Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,124
- 2,194
Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka UDART inapenda kutoa ufafanuzi juu ya tukio lililochapishwa katika mitandao ya kijamii ya Global na Manara Tv, taarifa ilichapishwa ikionyesha baadhi ya abiria katika kituo cha Kimara Mwisho wakizuia moja ya Basi la Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka.
Leo asubuhi majira ya kuanzia Saa 2 ndani ya mfumo wa barabara za Mabasi yaendayo haraka tulipokea taarifa ya lori la mizigo kukosea njia na kuingia sehemu ya Barabara eneo la katikati ya Kituo cha Kibo na Ubungo Maji kwa muda wa zaidi ya dakika 20 na kusababisha changamoto kwa mabasi yaendayo haraka kutopita inavyopaswa na kuweka msongamano katika mzunguko wa Mabasi, hali hiyo ilisababisha kuvurugika kwa mzunguko wa mabasi na kusababisha kuchelewa kwa Mabasi kufika katika vituo kwa wakati.
Changamoto iliyosababishwa na lori hilo ilisababisha kuchelewa kwa Mabasi kuwasili katika kituo cha Kimara na kusababisha baadhi ya abiria kushuka kutoka katika sehemu ya kupakia abiria na kuzuia Basi lililopaswa kuanza kupakia abiria katika vituo vya mbele wakati pia Basi zilizosalía zikijiandaa kuanza kupakia katika kituo cha Kimara.
Uongozi wa Kampuni ya Mabasi yaendayo haraka (UDART) unaomba radhi na unatoa pole kwa abiria kutokana na changamoto iliyojitokeza wakati huo wa asubuhi na kusababisha kuchelewa kwa Mabasi kuwasili katika vituo.