ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Uchumi kilema wa nchi unaongeza maumivu kwa vijana na wafanyakazi wa nchi yetu;
_Uchambuzi wa mwenendo wa ukosefu wa ajira na maslahi ya Wafanyakazi Nchini kuelekea siku ya Mei Mosi 2022.
Utangulizi;
Tukiwa tunaelekea katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, ambayo kila mwaka inaadhimishwa siku ya tarehe 1 Mei (“Mei Mosi”), Sisi ACT Wazalendo katika kutimiza wajibu wetu wa kuongoza umma kwa kuhakikisha Tanzania na rasilimali zake zinawanufaisha watanzania wote.
Kupitia sekta ya vijana, kazi na ajira ya chama tumeona tuungane na vijana na wafanyakazi wote nchini kwa kufanya uchambuzi wa hali halisi ya vijana hususani mwenendo wa ajira na hali za vipato, pamoja na haki_ustawi wa wafanyakazi wote nchini. Katika kuangazia hali za wafanyakazi na mwenendo wa ajira nchini, tumefanya uchambuzi wa kina juu ya mpango wa maendeleo ya taifa, bajeti za wizara na taarifa za utafiti za hali ya maisha, viwango vya ukosefu wa ajira na uwezo halisi wa nguvu kazi nchini.
Kwa kufanya hivyo, uchambuzi wetu utazungumzia maeneo makuu matatu;
Mosi, ukosefu wa ajira na ufinyu wa mazingira ya kujiajiri;
Pili, maslahi na haki za wafanyakazi nchini;
Tatu, mtazamo na mapendekezo ya ACT Wazalendo kuhusu changamoto ya ajira na ujira na maslahi ya wafanyakazi nchini.
A: Ukosefu wa Ajira na Ufinyu wa Mazingira ya Kujiajiri
i. Hali halisi ya Mwenendo wa Ukosefu wa Ajira Nchini.
Mwenendo na hali ya ukosefu wa ajira nchini inazidi kuwa gumzo na kuzua mtanziko nchi kwetu. Kila mwaka nguvu kazi inayoingia katika soko la ajira ni takribani watu laki nane (800,000). Ajira zinazozalishwa kwenye sekta mbalimbali huwa ni wastani wa 137,000 kila mwaka huku ikiacha watu hususani vijana zaidi ya 653,000 nje ya mfumo wa uzalishaji na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali ya utegemezi.
Takwimu za mwaka Juni, 2021 zinaonyesha kuwa idadi ya ajira katika sekta rasmi za umma na serikali inazidi kupungua pamoja na idadi ya ajira mpya katika sekta binafsi imepungua kwa takribani theluthi ya idadi kati ya 2015 na 2020, hii ni kutokana na serikali kutoa ajira chache sana na kupungua kwa uwekezaji kwa sekta binafsi.
Ingawa kiwango rasmi kinachotajwa na serikali cha ukosefu wa ajira ni asilimia 9.5 takwimu hizi bado hazitoi picha pana na kamilifu ya uhalisia wa hali ya ukosefu wa ajira na fursa ya kupata kipato miongoni mwa vijana. Kwasababu, vipimo vya kitakwimu kwa vigezo vya kiuchumi vinaacha vijana wengi walio vyuoni, mashuleni, walio kwenye ajira za vijungu jiko. Lakini pia zinachanganywa ajira rasmi na zisizo rasmi kwenye kapu moja.
Ongezeko la ajira rasmi za malipo ni dogo sana kwa miaka mitano, ni dalili kuwa uchumi wetu kama nchi haukuweza kuzalisha kazi zenye hadhi ya kulipwa. Kwa mujibu wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya (ILFS) kutoka ofisi ya taifa ya takwimu (NBS,2021) zinaonyesha ajira za malipo zimeongezeka kwa asilimia 0.2 kutoka asilimia 14.1 mwaka 2014 hadi asilimia 14.3 mwaka 2020.
Kwa maneno mengine, idadi ya nguvu kazi ya watu zaidi ya 22,152,320 watu wanaofanya kazi za malipo ni 3,167,782 pekee huku kati yao watu 18,984,538 hawana ajira rasmi, miongoni mwao vijana wenye umri wa miaka kuanzia 15 hadi 35 ni zaidi ya asilimia 13.4. Huku viwango vya watu ambao hawana kabisa ajira ni asilimia 9.5 kwa mujibu wa taarifa sawa na watu takribani 2,406,950.
