Uchawi wa Biashara ni Wateja, tumia gharama zozote kulinda "ulio nao"

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,999
23,400
Katika maisha ya biashara na Ujasiriamali hakuna kitu kizuri kama ukiwa na uhakika wa wateja kila siku, kuna furaha flani amaizing sana isiyoweza simulika.

Mtu ana simu ya ofisi ipo busy kila wakati,wateja wanapga kuuliza bidhaa zimefika au zipo au lah,raha sana ukiwa mfanyabiashara halafu ukawa na nyomi lako la wateja kuna raha isiyopimika.

Kila mtu anafanya biashara anayoijua yeye, Leo naongea na ndugu zangu ambao biashara zenu zime TIKI yani kama ni pepa mmepga 90/100 wengine mna 99/100 wengi wenu mnacheza na matokeo ya A+++

Mkifungua biashara zenu wateja ni wa kugusa tu,wengine hata hamjafika kazini simu zishaanza ingia kuulizwa mnafungua saa ngapi, leo naandika haya kwa ajili yenu.

Kuwa na wateja ni Jambo lingine

Kudumu na wateja ni Jambo lingine

Watu wengi sana nimeshawashuhudia biashara zikiwafia wakiziangalia na wakati biashara zao zilikua zina Jina kubwa hata yeye ana jina kubwa ila biashara zimewafia wateja wamepeperuka wotee.

Hakuna mtu anaeweza kukupeperushia wateja wako,hakuna mtu anaeweza kukuchukulia wateja wako ila ni wewe mwenyewe na namna unavyowatunza wateja wako ndio kutafanya wateja waendelee kubaki kwako au wakukimbie.

Naomba tuambizane namna ya Kutunza wateja Tulio nao

TOA OFA KWA WATEJA ZAKO


Ofa maana yake nini? ofa ni huduma yeyote unayompatia mteja wako bila yeye kuiomba ila unampatia Bure, inaweza isiwe huduma kinaweza kikawa kitu TU au bidhaaa lakini ipo ndani ya ofisi yako.

Boss upo ndani ya ofisi,ameingia mmama/mdada amekuja kuchagua nguo, kachagua Blauz umempga pesa,kachagua skirt umempga pesa wakati anaendelea kuchagua naamini ulikua ukimuona akishka nguo akichagua,uliona namna alivyofika mahali akapenda nguo mbili kwa mpgo ila hela yake ikawa ni yakutosha nguo 1

kwakua hela yake ilitosha nguo 1, atatoa pesa atalipia ile 1,sasa basi wewe kama boss unatakiwa ujue kutoa SADAKA na sadaka zenyewe ndio hizi ofa sio kila siku ila unaweza kutoa hata mara 1 kwa mwezi kulingana na uwezo wa mfuko wako.

Akishalipia ile nguo 1, mwambie "nimekuona umeipenda sana hii nguo kwanini usi inunue na hii"? unamtolea ile nguo aliyoipenda ila akairudsha, unamwambia mimi basi kwakua leo umenunua hizi nguo zote, nimeamua kukununulia na hiiii ili moyo wako uridhike hii n zawadi yangu kwako..

Huyu mteja atahisi wewe ni JINI kwasababu hatoamini kinachotokea mbele yake, huyu mteja kuhama duka lako ni Kifo tu kikutenge nae.

Mfano mwingine

Yawezekana wewe unauza chakula unafanya biashara ya chakula,unajua kabisa bwana Juma anapenda chakula aina gani, dada Asha anapenda chakula aina ipi kwakua una record nzuri ya ulaji wa wateja wako chakufanya ni simpo kabisa.

Tuanze na Bwana Juma anaependa Ugali mlenda na samaki mkavu, Bwana juma amekuja Ofisini kwako kuagiza msosi kama kawaida yake unampelekea mezani wakati akila unajua kbisa anapendaga na maziwa mtindi, Nenda kamletee mtindi bwana Juma mwambia Bwana Juma leo nmekuletea Mtindi ili ule vizuri ugali wangu leo ushindwe wewe TU, mwambie kuwa mtindi ni ofa utaulipia wewe,yeye ale alipie tu chakula chake.

Huyu bwana Juma hata ashinde njaa wiki nzima hatokula mahali pengine popote zaidi ya kwako na ukitaka kumlaza njaa baba wa watu usifungue ofisi.

UTANI


Hakuna kitu kizuri katika maisha kama utani, utani huongeza urafiki,utani huongeza furaha,utani huongeza ukaribu na kumpa mtu uhuru wa kuwasiliana nawewe.. Pendelea watania wateja wako.

Ni kweli unakua bize sana unachoka sana lakini usimalize siku hujatania wateja wako wawili au watatu tofauti tofauti,Acha nitoe mifano miwili ya utani ninayopenda watania nayo wateja wangu.

