Complicater
Member
- Jul 28, 2022
- 16
- 31
MRADI MDOGO WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI WENYE TIJA
YANAYO HITAJIKA
1. Kuku(tetea) kumi (10) na Jogoo mmoja (1)
2. Banda lenye ubora
3. Vyombo kwaajili ya chakula na maji
4. Chakula bora na kilicho na virutubisho kwa kuku
5. dawa na chanjo kwajili ya magonjwa
6. Chanzo nishati joto na mwanga ktk banda
7. Elimu na ujuzi wa namna ya kuwalea
8. Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
9. Mayai ya kuku, mayai mabovu ambayo hayakutotolewa/ kuanguliwa au ya kisasa
10. Daftari au kitabu cha kutunzia nukuu na kumbukumbu
KUKU (TETEA) KUMI (10)
Wakati wa kuanza mradi wako wa ufugaji hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa/usiopishana na hawajawai kutaga/kuanza kutaga. Chagua kuku kutoka katika familia bora kutegemea matazamio ya mradi wako. Kwafano kama lengo lako ni kufuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo itakua haraka na yenye uzito mkubwa,Au ikiwa lengo ni mayai basi chagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi/kwa wingi itasaidia kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kukuongezea faida, kwa mfugaji itapenkeza kamaata nunua kuku wadogo ambao wameachishwa kulelewa kutoka kwa mama zao. Kuku hawa unaweza ukawapata kwa bei ya chini, pia watafaa sana
JOGOO MMOJA (1)
Jogoo mmoja (tu) anatosha kuwahudumia kuku-tetea wote kumi.
Zingatia chaguzi bora ya jogoo lililochangamka, rangi nzuri, upanga/manyoya ya mkiani yaliyo simama, macho angavu, uzito wa kutosha, uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vizuri mfugaji akafahamukwamba kuku wote watakao (anguliwa)zalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutagaji kuku na upatikanaji wa mayai pia utategemea wa jogoo aliyechaguliwa.
BANDA BORA
Miongoni mwa vitu muhimu na vya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji, ni pamoja na uwepo wa banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasikumbwe na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa angalau mita 10 kwa mita 4. Yaani, urefu uwe mita 10 na upana mita 4. Kisha gawa vyumba vya mita 4 na urefu mita 2 kutoka katika banda lako hivyo vitapatikana jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa sawasawa.
Ujenzi uzingatie upatikanaji wa malighafi na vifaa kwa urahisi katika mazingira husika.
Kwa mfano,
1. Katika maeneo ambayo fito zinapatikana kwa urahisi, banda linaweza kujengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo.
2. Ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. Kumbuka, vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
Sakafu: Mbao, udongo, saruji, mianzi au fito
Kuta: Mbao, mabanzi, nguzo, mianzi, Fito,udongo,matofali,mawe, bati na wavu.
Paa: mabati, makuti, majani ya migomba, Nyasi na vigae.
Wigo: Mbao, fito, mabanzi, Matofali, mianzi, matete wavu
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
1. Imara na lililo na uwezo wa kuwahifadhi katika hali nzuri, pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, baridi na mvua, pamoja na wanyama wanao weza kuwadhulu.
Lililo hewa safi na nafasi inayotosha na inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Lijengwe sehemu iliyoinuka, isiyotuama maji, pia isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba inayoishi watu.
Liwe na sehemu kuweka chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
Liwe na nafasi ya kutosha sambamba na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
Sehemu yenye mazingira ya joto banda linatakiwa liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu, unaofikia paa.
Sehemu yenye mazingira ya baridi banda inatakiwa liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.
JINSI AU NAMNA YA KUFANYA.
Watunze kuku wako mpaka watakapofikia muda wa kutaga.
Wakianza kutetea ni dalili ya kuonesha wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia, viota vinapaswa viwe na ukubwa unaoendana na kuku ili kumuwezesha kuatamia mayai yote vizuri wakati ukifika, viota viwe vinavyozuia mayai kusambaa, viwe mahali safi na pakavu.
Kumbuka: Hakikisha kila kuku anataga katika kiota chake. Kuku anapotaga mayai matatu unakumbushwa kuchukua mayai mawili na kuwaachia yai moja moja ili kufanya waendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumtayarisha kazi ya kuatamia.
kufanya hivyo, kuku atataga mayai mengi zaidi na ikitokea akataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri tafuta mengine uongezee kufikisha mayai 20 kwa kila kuku.
Zingatia: mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yatunzwe sehemu salama, pakavu, pasafi na penye joto la wastani.
Kuku wote wanatakiwa kuanza kuatamia kwa siku moja. Ili kuwezesha hili unapaswa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kutamia muwekee mayai mabovu au ya kuku wa kisasa. Fanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuatamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku wa kisasa humfanya kuku aendelee kuatamia akidhani ni mayai yake.