Pia, tumeshuhudia ongezeko kubwa la ajira zisizokuwa rasmi kutoka asilimia 22.0 mwaka 2014 hadi asilimia 29.4 kwa mwaka 2020 (kwa mujibu wa taarifa za NBS,2021). Hii ina maana nchi imezalisha ajira zisizo na usalama mkubwa, staha na kipato cha uhakika kwa kiwango hiko.
Kwa miaka zaidi ya saba sasa tangu 2015 tumezidi kushuhudia wimbi kubwa la vijana wanaohitimu sekondari, vyuo vya ufundi, vyuo na vyuo vikuu kukosa ajira kwani ni asilimia ndogo sana ndio wanaopata ajira katika sekta rasmi.
ii. Jeshi la Wasio na Ajira, Linatumika Kunyonya Jasho la Wanyonge.
Kuwepo kwa watu wasio na ajira, ambao walio tayari kufanya kazi na wanaotafuta kazi kwenye sekta rasmi, kumetengeneza akiba kubwa ya nguvu kazi isiyotumika (labour reserve). Hali inayopepelekea kuwa na idadi ya watu wanaojitolea kwa ujira mdogo au bila ujira kabisa bado ni kubwa na inaendelea kushamiri nchini kutokana na mazingira magumu ya kujiajira na kupata ajira.
Athari za janga hili ni kubwa sana katika jamii yetu kwa sasa, pamoja na; kuongezeka kwa wimbi la umasikini na utegemezi katika ngazi zote, (familia, jamii na hata Taifa), kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na uhalifu nchini ikiwemo vitendo vya wizi, ukahaba, unyang’anyi, uporaji. Kuongezeka kwa upendeleo, kujuana, rushwa katika utolewaji wa kazi, kuongezeka kwa utumikishaji wa watoto kwa ujira mdogo au bila malipo hususani; Mashuleni, viwandani, majumbani, migodini nk kwa kigezo cha kupatiwa Ajira, Kwahiyo, nguvu kazi kubwa iliyotupwa nje ya mfumo wa uzalishaji inatumika kuwanufaisha watu wachache kwa kuzalisha faida zaidi huku wakiwafukarisha na kuwadunisha mamilioni ya watanzania.
iii. Hoja za Ukosefu wa Ajira na Uchumi Wetu
Kwanza, tunatambua kuwa nchi nyingi duniani zinakumbwa na kadhia hii ya ukosefu wa ajira, kutokana na mabadiliko ya sera za uchumi (mfumo wa uzalishaji wa dunia). Lakini namna ambayo kila nchi inavyolishughulikia tatizo hili ndipo utofauti na upekee huonekana.
Katika historia ya hali ya ukosefu wa jira tumeweza kushuhudia mapinduzi ya serikali kadhaa ikiwemo nchini Misri 2011, tumeona baadhi ya mabadiliko ya sera katika kushughulikia suala hili matahalani nchi kadhaa zimekuwa zikitekeleza sera ya kutoa ruzuku za ukosefu wa ajira kama vile Marekani, Ujerumai, Uingereza, nchi za Skandinavia kutaja kwa uchache. Kuwatafutia ajira kwenye nchi za pembezoni kwa staili tofauti tofauti (kuuza utaalamu, uwekezaji).
Nchini kwetu, tunashuhudia kuwa mashambulizi dhidi ya vijana wanaokosa ajira ni makubwa kutoka kwa watawala (wa kiuchumi na kisiasa), zipo hoja lemevu zinazojengwa katika kutafakari hali ya ukosefu wa ajira nchini. Wapo wanaowashambulia vijana kwa kuwa ambia hawajitumi, hawana ubunifu na uthubutu au kutojitolea. Wapo wanaoenda mbali zaidi kwa kusema ubovu wa mitaala ya elimu au wahitimu kukosa ujuzi unaohitajika na soko. Lakini hakuna anayejiuliza ajira zinazozalishwa zipo wapi? Kwanini uchumi wetu hauzalishi ajira za kutosha, vipato vinavyotokana na ajira zinazozalishwa zinawasaidaaje wafanyakazi, usalama na mazingira yake yapoje? Kwa ufupi, hakuna anayejitahidi kudadisi kiini cha tatizo la ukosefu wa ajira nchini kwetu.
