Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,669
- 119,297
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali kuhusu Huu udikiteta unaozungumzwa sana kwenye mitandao kuwa Tanzania tunatawaliwa kidikiteta, na watu kudai kuwa rais Magufuli ni dikiteta hadi kutaka kuandamana tena hiyo tarehe 26/04/2018. Hili ni bandiko la swali kuhusu huu udikiteta, kwanza kama ni kweli upo, au ni dhana tuu ya watu waliofilisika kisiasa, baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi huru na wa haki, hivyo hoja ya udikiteta ni dhana tuu ya kizushi, kwa hoja kuwa Tanzania hakuna udikiteta wowote, bali ukweli ni kuwa Tanzania ilikuwa ni nchi iliyopinda sana kwa miaka mingi kwa rushwa, ufisadi, ubadhirifu na uzembe, anachokifanya rais Magufuli ni kuinyoosha nchi hii iliyopinda ili ikae kwenye mstari, na ni katika kunyoosha huku, watu waliopinda na kuipindisha, lazima wanyooke, na katika kunyooka huku, wanaumia, na ndio hawa wanaopiga hizi kelele za udikite Tanzania?.
Sio mara moja au mara mbili, Tanzania imekuwa ikizungumziwa kuwa inatawaliwa kidikiteta, Vyama vilivyounda UKAWA, vikahamasisha maandamano nchi nzima kwa jina la UKUTA, ili kupinga udikiteta, serikali ikatumia nguvu zake zote kuyapinga, na kweli yakasitishwa, sasa Watanzania kote ulimwenguni, wamahamasishwa kujitokeza tena kuandamana siku ya tarehe 26 April,mwaka huu 2018 ili kupinga udikiteta ambayo nayo tayari yameisha pigwa marufuku.
Hivyo hii mada ya kujiulizwa swali moja tuu kuhusu huu udikiteta unaozungumzwa nchini Tanzania, Jee ni kweli Tanzania tuko kwenye utawala wa kidikiteta?, Jee ni kweli rais Magufuli ni Dikiteta?. Andamana name.
Hapa swali la msingi ni jee huu udikiteta unaozungumzwa nchini Tanzania ya leo, ni kweli upo na una exist in reality au ni uzushi tuu wa jambo la kufikirika tuu ndani ya mawazo ya watu waliofilisika kisiasa baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi huru na wa haki, sasa wana zusha dhana za kizushi udikiteta ili tuu kujifariji na kipigo cha mwereka kwenye sanduku la kura?.
Tangu baada ya kuibuka kwa dhana ya udikiteta nchini Tanzania, nimeanza kushuhudia baadhi ya watu na taasisi zikianza kutoa matamko na kauli za kujiumauma na kujichanganya kuhusu udikiteta, huku wengine wakitoa kauli za kujikombakomba, wengine wakiongea kwa uoga uoga kuhusu huu udikiteta, huku wengine wakiamini kabisa kuwa Tanzania tuko kwenye udikiteta na wengine wakisema hakuna udikiteta Tanzania , ali mradi kila mtu anasema lwake!, hivyo ili kumaliza ubishi, naomba kwanza kibali chenu tumfufue kidogo Baba wa Taifa, hili, Mwalimu Nyerere tumuulize kwanza, kiongozi mwenye udikiteta ni kiongozi wa namna gani au ni kiongozi mwenye tabia gani?.
Msome Mwalimu Nyerere kuhusu udikiteta na hapa nina mnukuu...
View attachment 378704
Tena Mwalimu Nyerere, hakuishia hapo, miaka mingi nyuma, alizungumza kama Nabii, kuhusu huu udikiteta unaozungumzwa sasa nchini Tanzania, tena wengi wa kizazi cha sasa, maneno ya Mwalimu Nyerere wanafanya kuhadithiwa tuu kama hadithi, lakini mimi nakiri kuwa nilikuwa ni mmoja miongoni mwa watu wachache wenye bahati ya kuwepo mahali Mwalimu alipozungumzia udikiteta na kumsikia Mwalimu akizungumza sio tuu kwenye redio , RTD ya enzi hizo, bali kwa kukaa chini kwenye sakafu ya kiambazani cha nyumbani kwake Msasani maana viti vilijaa waandishi wakubwa zetu wa enzi hizo, sisi tukiwa ni waandishi wachanga, tukiwa TSJ, nakumbuka ilikuwa ni 1993 au 1994,
naomba pia niwasaidie wavuvu wa kusikiliza video. kwa kuwaandikia Mwalimu amesema nini na hapa ninamnukuu
“Tujenge utamaduni wa kudhibiti viongozi wetu kama wanavunja sheria ya nchi (Katiba) tusiogope, mkianza, mkiwa na woga, I’m, I promise you, mtatawaliwa na dictators, (huku anacheka), I promise you, mkiogopa ogopa namna hii, nyinyi, wabunge, nani, wote mkiogopa ogopa, mkisema mzee wanakuwa wakali, then you are making it absolutely certain, you will be under a dictatorship" mwisho wa kunukuu.
Na baada ya kumsikia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akizungumzia sifa za kiongozi dikiteta, na kusema iwapo kutajitokeza kiongozi mwenye sifa hizo, Watanzania tunatakiwa kufanya nini, kabla hatuja kwenda huko kwa tunatakiwa kufanya nini, hatua ya kwanza ni kujiuliza, jee hapa tulipo ni kweli tuko kwenye udikiteta?. Rais Magufuli ni kiongozi dikiteta?.
Hatua ya kwanza, ni kujiuliza, huu udikiteta ni nini, na viongozi madikiteta ni nani?.
Hivi karibuni, Wanasiasa wa Upinzani wamekuwa wakimuelezea Rais Magufuli kuwa ni dikteta na anakiuka misingi ya demokrasia. Msingi wa malalamiko hayo ulitokana na kauli ya Rais kuwa Sasa ni muda wa maendeleo, kufanya siasa hadi 2020. Hii ilienda mbali hadi kutangazwa kwa maandamano yaliyopewa jina la UKUTA (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania). Maandamano haya yalikuwa na lengo la kudai haki ya kufanya siasa kwa vyama vya upinzani na pia kudai uhuru wa kujieleza kwa wananchi.
Taasisi ya TWAWEZA kupitia Sauti za Wananchi, ambao hukusanya maoni ya wananchi kupitia simu za mkononi kuhusu kinachoendelea nchini katika nyanja zote za maisha, imetoa Ripoti ya maoni ya wananchi kuhusu demokrasia, udikteta na maandamano nchini.
Utafiti wa Taasisi ya Twaweza, haukutoa maana ya udikiteta bali umetumia mfumo wa kutumia hojaji, kuuliza kuhusu demokrasia na udikiteta, matokeo yake ni haya.
=> Takwimu: Mwananchi 1 kati ya 3 alitoa maana ya neno “udikteta” akilitafsiri kama kutawala kimambavu.
=> Takwimu: 15% wanalitafsiri neno udikteta kama mtu mmoja ndiye mwenye maamuzi nchini, 6% wamelitafsiri kama ubaguzi.
Baada ya kutoka kwa ripoti hii ya Twaweza, mimi binafsi kwanza niliwapongeza Twaweza, kwa kitendo chao cha kishujaa kuhoji kuhusu dhana ya udikiteta, maana sii wengi wenye ujasiri kuwa kuuzungumzia udikiteta wa Tanzania, haswa kwa kuzingatia, anayezungumziwa ni rais wa Jamhuri, Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu, hivyo niliwapongeza Twaweza kwa ushujaa huu, ila mwisho wa utafiti huu, Twaweza nao, walituacha solemba, kwa kutokusema huu udikiteta ni nini haswa na jee Tanzania tuna udikiteta ama tunatawa;iwa na dikiteta au la?. Twaweza waliyachukua matokeo ya utafiti wao na kwa kuchapisha tuu maoni ya wananchi kuhusu udikiteta bila kuusema au kuizungumzia status ya Tanzania.
Kwa vile dhana ya udikiteta ni dhana pana na pia ni dhana mtambuka, nitaizungumzia kwa udani katika makala ijayo, ila kwa vile kuna watu wanapanga tena kuandamana siku tarehe 26 April, na serikali imeishayapiga marufuku maandamano hayo, wito wangu sio kwa jeshi la polisi kuyaachia maandamano hayo, polisi wao waendelee kutimiza wajibu wao kuhakikisha nchi inakuwa na salama, amani na utulivu, bali natoa tuu angalizo kuwa sio kila maandamano ni maandamano ya kuleta fujo na vurugu, bali mara nyingi, tumeshuhudia fujo na vurugu zikisababishwa na polisi katika kuzuia maandamano, na mfano hai ni tukio la hivi majuzi la kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwiline, kilichosababishwa na risasi, iliyofyatuliwa na polisi kuzuia maandamano!. Nimeyashuhudia maandano yale kwenye video, watu wanaandamana wameshikana mikono bila silaha yoyote, halafu polisi wanawatawanya lwa silaha za moto!.