1.DENI

Mteja yeyote atae ingia ofisni kwangu yani kwanza nakukaribisha vizuri halafu kinachofuata nakumbushia deni langu,Yes huwa wateja wanashtukaga sana utashangaaa ananiuliza kwa mshangao "wee controla unanidai nini mimi" namwambia umesahau eeh,subiri nimalizane na huyu mteja tutakumbushana. Yani mimi kila mteja wangu Namdai na nakuaga serious nikianza wadai,walionizoea wananiambia live kuwa Hawanilipi na nisiwasumbue....

2.MPENZI

Mimi nishazoeleka ofisini kwangu wanawake wote wanaoingia awe dada,awe mama, awe bibi wote ni ma baby zangu kitendo cha kuingia tu Ujue wewe n baby wangu,nina wake wakubwa,wake wadogo yani hata uwe na mumeo Mtajua wenyewe "ukija OFSINI kwangu wewe n Wangu TU", balaa ni pale anapokujaga mama na binti ake Nakuaga bubu sometimes sema najuaga miliki game, sikaagi kimya kukuzingua ni muhimu. (huu utani sio wa ku ufanya kama hujazoeana vilivyo na wateja zako,kuwa makini eneo hili)

KOPESHA


Unajua tunasema katika biashara epuka sana kukopesha na kweli hata mimi nasema leo EPUKA kukopesha na USIKOPESHE kama ukiweza,ofisi zangu sikopeshi ni kweli kumkopesha mteja ni kumkimbiza, lakini kwann nmeiweka ktk vitu vyakumkamata mteja wako na kumtunza?

Kwanza usikopeshe mtu anaekuja ofsini kwako hana hela eti anataka huduma au kitu,Huyo usimkopeshe hata alieje Kama umemuonea huruma we mpe anachotaka ila sio umkopeshe, sasa unakopeshaje hapa?

Mteja anaweza ingia dukani kwako akapenda bidhaa mbili ila mfukoni ana pesa ya bidhaa 1,yawezekana ni nguo kapenda magauni mawili ila hela inatosha gauni 1 tu, Chakufanya baada ya kuligundua hilo

Mwambie kwakua hii pia umeipenda na kwasababu wewe n mteja wangu wa mara kwa mara, naomba nikupe hii nguo kisha wewe siku yyte utakayopata hela yangu utaileta hapa ofisini,hili ni duka lako umedumu muda mrefu sana sasa mimi naomba ichukue hii moyo wako leo uwe na amani,najua ukipata hela utaniletea,Kisha mkabidhi nguo yake.

Huyu mteja umemkopesha kwsbabu kwanza kuna manunuzi ameyafanya ofsini Hakuja direct na gia zake za kuanza kulia lia akopeshwe, Mteja wa namna hiii kuondoka ofisni kwako, Labda anyakuliwe tu vuup apoteee ila sio rahisi.

UPENDELEO

Katika biashara lazima uwe na upendeleo,kulingana na siku na siku unavyojiskia Unaweza mpendelea mteja bei ukamshushia bei kwa 100% yani unamuuzia bei bidhaa ile ile uliyonunulia huko ulipofata mzgo wako.

Hakikisha vitu unavyowapendelea wateja wako n zile huduma/vitu wanavyovipenda na kuvihitaji, Mfano mimi ofisini kwangu nina bidhaa ambazo siuzi chini ya faida ya 50k yani chini ya 50k (faida) sikupi lakni kuna siku huwa naamka nasema leo mteja ataekutana na mimi lazima a smile, bidhaa ile ile ambayo siuzagi faida isiyopungua 50k ntampa mteja kwa faida hata 10k tu,ntachukua kisha namwambia Hii nimekupendelea wewe TU leo iwe siri yako. Huwa wateja n waelewa maana wanajua hawawezi pata hicho kitu popote kwa bei niliyompa,Basi anaenda zake akiwa na amani.

Unaweza ukapendelea wateja wako kwa namna tofauti tofauti, kama n muuza chakula unajua kabisa huyu mteja wangu utumbo wake ni mithili ya sox hashibagi chakula cha 1500, na kwakua kaja na 1500 hyo hyo sasa wewe leo mpendelee mtilie msosi wa 2500 wakushiba halafu mwambie leo nataka ushibeeeee.... Atavyokenua meno hutoamini...

KUBALI HASARA


Hivi umeshawahi kupata mteja ameingia ofisini mwako halafu akawa hajui kama kabati halitakiwi kuegemewa akaegamia mara paaap viooo vyote chaliiiii, usikasirike linapotokea hili jambo (japo n hasara) ila usikasirike ONYESHA UTU mpe poleee sana na mwambie asijaliii kabisaaaa, mpeti petiiii muondoe hofuuuu, usije ukafanya makosa kama wafanyayo wafanyabiashara wengine kuwalipisha wateja zao wanapoharibu vitu USIFANYE HAYO.

au kuna wamama wanaingia na watoto ofisini,ki ukweli kuna watoto watundu kuna kitoto kishakujaga ofisni kikanitia hasara ya 600k kilivunja kitu ambayo laiti angekua kavunja Mtu ninae mmudu asee ningembeba mgongoni nitembee nae wiki nzima, ile kitu nili ipotezea with a soft smile, kitendo kile kilifanya yule mteja hadi leo hii atake hata bidhaaa ya milions of money lazima anishirikishe mimi nitoe go ahead ndio aendeleee, ninachotaka kusema n kwamba,Jifunze kukubali hasara zinazo sababishwa na wateja wako.