Tafiti zinaonyesha mchango wa sekta kuu za uchumi kwenye ajira kilimo kinachangia asilimia 61 (asilimia 58.4 mashamba ya familia na kaya, asilimia 2.7 ajira za malipo) ya ajira zote. Viwanda inachangia asilimia 8 na sekta ya huduma inachingia asilimia 31. Tunashuhudia kusinyaa kwa ajira zinazozalishwa na serikali kuu na mashirika ya umma ambayo yanachingia kwa asilimia asilimia 2.6 na 0.3 mtawalia.
Mfumo wa uchumi wetu umejengeka kwenye hali ya utegemezi, ambao tumeurithi tangu enzi za ukoloni. Uchumi tegemezi hauzalishi ajira badala yake usafirisha ajira kwenda nje ya nchi. Tunaona mchango wa sekta ya kilimo Lakini kilimo hakijafungamanishwa na viwanda ambayo inatoa ajira ndogo sana. Kilimo chetu ni cha kuuza nje malighafi na kutegemea mahitaji mengine kutoka nje.
iv. Ajira, Uwekezaji na Mazingira ya Kujiajiri
Tumeona mchango wa sekta ya kilimo (Mazao, uvuvi, ufugaji, wanyamapori na misitu) kwenye ajira lakini bado kilimo chetu hakijawekewa mkazo na serikali, hivyo kukifanya kilimo kuwa mzigo kwa nguvu ya vijana na watu wengine. Sifa kuu za kilimo chetu kwa miaka mingi ambazo zinahitaji kufanyiwa mapinduzi ni kama zifuatazo;
• Kilimo chetu kimetawaliwa na utumiaji wa nyenzo duni
• Kuzalisha bidhaa za kilimo kwa ajili ya soko la nje
• Kiwango cha utegemezi kwenye soko la nje ni kukubwa zaidi
• Kukosekana kwa uhakika wa bei za mazao
• Kutokuwepo kwa ruzuku za uzalishaji
Pili, Mazingira kandamizi kwa wafanyabiashara na watoa huduma wadogo.
Miezi ya hivi karibu tumeona fukuza fukuza ya wamachinga na kubomolewa kwa vibanda vyao, kwa mujibu wa takwimu zilizopo mchango wa sekta ya biashara na matengenezo ni wastani wa asilimia 14 ya ajira zinazozalishwa. Pia takwimu za wizara ya TAMISEMI 2021 inaonyesha kuna takribani wamachinga 2,335,711 na zaidi. Lakini tunaelewa mazingira ya biashara ya kundi hili kubwa yalivyo nchini kwa sasa kila uchao wanaporwa mitaji yao na migambo au kuchomwa moto kwa vibanda vyao.
Tatu, kuna changamoto za mitaji kwa vijana. Changamoto kubwa iliyopo ni kwa Halmashauri nyingi nchini kutokutoa kabisa fedha na zingine zikitoa hazifiki asilimia hiyo 10% kwa kisingizio kwamba makusanyo ni madogo. Mfano, kupitia taarifa ya CAG ya 2018/19 Mamlaka 115 za Serikali za mtaa hazikutenga fedha hizi, pia taarifa ya 2019/2020 ya CAG iliweka wazi kwamba Mamlaka 82 za Serikali za mtaa hazikutenga 10% ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu. Lakini kuwepo kwa upendeleo wa utoaji wa mikopo na kukosekana kwa uwazi wa utolewaji wa mikopo hiyo.
Nne, serikali haitoi kipaumbele kushughulikia janga la ajira.
Tunashuhudia mahitaji makubwa ya wafanyakazi na watumishi tena kwenye sekta nyeti kama vile elimu, afya na kilimo. Lakini serikali haijaweka mkazo kabisa kwenye kuhakikisha sekta hizo zinapata wataalamu na watumishi, licha ya kuwepo kwa wataalamu waliosomeshwa kwa gharama kubwa, serikali ina waacha mtaani. Sekta za umma zinazidi kudorora kwa kutopewa mafungu ya kutosha, huku sekta binafsi nazo huzalisha ajira za vijungujiko.
