N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,405
- 10,878
Unaweza kusema headline iwe "Ni Uchina Tena"
Kamera za Ufukunyuzi Zenye Nguvu Zaidi Duniani zimetengenezwa na Wanasayansi wa China nchi hiyo ikiweka Viwango Vipya vya Upelelezi na Ufuatiliaji wa Kimataifa visivyomithirika.
Kamera hizi mpya zina uwezo wa kushinda viwango vya kimataifa vya kamera za ufuatiliaji na zinaweza kuchukua picha za hali ya juu kwa umbali wa kilomita nyingi hata katika hali ya hewa mbaya kutokea anga za juu yaani space.
Kamera hizi kwa mujibu wa Yahoo News hutumia teknolojia ya kisasa inayojulikana kama "single-photon detection" ambayo inaruhusu kuchukua picha za hali ya juu hata katika mazingira yenye mwanga mdogo. Hii inafanya kamera hizi kuwa bora zaidi kuliko zile zilizotumika hapo awali kutokea kwenye Satellite za Mawasiliano na za kipelelezi za hapo kabla.
Kwa sababu ya uwezo wake mkubwa kamera hizi zinaweza kutumika kwa ajili ya ufuatiliaji wa kijeshi, usalama wa mipaka na hata katika utafiti wa kiikolojia. Wataalamu wanasema kuwa teknolojia hii inaweza kuwa na matumizi mengi zaidi katika siku za usoni.
Uwezo wa Kamera hizi ni kunasa picha kwa saizi ya Milimita na zinaweza kuzoom na kuleta serial namba za Satellite nyingine anga za juu au ardhini kuzoom kwa karibu na kwa uangavu wa juu vitu vidogo sana hali inayowezesha na kuboresha zaidi upelelezi wao...