Kwa vile huu udikiteta wa rais Magufuli unazungumzwa sana, mimi nilifanya juhudi kuwatafuta maprofesa wa sheria kuwauliza, nikaanzia kwa Prof. Issa Shivji na Prof. Chriss Peter Maina, hawakunijibu kitu, bali walionyesha tuu ishara za mikono kuwa wao hawako tayari, kulizungumzia hili, bado nitafanya juhudi kumtamfuta Waziri wa Sheria, Prof. Palamafamba Kabudi, Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu kulizungumzia hili. Hivyo naomba usichangie kwanza uzi huu, nisubiri nakuja kumalizia kwa kuelezea ili kujua kwa uhakika, jee ni kweli Tanzania kuna udikiteta, tunatawaliwa kidikitea na jee rais Magufuli ni dikiteta?.
Nawatakia Furahi Dei Njema.
Paskali
Update1
Hii ni update from very objective contribution kuwa rais Magufuli sio dikteta.
Paskali
Update 2.
Huu ni mchango very objective kuwa rais Magufuli ni dikiteta.
Paskali
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade!"Dikiteta ni Mtu Mwenye Tabia Hizi!".
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka Ukweli!. Dawa ya Uongo ni Ukweli.

Thanks Wilderness Voice for objectivity yako kuwa rais Magufuli sio Dikiteta.Udikiteta kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni utawala wa mabavu usiyofuata misingi ya sheria iliyowekwa katika nchi hivyo uondoa matakwa yote ya kidemokrasia toka kwa wananchi na kujilimbikizia nguvu za maamuzi kisiasa, kiuchumi na kufanya mfumo wa uongozi wenye vitisho, mabavu, na wenyekutojari haki na misingi ya utu au ubinadamu.
Je, Magufuli ni Dikiteta? Nacho jiuliza hapa wanasiasa hasa wa upinzani, baadhi ya wana CCM ambao walitegemea kunufaika kupitia mgongo wa nyuma, na baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatakipato kwa njia zisizo halali wengi wao ndiyo walio shupalia kumuita Rais Magufuli Dikiteta. Tena wanaongea kwa uchungu unaona wazi wanavyoonesha chuki zao za kukoswa walicho kitarajia. Mfano vyama vya upinzania hasa CHADEMA kilijipambanua kwa kupigania wananchi na hasa kupinga ufisadi, uzembe wa serikali na upotevu wa maliasili zetu kwa kuziacha zipotee kwa kuingia mikataba mibovu. Kupitia hili tuliona serikali ikiwajibishwa baadhi ya viongozi wakijiuzuru nafasi zao na baadhi ya wanasiasa toka vyama vya upinzani kujipatia umaarufu.
Sasa hali leo ikoje. Kila mtu anafahamu japo wengine hawapendi kusema ukweli Magufuli kabadili upepo wa kisiasa nchini hasa baada ya kushughulika na hoja zote za wapinzani walizozoea kuzitumia kama vile kurekebisha utendaji wa serikali na kufanya watumishi kuwajibika kwa wananchi leo huduma katika maofisi ya serikali imeongezeka. Kupitia masuala ya mikataba ya madini hasa kuangali Taifa litafaidika vipi, Kukaba mianya yote ya rushwa na kushughulikia mafisadi, na mengineyo mengi. Wapinzani wa Tanzania wamejikuta hawana hoja na ubunifu mwingine wameamua kumshambulia mtu mmoja kufuatana na wajihi wake badala ya kuleta hoja mtambuka kwa Taifa. Mfano nilimsikia Mbowe mwenyekiti CHADEMA katika uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni akimuongelea Magufuli kama yeye binafsi kwa kusema... naomba kunukuu "Magufuli ni nani kwani...nikajitu kamoja kafupi hivi...." mwisho wa kunukuu! Hii ni kukoswa hoja na kuanza kuingilia utu wa mtu. Kwanini lisiongelewe suala linalohusiana