Baada ya kuona kuwa kuku wako wote wapo tayari kuatamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuatamia (kimoja katika lile banda letu). Katika vile viota weka mayai 20 kwa kila kiota, kama hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi uliyopanga.
Waamishe kuku kutoka wanapotagia au kuatamia na kuwa peleka katika chumba kilichoandaliwa kwajili ya kuatamia. Zoezi la kuwahamisha kuku inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Muweke kuku katika kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie vizuri kwa chakula na maji ya kutosha.
Nyakati za usiku waongezee joto la ziada kwa kuwa wekea jiko au ndoo ya chuma yenye moto wa chengachenga za mkaa au kama una umeme tumia taa za joto.
Baada kama ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua/ kutotoa vifaranga.
wakati huu ndio ukaribu na kuku wako unahitajika sana kuliko wakati wote.
Tenganisha vifaranga kutoka kwa mama zao mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba maalumu mbali na kuku wakubwa. Kama chumba cha kuatamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawekwe chumba cha mwisho (hii ni kutokana na hitaji lako)
Ukishatenganisha vifaranga mbali na mama zao(matetea wako), wawekee mayai mengine tena 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua (nunua kabla hawaja tutoa hawa tetea walia atamia) kwa wafugaji wenzako. Hakikisha hayo mayai yametagwa na kuku walio katika hali nzuri, hawana magonjwa na ukubwa na uzito unaofaa. Mayai yote yakaguliwe kwa uangalifu ili kujua kwamba yameharibika au la!. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba kipo safi na viota vimesafishwa vizuri, havina wadudu. Kuku wako pasipo kujua wataanza kuatamia upya mayai uliyowawekea.
Ukishawawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyoelezea hapo awali. Baada ya siku 21 hadi 25 utapata vifaranga wengine tena.
Fuata hatua zote kama nilivyoelezea hapo awali. Lakini kwa awamu hii waache matetea wako, wala usiwapatie mayai mengine tena.
JINSI NA NAMNA YA KULEA VIFARANGA
Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuatamia, andaa chumba kwa ajili ya kulelea vifaranga.
Safisha chumba kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.
Weka chombo cha kutoa joto au taa ya kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla ya kuanza kuingiza vifaranga wako katika chumba. Weka chakula na maji ya kutosha kwenye vyombo vilivyo na umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, mapepe(pumba za mpunga), marando ya mbao n.k katika sakafu ya chumba hicho.
Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi katika sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao wanaweza ili uweze kufanikiwa katka hili, banda lako liwe la duara.
Weka Joto la kutosha, litakalo wafanya vifaranga watawanyike chini au pembeni ya chanzo cha joto, kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujikusanya chini ya chanzo cha joto.
Baada ya siku ya 3 wapatie chanjo ya Gumboro na siku ya 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa hiyo chanjo baada ya mwezi mmoja, baada ya hapo utafanya hivyo kila baada ya miezi mitatu-mitatu.
MAKADILIO MAPATO YA MRADI
Kwa utotoreshaji kwanza utapata vifaranga 150 kwa makadilio ya vifaranga 15 kwa kila kuku.
Hapo, haujazingatia kanuni za ufugaji za hii makala, au ukapata vifaranga 100 yaani wastani wa vifaranga 10 kwa kuku mmoja. Baadaye wakakua 50 kati ya 100 wakafa yaani watano kwa kila kuku mmoja, hapo utakuwa na jumla ya kuku 50 walio baki.
Baada ya wiki 3 (uzao wa pili) utapata tena kuku tufanye hesabu kama hiyo hapo juu kwa hasara utakuwa tena na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa uliwapumzisha kuku wako baada ya uzao wa pili kwa miezi miwili, mwezi wa 3 utapata unaweza pata tena vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata vifaranga wengine 100. Kwa hesabu kama hile ya awali, wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa baada ya miezi 6 utakuwa na uhakika kuku wakubwa wale wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.
Kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Kama kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwisho utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku 900 wanaweza kupatikana kutoka katika uzao wa kwanza, wapili na watatu.
KWAHIYO: mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.
Ukiuza kuku wote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujengea miundombinu bora kwasababu utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana, utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa waweza ongeza kuku wako wa kutaga hadi kuku 4,000 kwa maana utakuwa na pesa za kutosha kuendeshea mradi wako wa ufugaji.
Kwahiyo, ukiwa na kuku 4,000 wa kienyeji na wakataga mayai, kama kuku 3,000 tu wakataga ukauza yai moja kwa bei ya TZS 250 tu, unawezapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo makadilio sawa na TZS 22,500,000/= kwa kila mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa na 128,572 USD.
Kumbuka kwamba makadilio haya yote ni ya chini. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukiendelea kumtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.
MUHIMU
Hakikisha unatunza kumbukumbu zako zote za fedha na shaghuli zote zamradi katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi. Pia hali na maendeleo ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo, mwisho, siku walipoanza kuatamia, magonjwa yanayo/ yaliyo wasumbua mara kwa mara.