Hivyobasi, tathmini yetu ni kuwa kuna uwekezaji mdogo sana kwenye kuzalisha ajira, kilimo kinapuuzwa na mazingira ya kujiajiri kwa bodaboda, mamantilie, machinga na wafanyabiashara wengine bado sio rafiki.
B: Maslahi na Haki za Wafanyakazi nchini.
i. Madai ya Wafanyakazi na Aatumishi wa Umma Kuongezeka Kila Mwaka.
Kwa takribani miaka saba mfululizo maslahi ya wafanyakazi wa Tanzania yamekuwa yakipuuzwa. Suala la nyongeza ya mishahara zimeonekana kuwa suala la hisani hususani kwa siku ya Mei Mosi. Malimbikizo na madai ya wafanyakazi yanazidi kuongezeka. Kwa mujibuwa ripoti ya CAG ya 2020/21 inaonyesha kuongezeka kwa madai haya kutoka Sh. bilioni 334.15 kwa mwaka wa fedha 2019/20 hadi Sh. bilioni 429.80 kwa mwaka huu wa ukaguzi.
CAG anasema kuwa “Madai hayo yanaongezeka kutokana na ufinyu wa fedha zilizotengwa na Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina) kwa ajili ya kulipa madai yanayotokana na upandaji wa vyeo tarajiwa, ajira za kwanza, na stahiki za Watumishi kama posho za kukaimu, posho za safari, na posho zingine zinazohusiana na ajira”.
Mpaka sasa Serikali imelipa malimbikizo ya mshahara kwa watumishi 65,391 yenye thamani ya Tsh. 90,698,408,006.34 pekee ukilinganisha na madaia ya Bilioni 429 wanayoidai Serikali. Mwenendo wa madai na malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi kuongezeka kila mwaka tafsiri yake serikali hailipi madeni haya kwa kasi inayoendana na mahitaji.
ii. Michango ya wafanyakazi kutowasilishwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF na PSSSF)
Wafanyakazi wanakatwa katika mishahara yao ili kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, Lakini kwa sehemu kubwa taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi kutowasilisha kabisa michago yao kwenye hiyo mifuko. Huu ni unyonyaji kabisa wanaofanyiwa wafanyakazi hawa, hili ni takwa la kisheria sio hisani ya mwajiri Lakini serikali inashindwa kuwasimamia wafanyakazi wafaidike na jasho lao.
iii. Upungufu wa Wafanyakazi Katika Sekta za Umma.
Ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma katika sekta ya umma hususani kwenye sekta ya elimu, afya na kilimo umeathirika kutokana na Watumishi waliopo kuzidiwa na majukumu. Kwa mujibu wa ripoti ya CAG, mwenendo wa uchambuzi wa upungufu wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa miaka 6 unaonesha kuongezeka kwa asilimia ya upungufu kutoka asilimia 22 mwaka 2014/2015 hadi asilimia 41 mwaka 2020/2021 licha ya mapendekezo ya kila mwaka ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa OR-TAMISEMI na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) ya kupunguza asilimia ya upungufu wa watumishi
iv. Mkato ya PAYE na Marejesho ya Mkopo wa elimu ya Juu (HESLB)
Kwa Kipindi kirefu wanyakazi nchini wamekuwa wakililia na kuomba kuongezewa mishahara, Kupandishwa madaraja/ vyeo, kuondolewa au kupunguzwa kwa makato ya PAYE, Kuondolewa kwa tozo ya mkopo wa Elimu ya juu ijulikanayo kama Value Retantio Fees (VRF), kurejeshwa kwa fao la matibabu kwa wafanyakazi wa sekta binafsi, kuboreshewa mazingira ya kazi nk lakini mpka sasa hakuna dalili za wazi za kutatuliwa kwa madai au kero hizo kwa wafanyakazi nchini.
v. Uhuru wa Wafanyakazi Nchini.
