Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 556
- 1,322
Wakuu kwema!
Kama tunavyofahamu hapa jukwaani kumekuwa na mijadala tofauti tofauti kuhusu udhamini wa GSM na vilabu zaidi ya 7 kwenye Ligi ya NBC. Ambapo kuna wadau wa soka wanasema hii si nzuri na inawabeba Yanga zaidi kwa kuzingatia GSM ni Yanga na ni Mwanachama wa klabu hiyo. Lakini Pia ni mfadhili wa klabu hiyo
Lakini kuna wale wanasema ni sahihi kwa GSM kujitolea kudhamini vilabu hivyo maana inaleta chachu ya ushindani kwa maana vilabu vinakuwa na mnyororo wa uchumi mzuri kuliko timu kukosa udhamini kabisa ambapo kuna weza kupelekea kushawishiwa na timu yenye uwezo wa kifedha na ukatokea mpango wa upangaji wa matokeo.
Sasa kipi ni sahihi kwenye mitazamo ya makundi haya mawili?
Mjadala ujikite kwenye maswali haya
1. Kanuni zinasemaji Kampuni au taasisi kudhamini timu zanashiriki ligi moja?
2. Je udhamini wa GSM ni kweli unaharibu ligi ya NBC na kuibeba Yanga zaidi?
3. Je kuna viashiria vyovyote vya upangaji wa matokeo TFF na Bodi ya Ligi wameubaini na hatua zipi wamezichukua?
4. GSM ajitoe kwenye udhamini wa vilabu vingine na abaki na Yanga pekee?
5. Nini kifanyike sasa ili wadhamini wapatikane wengi ili kampuni au taasisi moja isipate nafasi ya kudhamini klabu zaidi ya moja kama ilivyo sasa?
Timu zinazodhamini na GSM wao wanasemaji pia kwenye hili
Pamba FC, Yanga SC, Coastal Union, Mashujaa, Dodoma Jiji na Namungo