na manufaa ya Taifa kuliko kumongelea mtu binafsi wajihi wake? Hapa inaonesha Wapinzani hawana hoja ya kuwaeleza wananchi. Wamebaki kushambulia mtu binafsi kama Magufuli. Kama ulikuwa nae Bungeni ni wakati huo...lkn sasa ni Rais. Ndo maana wapinzani wanashindwa katika chaguzi wanabaki kulaumu. Watanzania si wajinga ila upenda kusikiliza na inapofika maamuzi utafakari ni nani wampe kura kwani wapinzani hawana hoja sasa wamebaki kuongelea mtu binafsi. Ukienda katika mikutano awaongei nini watafanya sera zao wamebaki kulalamika Magufuli dikiteta, Lisu kapigwa Risasi, Mwanafunzi kauwawa. Haya mambo si ya kwanza kutokea leo nchini. Toka nipo mdogo nikiwa na miaka 8 nakumbuka mtu mmoja aliuwawa kwa kupigwa risasi na alikuwa na cheo kikubwa tu kisiasa. Nilisoma na watoto wake. Nilishuhudia watu kuuwawa, watu kupotea. Hii hata katika nchi nyingine zilizoendelea yapo sana. Je haya ndo tunasema ni udikiteta? Je kwanini tumuhusishe Rais kwa mambo tusiyokuwa nayo ushahidi? Kusema hivi si kwamba natetea mambo mabaya yanayo tokea la hasha ni ktk kutoa picha kwamba anacholaumiwa nacho Rais Magufuli siyo wala si yeye anae fanya. Nakumbuka mchezaji mmoja toka timu ya taifa ya Colombia alisababisha timu ya nchi yake kufungwa na kurejeshwa nyumbani, aliporudi shabiki mmoja alimpiga risasi na kumuuwa mchezaji huyu kisa tu aliona hakuwa mzalendo na kusababisha timu yao kufungwa. Lisu kupigwa Risasi kwanini tuhusishe na serikali hasa Rais Magufuli. Jambo laweza kufanywa na watu wengine kwa lengo lao kwa nini kumuhusisha rais bila kuwa na ushahidi timilifu.
Nje ya nchi Magufuli anasifiwa sana. Ni dikteta gani nchi nyingine zinamuongea vizuri. Make madikteta wengi walifahamika duniani waliongewa vibaya. Nchi zilizoendelea ni kazi kazi tu. Siasa na porojo uisha kipindi cha kampeni, baada ya hapo ni kuwajibika. Watanzania tulizoea kila siku siasa vijiweni. Sasa Magufuli kaleta mabadiliko watu waliozoea wanaona siyo. Magufuli hajazuia mikutano bali kaweka utaratibu wa mikutano hiyo. Hivyo hakuna katiba iliyo vunjwa watu bado wana uhuru wa kujieleza, na ndiyo uhuru huo wanautumia kwa kusema Magufuli ni Dikiteta. Hivi uwe na rais dikiteta unaweza kweli toa hayo matamshi kwa kuita waandishi wa habari? Nadhani watanzania hatufahamu udikiteta ni nini?
Wapinzani wanatukana na wakati mwingine kutaka kumchonganisha rais na wananchi, je waachwe tu kisa wao ni wanasiasa wakichukuliwa hatua inasemwa Magufuli dikiteta. Pascal umesoma Sheria nini maana ya mtu kutukanwa au kudharirishwa. Sheria inaruhusu mtu akikutukana umfungulie mashitaka. Je kwa nini Rais atukanwe eti awa watu waachwe kisa wao wabunge. Kwani mbunge kuchaguliwa na wananchi ndo upo tayari kutukana. Mie nadhani upinzani Tanzania wanahitaji semina elekezi kujua nini maana ya upinzani kwa manufaa ya Taifa na si kum...attack mtu "Rais"
