwa kupisha ili wengine waliomudu waweze kuendelea na biashara ama shughuli mahsusi za kampuni.
Ili kuweza kulitekeleza jambo hili, BRELA huhitaji baadhi ya nyaraka zinazothibitisha suala hili na mara nyingi huwasiliana na hao wanaotolewa ili kuthibitisha kama maomb hayo ni halali hivyo hapa tutahitaji ruhusa ama dhamira ya dhati ya huyu mwanahisa anayetolewa kwa kuambatanisha baadhi ya nyaraka kuthibitisha ridhaa hiyo.
Changamoto ya njia hii huwa pale ambapo mtu ambaye hajalipia hisa zake hatoi ushirikiano wowote na kimsingi hataki kutoka katika kampuni hutakiwa kupelekwa mahakamani kisha uamuzi husika ndio uwasilishwe BRELA lakini kama muhusika yupo tayari, basi huwa ni njia rahisi zaidi ya kumtoa mwanahisa kwani huwa na ridhaa ya mwanahisa mwenyewe.
Pia changamoto nyingine huja pale ambapo unakuta kampuni hii ina zaidi ya mwaka mmoja na katika mahesabu ya mwaka ya kampuni(Annual Audited financial statement) kulioneshwa na Mhasibu kuwa ALL SHARES ARE PAID) hapo ndipo kivumbi hutokea maana nyaraka ambazo ziliwasilishwa TRA na zilithibitishwa na mkurugenzi wa kampuni husika zinaonesha kuwa hisa zote zililipiwa.
2. UUZAJI WA HISA(SALE OF SHARES)
Hii ni njia mabayo ni maarufu zaidi kwani mwanahisa anapouza hisa zake zote katika kampuni basi anakua amejitoa 'automatically' katika kampuni husika na hutakiwa kuandaliwa nyaraka kuthibitisha suala husika kisha kuzipeleka TRA kwa ajili ya kulipia kodi mahsusi za mauzo hayo kisha kuwasilisha hiyo 'tax clearance' sambamba na nyaraka nyingine huko TBRELA kwa ajili ya utaratibu wa kumtoa huyo aliyeuza hisa na kumwingiza katika database huyu mnunuaji mpya.
Katika utekelezaji wa suala hili, TRA watatoza kodi husika kwa kuzingatia masuala mawili aidha iwe ni thamani ya mauziano halisi ya hisa ama iwe ni thamani halisi ya hisa kulingana na kampuni husika, kwa hiyo ile itakayokua juu ndio itatchukuliwa kwa minajiri ya kutoza kodi.
MUHIMU: Tukumbuke kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi ni kuwa kampuni inapswa kuwa na wanahisa kuanzia WAWILI. Hivyo katika kutekeleza mchakato wowote hapo juu hakikisha kampuni inabaki na watu kuanzia wiwili na endapo itatokea mlikua wanahisa wiwili basi mnapaswa kuandaa nwanahisa mpya wa kuingia kabla ya huyo mmoja kutolewa ili kukidhi kigezo hiki cha kisheria.

Kama kuna lolote la kuongezea basi karibuni wadau.

0755963775 calls|WhatsApp​
 
Tupe elimu kuhusu holding company. Je mwanahisa wa holding campany flan anaweza kuwa mmiliki wa subsidiary inayomilikwa na holding company husika?
 
Ndio inawezekana kabisa na haina shida
 
kwa namba 1 ikitokea mwanahisa anataka kujiondoa katika kampuni yenye zaidi ya miaka say 7 na yuko tayari kupoteza/kuziacha hisa zake utaratibu unakuwaje? Bexb
 
Habari mkuu, utaratibu nimeuelezea hapo juu, ukijiangali kuna sehemu unaangukia? Je katika miaka hiyo 7 kuna mahali katika vitabu vyenu vya audits vimesema kuwa mlishalipia hisa zenu? Kama ndivyo basi kuna suala la transfer of shares. Kama hakuna basi tunaweza kuangukia kwenye forfeiture na pia kama unaona hizo options hazikufai basi itabidi tuangalie memart kama imetoa nafasi ya mwanachama kufanya surrender of share kwa kampuni
 
Back
Top Bottom