Katika historia ya nchi yetu mara kadhaa tumeona, dola linavyoweza kuingilia uhuru wa vyama vya wafanyakazi na kuvinyamazisha katika kutetea haki za wafanyakazi. Hali hii imejirudia tena kwa takribani mika saba (7) serikali ikitumia hila tofauti tofauti kuwanyamazisha wafanyakazi nchini zaidi ya kujipendekeza na kutii matakwa ya Viongozi wa kisiasa walio madarakani kuliko kutetea maslahi na matakwa ya Wafanyakazi. Ukiangalia Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), Chama cha Walimu Nchini (CWT), na Asasi zingine za kutetea na kupigania masilahi ya Wafanyakazi vimekosa nguvu na meno kabisa ya kuwatetea na kuwasemea wafanyakazi kama ilivyowajibu wao.
C: Mapendekezo ya ACT Wazalendo Juu ya Ajira na Kuboreshwa kwa Maslahi ya Wafanyakazi Nchini.
i. Tunamtaka Waziri Mkuu kutangaza rasmi swala la ukosefu wa ajira nchini kama janga la Taifa linalopaswa kupewa kipaumbele na kushughulikiwa kwa dharura kama yalivyo majanga mengine makubwa yaliyowahi kulikumba taifa kama; Uviko-19, matetemeko, ukame, mafuriko, njaa. Na iundwe kamati maalum ya wataalamu kuja na mapendekezo ya kukabiliana na ukosefu wa ajira.
ii. Kuongeza kiwango cha ajira kwenye sekta za umma hususani kwa sekta za elimu, afya na kilimo kutoka hali ya sasa ya wastani wa ajira elfu thelathini hadi kufikia laki moja na elfu sabini (170,000) kila mwaka.
iii. kubadili mfumo na muundo wa uzalishaji wa uchumi tegemezi na kujenga uchumi shirikishi unaozalisha kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza bidhaa nje.
iv. Tunaitaka Serikali kuweka utaratibu mzuri wa utolewaji na usimamizi wa mikopo/ fedha zinazopelekwa Halimashauri kwa ajili ya Vijana na makundi maalumu. Hili liende sambamba na kuwekwa wazi kwa fedha hizo kwa walengwa wote.
v. Tunaitaka Serikali kuboresha na kuongeza vyuo vya ufundi stadi nchini (VETA) ili kukuza ujuzi na utaalamu kwa Vijana hali itakayopelekea kupunguza changamoto ya ajaira nchini kwa kutegemea Serikali pekee.
Mapendekezo Kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi
i. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali iwalipe watumishi wote malimbikizo ya madai yao mara moja kwa mkupuo ili kuwawezesha kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimeendelea kupanda miaka hii ya karibuni, pia kulipa mafao ya watumishi wa umma kwa wakati.
ii. Tunaitaka serikali kufuata sheria kwa kupandisha madaraja na mishahara kwa mujibu wa sheria kila mwaka.
iii. Tunaitaka Serikali kuwarejeshea fao la matibabu wafanyakazi wote wa Sekta binafsi. Kwani fao hili ni kivutio kwa wafanyakazi wengi wa Sekta binafsi kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya jamii NSSF.
iv. Serikali ipunguze kodi ya PAYE kwenda kwenye herufi moja (single digit) wastani wa 6 hadi 8.
v. Kupitia upya kwa viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma na sekta binafsi. Viwango vilivyopo sasa haviendani na uhalisia wa gharama ya maisha.
vi. Tunaitaka Serikali kuweka utaratibu maalumu kisheria, hususani katika malipo kwa Wahitimu wanaojitolea katika Taasisi na Ofisi mbalimbali za Umma na Binafsi nchini.
Siku ya wafanyakazi duniani imekuwa ni chachu ya kufanya tafakuri ya namna wafanyakazi katika maeneo mbalimbali wananufaika na jasho lao na kuondoa vikwazo, udhalilishaji na dhulma dhidi yao. Lakini kwa sasa siku hii inapaswa itazame kwa upana zaidi hadi watu wasiokuwa na ajiara kwa sababu upo uhusiano wa karibu na maslahi ya wafanyakazi katika jamii zetiu. Ndio maana uchambuzi wetu tumewaweka kwenye kapu moja.
Imetolewa na;
Mwl. Philbert S Macheyeki
Msemaji wa Sekta ya Vijana, Kazi na Ajira
ACT - Wazalendo
30 April 2022