Nadhani watu wanatafsri vibaya maana ya demokrasia. Demokrasia inamipaka yake kwa kufuata sheria za nchi. Swala la kuandamana Mayala sikubaliani nawe kuwa polisi ndo uanzisha vurugu hapana, waanzisha vurugu nipale unapoanzisha maandamano yasiyo na kibali na unapoambiwa utawanyike hutaki unategemea polisi wakuache. Kutotii amri halali ya polisi ni kuvunja sheria. Maandamano yanaruhusiwa ila kuna taratibu zake. Swala la tarehe 26/04/2018 watu kuandamana mie niseme hizo ni porojo tu, huyo mtu anaejifanya anauchungu na nchi yeye yupo Marekani. ebu Tazama wapamabanaji wote walipambana wakiwa nchini mwao. Huyu analengo la kuvuruga amani ya nchi tu hana chochote. Nachoamini hakuna maandamano. Pia Hata Yesu alipingwa na watu wa dini na ni hao hao watu wa dini waliomuuwa Yesu. Raisi Magufuli atapingwa na kila mtu asiye jua nini Magufuli anafanya kwa Taifa hili. Lakini Hakuna atakae muondoa Rais kwa kutunga na kuweka au kujenga chuki za kizandiki. Hakuna sehemu nchi imeendeshwa bila kufuata sheria na taratibu za nchi. zaidi watanzania tulivunja sheria na taratibu za nchi na kufanya tutakavyo kwakuwa Rais anaturejesha kwenye mkondo tunaona shida. Rais si dikiteta bali udikiteta upo vyama vya upinzani wanao badili katiba ili waendelee kuongoza uenyekiti. Na ndiyo waamuzi wa mwisho. Kunamuda nilikuwa nje ya Nchi nikamuuliza mtumishi mmoja nasikia huko vyuma vimekaza hali mbaya kwa watumishi wa Umma. Huyu mtu tena ni mdada akaniambia nanukuu.... "mie naoana maisha si mabaya kwani nilichokuwa nikikipata naendelea kukipata sikuwa nategemea semina au kujipatia hela kwa dili, hivyo naona sawa tu, ila waliokuwa wanaishi kwa madili hao wanapata shida" Mtumishi huyu wa serikali namfahamu amekuwa mtenda haki na si mpokea wala mtoa rushwa. Anatenda haki tu, na ni mwajibikaji. Hivyo Udikiteta wa Raisi Magufuli unatamkwa na wale watu waliotegemea maslahi fulani toka serikalini au katika nyanja kadhaa. Huku nje Rais Magufuli anasifiwa japo jitiada za kumchafua zinafanyika lakini hakuna kilichoharibika na bado wanamuona ni rais anaetaka kuleta maendeleo ya nchi yake. Ni shauri wapinzani wajikite kuangalia ni namna gani ya kuja na hoja za maana ili kufanya upinzani hudumu na si hivi sasa kukalia Majungu tu. Hakuna la maana imebaki mipasho. Hata humu Jamii forum hoja zinazo pewa kipa umbele ni zile zenye kuonesha unaipinga serikali hakuna utaifa.
MWACHENI RAIS AFANYE KAZI NA KUTEKELEZA ALIYO AHIDI. RAIS MAGUFULI SI DIKITETA
Paskali
Update 2.
Huu ni mchango very objective kuwa rais Magufuli ni dikiteta.
Asante sana field marshall1 kwa objectivity yako kuwa rais Magufuli ni dikiteta.Nimependa thread yako. Naomba niseme ukweli....Nothing else but only truth" MAGUFULI ana kila kiashiria cha udikteta tena ule ambao ni level ya wale madikteta wanaofanya jambo kwa kukomoa kwa sababu tu wana uwezo wa kufanya bila ya yeyote kumuuliza! Definition ya "Dictator"ameeleza Nyerere vizuri sina haja ya kurudia, Kamusi imeeleza pia dikteta ni mtu wa namna gani, wana tabia za namna gani n.k.
Ukiangalia tabia za madikteta hakuna shaka kabisa huyu ndiye dikteta wa kwanza ambaye tunaye katika historia ya nchi yetu. Waangalie Paul Kagame, Yoweri Museveni na Joseph Kabila
(Bahati mbaya wote wanaongea Kiswahili na wapo katika ukanda wetu).wana tabia zinazofanana, na sasa huyu wa kwetu.
Waangalie Adolf Hitler, Mussolini, Nicolae Ceauscecu, Ghaddafi na Bokassa wote hawa wanazo tabia zenye kufanana, wanaogopesha wananchi na walitaka kuabudiwa kama miungu wadogo, mitazamo na maneno yao yanafanana...wanasema tofauti na wanayoyafanya ingawa wanasisitiza kutetea wanyonge.
