Uchambuzi wa EP ya Prof. Jay

KJ07

JF-Expert Member
Dec 17, 2021
2,284
5,198
Screenshot_20231213-121349.png

Salaaam wakuu wa JamiiForums,

Tarehe 10/12/2023 kulikuwa na uzinduzi wa taasisi ya professorjay foundation ambayo lengo lake kuu ni kukusanya michango kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa figo ambapo matibabu yake yanagharimu kiasi kikubwa cha pesa hivyo kuwafanya watu wasio na uwezo kushindwa kuhimili matibabu.

Baada ya uzinduzi wa taasisi hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri na maarufu hapa Tanzania na wengi wao kuchangia kwa viwango tofauti kwenye taasisi hiyo.

Tukio lililofuata ni kuachiwa kwa Extended Playlist(EP) ambayo inaenda kwa jina la NUSU PEPONI NUSU KUZIMU.

EP hiyo ya mkongwe huyo katika bongoflava hasa miondoko ya hiphop professor jay ina nyimbo nne(4)
  • Siku 462- ft walter chilambo
  • Calling- ft alikiba
  • Hayakuhusu
  • Shemeji shemeji- ft ndelah
Tatu za mwanzo zikiwa zimetengenezwa na producer binladen na moja ya mwisho ikiwa imetengenezwa na producer sulesh. Nikienda moja kwa moja kwenye uchambuzi wa nyimbo hizo;

1: SIKU 462
Ngoma hii ni miongoni mwa ngoma ambazo ziliteka hisia za wasikilizaji wengi hasa baada ya kusikia mabadiliko makubwa katika uimbaji hasa sauti ya mtaalamu professor jay. Professor aliflow kwa namna ambayo imeacha watu wengi wakitiririsha machozi baada ya kuisikiliza kwa mara ya kwanza akiwemo mimi.

Nyimbo inaelezea safari nzima ya kuumwa kwa professor jay, maswaibu aliyoyapitia, maombi ya watanzania dhidi yake, matibabu yake kwa ujumla mpaka alivyopata unafuu. Nyimbo hii ilijumuishwa kwenye EP Mpya hiyo lakini tarayi ilikuwa imeshasikika masikioni mwa wasikilizaji.

Miongoni mwa part zilizoliza watu pia ni namna Walter chilambo alivyokuwa anatembea na chorus. Sikumbuki nyimbo hii nimeisikiliza mara ngapi ila nakumbuka kuna siku niliisikiliza siku nzima na kugundua mambo mengi sana kwenye kila msikilizo mmoja niliousikiliza.
This is the legend professor jay

2: CALLING
Nyimbo hii ni mpya katika EP hiyo huku akiwa amemshirikisha Alikiba na huku mtindo ukiwa ni ule ule wa storytelling ikitoa story ya kijana mmoja ambaye anaonekana kupitia maisha magumu sana akilelewa na mama wa kambo baada ya mama yake mzazi kufariki.

Alipitia changamoto nyingi lakini huku akipambana na elimu kwa ugumu alifanikiwa na kuweza kuwasaidia wadogo zake. Nyimbo hii sauti halisi ya professor jay inaanza kusikika ukitofatisha na sauti ile ya kwenye nyimbo ya SIKU 462. Nyimbo hii pia ina toa mafunzo fulani ambayo nimeyapata kwa harakaharaka.

3: HAYAKUHUSU
Nyimbo fulani hivi ya kuchangamka ikiwa na mahadhi kama bongo piano. Kama title ya nyimbo professor jay ana wadis watu ambao kazi yao ni kufuatilia mambo yasiyowahusu. Energy ya Professor Jay katika nyimbo hii inatupa matumaini ikiwa nyimbo hii ilifanywa baada ya kutoka hospitali.

Tuendelee kuamini kuwa ipo siku mwamba atarudi katika hali yake ya uzima kama zamani japo juzi kwenye uzinduzi wa EP yake alionekana kutembea na wheelchair (kitimwendo).

4: SHEMEJI SHEMEJI
Nyimbo ambayo inatoa story ya familia fulani hivi ambayo wahusika wa hiyo familia ni watu wa ugomvi, usaliti, kudharauliana huku wakiwaasa kulea watoto maana malezi bora ya watoto yanawahitaji wazazi wote wawili.

Mwisho wanawashauri wapatane na kusameheana madhaifu yao na kuacha michepuko.
Nyimbo hii pia professor jay ameflow na energy nzuri. Hakika Mungu ni mkuu ukimtumainia yeye. Kwa hali aliyokuwa nayo professor jay basi ni neema ya Mungu tu mpaka leo tuko nae hapa.

Jina la EP ni NUSU PEPONI NUSU KUZIMU. Ikiwa na maana kwamba katika mapitio yote aliyoyapitia alikuwa ni kama mfu ila baada ya mapitio yote leo hii ni mzima. Japo afya yake bado haijaimarika na kuwa kamili.

Hakika Mungu ni Mkuu.

Sikiliza nyimbo ya kwanza utaelewa ninachokiongea. Au tembelea na kufatilia historia za wagonjwa mahospitalini na mapitio wanayoyapitia.

Itaendelea..................
 
Nyimbo zinapatikana katika digital platforms zote hivyo ni vyema ukienda kusikiliza huko uzuri majina nimeyaweka ili kulinda hakimiliki ya Professor jay
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom