Udhalilishaji kingono kwa wanawake ni tatizo kubwa sehemu za kazi

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,606
8,406
Mabosi wa kiume wamekuwa wakiwadhalilisha sana wanawake sehemu za kazi ila wanawake wengi hawana ujasiri wa kusema wazi.

1. Maofisini.
2. Vyuoni.

Viongozi wengi sio waadilifu, wengi ni wasaliti wa ndoa zao, wengi ni wazinzi.

Kama kiongozi anakuwa mzinzi/ anasaliti ndoa yake, hivi kweli kiongozi huyo anaweza kutenda haki kwa anao waongoza?!!

Ngono maofisini baina ya viongozi na walio chini yao umeshamiri....
Tatizo hili lazima likomeshwe.

Endapo leo uchunguzi ukifanyika kwa viongozi maofisini basi karibu asilia 99 wanasaliti ndoa zao kwa kuwa na mahusiano ya kingono na wafanyakazi.

lakini wahanga wakuu wa rushwa ya ngono vyuoni na maofisini ni wanawake.

Wanawake wengi wanatumiwa kingono na mabosi wao au na walimu wao ili kujihakikishia ufaulu au usalama mahali pa kazi.
asilimia kubwa wanawake wengi wanarubuniwa na mabosi wao au viongozi wao, na hivyo wanawake wengi na hata walio Olewa hujikuta bila kupenda wanaingia kwenye ngono na mabosi wao.
Hili ni tatizo kubwa maofisini na vyuoni.

Leongo ni kutaka kuwakomboa wanawake kutoka kwenye udhalilishaji wa kingono vyuoni, makazini na hata kwenye siasai. tunataka kuona wanawake wanashika nafasi mbalimbali kwa sifa na uwezo wao na sio favor ya rushwa ya ngono kwa mabosi wao.

Rushwa ya ngono ni hatari sana.

Tunaziomba mamlaka zinazoteua zichunguze sana kipengele hiki cha uzinzi/usaliti.
 
Hawa mabinti wangekua wanavaa magauni marefu na raba hayo mambo yasingewatokea kamwe.
1718187729053.jpg
 
Hawa mabinti wangekua wanavaa magauni marefu na raba hayo mambo yasingewatokea kamwe.View attachment 3015390
Nenda Zanzibar mwanamke kutwa kavaa buibui kuuubwa kajifunika mwili mzima mpaka hata macho hayaonekani na jinsi wengi walivyo vimodo unaweza hisi nguo imetundikwa juu ya mti unakuja kusikia kabakwa binadamu ni kiumbe complex sana .
 
Nenda Zanzibar mwanamke kutwa kavaa buibui kuuubwa kajifunika mwili mzima mpaka hata macho hayaonekani na jinsi wengi walivyo vimodo unaweza hisi nguo imetundikwa juu ya mti unakuja kusikia kabakwa binadamu ni kiumbe complex sana .
Hili linaweza kuwa kweli 🤔 ila kwanzibar ninayoijua vitendo vya hivyo na vya kihalifu huwa ni vichache mno.
 
Ni changamoto sana
Ni changamoto kubwa sana.

Kama kuna vita ya kuwakomboa wanawake basi hii ya udhalilishaji kingono ni kubwa sana.
asilimia kubwa ya wanawake waliopo maofisini wanamahusiano ya kingono na wakubwa zao kwalengo la kupata upendeleo yaani favor.


Lakini wanawake wenyewe waache kujirahisisha miili yao, wawe na msimamo.
 
Back
Top Bottom