Leo nilikuwa naongea na rafiki yangu Mnyarwanda (Mtutsi), Alivyokuwa Rwanda mwaka 2014 nikimuuliza vipi Rwanda inaonekana Kagame anaendesha nchi vizuri huwa akinijibu siwezi kuongea kwenye simu (Bahati mbaya watanzania leo yanatukuta hayo hayo ya Rwanda uki-text" kuhusu rais Magufuli utapelekwa mahakamani ili ufungwe...mara chache sana mfumo utakubali utozwe faini), Kitu cha kushangaza hawa watesi wa demokrasia wanadhani raisi Magufuli hapaswi kushauriwa hata kama anakosea (Hapo ndiyo jina la uungu mdogo linapokuja) mwenyewe atakwambia hataki kufundishwa au kuelekezwa utadhani urais ni kazi ya familia!.....Ufalme unasahihishwa sembuse urais wa kuomba kura kwa unyenyekevu huku akiweka mikono nyuma kwa heshima!
Swali la kwanza nililomuuliza rafiki yangu Mnyarwanda leo ni " Kwanini rais Kagame kayafungia makanisa 700 na msikiti mmoja? Akasema Kagame huwa haaminiki! akaendelea kusema makanisa yaliyofungiwa siyo ya madhehebu makubwa kama ya Kikatoliki au waprotestanti akasema hawezi kufungia hayo makanisa kwa sababu yana nguvu na ushawishi mkubwa. Akasema Kagame ni mkatoliki (hilo nilikuwa nalijua) ila huwa haendi kanisani...sikufahamu hilo!
Swali la Pili, je ni kweli Kagame na Museveni hawaelewani? Akasema hapana.....Wanaelewana sana ndiyo maana kila analofanya mmoja wao mwingine anakuja kulifanya baadaye! Mfano kuongeza muda wa kutawala!
Swali la Tatu, Ilikuwaje Kagame alisema hataki kuendelea na uongozi, muda wake wa uongozi ukiisha na sasa bado anang'ang'ania kuendelea kuongoza? Akasema Kagame alinunua watu (Wapinzani) wa kumsemea ili kuongeza muda, ni mbunge mmoja au wawili wa upinzani walimkataa ndiyo maana alipata asilimia 99 na zaidi ya kura za ndiyo (Hilo naona kwetu tulishaanza....ila sijul lakini nadhani tunaelekea huko ndiyo maana tunasikia mambo ya kuongeza muda na term ya kutawala..I might be wrong!)
Je ni kweli madikteta wote huwa wanaigana kila wanalofanya? Bird of the same feather flock together!
Je kuna madikteta wazuri na wabaya? Jibu ni HAPANA Madikteta wote ni wabaya awe Vladimir Putin, Donald Trump,Pinochet n.k wote wana tabia zinazofanana ila kwenye nchi za wenzetu ambako demokrasia imeshika kasi huwa wanawekwa breki.....hawaendi mbali sana ku-"abuse" madaraka yao kama kwetu! Swala la kubadilisha katiba kwa ajili ya kumsaidia kumfitisha mtu mmoja huku anayesaidiwa anajua ni kinyume cha sheria na katiba ni udikteta na uvunjifu mkubwa wa sheria!
Tangu alivyoingia madarakani Magufuli wapo tuliohisi ataanza kulewa madaraka na kupitiliza ile "level" ya ustaarabu! Kulivyokuwa na ile "Hashtag" [HASHTAG]#What[/HASHTAG] would Magufuli do? kuna wasomaji wengi duniani walitabiri kuwa Magufuli ataanza tabia fulani tofauti na jinsi anavyokuwa "portrayed" Haukupita muda maoni ya wasomaji wengi yakaanza kujaza "comments" section ya magazeti kama Daily Nation" The standard" News24" the guardian la UK, Daily Mail" n.k kuwa mambo anayofanya huyo rais siyo ya kupendeza na inaonekana kama anatoa "decrees" mara nyingi akisema "Mimi nasema" Sitaki", "Sikuhonga hata shilingi nimechaguliwa bila kutumia hela" (Sidhani kama atakuwa amesahau kuwa mwenyekiti wa CCM aliingia na majina yake matano mfukoni...mengine yaliyoendelea wote tunayafahamu) na vitabia vingine vya kung'aka hadharani, kufukuza wafanyakazi kwenye mikutano ya hadhara! AMBAYO KIMSINGI NI UKIUKWAJI MKUBWA WA SHERIA!
Kwa wale wanaofahamu kwa kusoma historia ya Adolf Hitler ( fuhrer) ni rahisi kuelewa tabia za madikteta....Mara nyingi hawasemi wao wenyewe ila wanakuwa na henchmen wake ambao wanawasemea. Kagame ana watu wa kumsemea, Museveni anao wa kumsemea pia, Kabila anao wa kumsemea na yule mwingine anao watu maalum wa kumsemea.
