The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 316
- 589
Kwa mujibu wa mashuhuda, ghorofa hilo lilianguka ghafla saa tatu na dakika tano asubuhi wakati mafundi ujenzi walipokuwa kazini wakitoboa kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka.
"Tulianza kusikia kelele za mtikisiko, kisha kwa ghafla jengo zima likaanguka. Wananchi wameshindwa kujiokoa na zoezi la ujenzi lilianza tangu jana hivyo angetaka urahisi angebomoa tu jengo lote," amesema mmoja wa mashuhuda, Harrison Shayo.
Mfanyabiashara mmoja ambaye hakujitambulisha kwa majina, ameeleza kuwa uchimbaji wa maduka ya chini ndio chanzo cha jengo la ghorofa kuporomoka katika eneo la Kariakoo, mtaa wa Congo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa mtu mmoja amefariki dunia na wengine 28 wameokolewa katika ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Soma pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16
Chanzo: Bongo FM, Mwananchi