ZAWADI

kutoa zawadi si mpaka uwe na pesa unajua eh,kuna wakati unaweza ukajiskia tu kutoa zawadi kwa wateja wako zawadi zenyewe si kubwa n vitu vidogo vidogo tu, mko ofisni nnje anapta kijana na kibegi cha bakhressa Muite yule kijana mwambie ampe kila mteja wako kitu anachotaka, waache wateja wajichukulie ice cream na kila kilichopo mule ndani ya kile kibegi kisha walipie.

Anaweza akapta muuza karanga,muite muuza karanga mwambie awape wateja wako karanga kila anae hitaji,fanya hv kwa kila unachojiskia kwa wateja wako zawadi ziko nyingi kila mtu atoe zawadi kwa wateja wake kulingana na uwezo alio nao.

TATUA MATATIZO YAO

Umeshawahi pata mteja anakuj ofisni kwako unamuhudumia huku analalamika na mambo ya nyumbani kwake, unaweza mskia yani binti angu wa kazi katoroka hapa nawaza sijui nani atabaki na wanangu, Msaidie haraka iwezekanavyo kumtaftia binti wa kazi huyu mteja wako,kama unaweza.

au mteja anafika ofisni anakwambia daaah yani leo nmeibiwa simu kwenye dala dala sijui kesho kazini naendaje mimi,ningekua hata na kisimu kidg chakuweka laini ningeweka kalaini kangu kale ka voda, Kama una simu ndogo mahali mpe mteja wako mwambie Tumia hiii kisha ukipata simu unirudshie simu yangu isaidie na wenzako,atashukuru na atafurahi sana.

au kama una skills za kutrack simu na kujua namna ya kupata simu iliyoibiwa basi mwambie akuletee details za simu iliyopotea kisha fanyia kazi swala lake ukipata simu yake mrejesheee,Atakushukuru si kawaida.

Matatizo ni mengi lakini yote kwa yote usiruhusu wateja zako wakaingia ofisini kwako wakilalamika na wakati uwezo wakutatua matatizo yanayowasibu unao, hebu kuwa sehemu ya maisha ya wateja zako wafanyie na waonyeshe how customer care ipo.

Mbinu ziko nyingi sana za kufanya wateja wako wasichukuliwe na mtu yeyote yule,zipo zaidi ya hizi nilizoandika ila nmeandka hizi chache ili kufahamisha wasiojua namna ya kutunza wateja wanaowapata Ukauzu uboss hautokutoa hapo ulipo,unapokua ofisini fanya ie sehemu ya amani na furaha kwa kila ataetia mguu ofisni kwako.

Ukitaka kujua wateja LOYAL wanapatikanaje basi fanya haya niliyoyagusia na mengine kisha utaona kama kuna siku utafungua bishara ife au ishindwe kudumu, Biashara ni Tamu na Nzuri ukiwa na uhakika wa wateja lakini sio wateja wakuja na kuondoka,wateja ambao hata akihama Dar akahamia dodoma bado atakupgia simu umtumie kitu flani, Hata akihamia kigoma bado atakupgia simu akuulize kuhusu jambo flani,Tengeneza aina hiyo ya wateja Gusa mioyo yao kwa namna flani, tumia ofisi yako kufanya wateja waone Walichelewa kukujua.
 
Screenshot_20220317-211726.jpg
Nimeanza kuufanyia kazi acha tuone itakuaje
 
Wateja ndio mambo wanayoyapenda hayo,wapo kama watoto danganya toto kibaoooo "wote wanajaaa kwako" watu wanakuita mchawi kumbe biashara haitaki nguvu nyingi ni akili tu.
 
Huwa sitoagi likes kwa thread za watu humu ama ktk mitandao yoyote ya kijamij lkn kwako nakupa LIKE ya nguvu ase, kuna moja ama mbili kati ya hayo uliyoorodhesha nikiifanyia kazi na kweli ikawa Good na inasaidia.

Shida ni kwamba wafanyabiashara wengi wa kibongo ni wabishi na wavivu wa kujifunza mbinu mpya za kibiashara.

Na wengi wanavamia hii kazi bila kutaka kujua maarifa ya biashra na mbinu za kuwashika wateja, hiv mm nina wateja wangu wamekuwa kama mateja wa bidhaa zangu, bila mm kuwepo hawafanyi manunuzi sehemu yoyote ile.

Congratulation
 
Back
Top Bottom