Idi Amin alikuwa na Isaac Malyamungu, Bob Astles na wengine waliotoka kwenye kabila lake, hao waliamini na usingeweza kuwabadilisha kuwaambia kwamba General Amin alifanya au anafanya jambo haramu...ni kama walikula yamini na viapo kwa kiongozi wao....Hawatakuamini kwa lolote hasi utakalosema kuhusu kiongozi wao!
Tabia za madikteta zikoje?, Moja....Wanataka wawe VINARA kwenye kila jambo....hata kama ni dogo kiasi gani!
Mbili, Si wavumilivu wakisemwa (Ninamaanisha hawawezi kukubali "criticisms" hata iwe ndogo kiasi gani). Kwa kiongozi mwenye busara lazima ukubali kukosolewa kwa sababu kazi uliyoiomba na kuikubali inataka ukosolewe hata kama hujakosea (Ninamaanisha ukikosolewe hutakiwi ujibu kila kitu zaidi ya kujiangalia na kujisahihisha kama umekosea), Kama hakubaliani basi hafai kuwa kiongozi!
Kwetu tumeona Ben Saanane alipotea baada ya kuandika makala madogo akihoji Ph.D ya rais Magufuli! Azory Gwanda alipotea baada ya kuandika jambo la kweli kuhusu kupotea kwa baadhi ya wananchi wa Kibiti,Pwani.....Tumeona Tundu Lissu akipigwa risasi 38 (kumi na sita zikimpata mwilini) kwa kuongea kupinga yale anayoamini kuwa si sahihi yaliyofanywa na serikali hii (Magufuli alisema "Mtu anapinga kila kitu halafu anaachwa a-survive tu?") kwenye hali kama hiyo unaweza kusema mtuhumiwa namba moja ni nani? Idi Amini inasemekana alimuua Field Marshal Okello aliyepanga na kuhusika na Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964...Kwanini alimuua Field Marshal Okello (ingawa si kweli alikuwa na cheo cha Field Marshal) Idi Amini alisema Uganda ilitakiwa iwe na Field Marshal mmoja tu ambaye ni yeye! the easiest way of solving problem for dictators..KUFUNGA WAPINZANI WAKO..KUUA..KUPOTEZA N.K.
Madikteta huwa wana suluhisho la aina moja tu, hawana muda wa kuongea wala kujadiliana na wapinzani wao. Wakisema "mimi nimesema" sitaki" sibabaishwi" usinifundishe" hukuniweka hapo" (wamesahau kuwa sisi wananchi ndiyo tuliwapa kura) "They real mean it" (Wanamaanisha wanayoyasema hawatishii kweli).
Madikteta siyo wavumilivu wakisemwa (intolerant) ndiyo maana utasikia makanisa yanafungiwa, viongozi wa dini wanakamatwa na kusingiziwa mambo ambayo hawayakutenda, wanabambikizwa kodi, wengine wanaambiwa siyo raia n.k wakivuka viunzi vyote si ajabu kusikia kiongozi kapata ajali amekufa..........
Madikteta muda wote hawapatani na magazeti au media yanaowakosoa (positive or negative criticisms). Kufungia magazeti, Radio, Televisheni na mashirika ya haki za binadamu ni jambo la kawaida kwao....Mifano ni mingi.
Mwisho, Nimezoea kusema ukweli na sitaogopa kusema kwa sababu ni haki ya msingi kusema . Magufuli kama hapendi kukoselewa basi asingeomba kazi ya urais, ni bora angeanzisha kampuni yake akawa CEO. Kazi ya urais ni kazi ya umma hivyo sisi kama waajiri wake tunapaswa kumuuliza swali lolote lile, hao henchmen wake hawapaswi kuwaadhibu watanzania kwa kuwa na mawazo tofauti na yeye au wao...hatuwezi kufanana kwa ufikiri, kila mmoja wetu ni tofauti.
Kwa mawazo na ufikiri wangu napenda kusema kuwa MAGUFULI NI DIKTETA, simtukani ila lazima niseme ukweli, Kwa tabia alizonazo ame-fit kwenye category hiyo. Tabia zote za madikteta nilizozitaja anazo! Jambo nisilolijua ni kama anafahamu anachofanya si sahihi au anaamua kufanya kwa sababu ana nguvu na uwezo wa kufanya? Ameshabihiana na Kagame kwa asilimia 85 na Museveni asilimia 80.