Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,452
- 22,145
Uchaguzi wa Marekani umetoa majibu kwamba raisi ajaye ni Donald Trump akiwa raisi wa 47 wa nchi hiyo lakini pia akirudi kutawala taifa hilo kubwa duniani kwa ushindi wa kishindo.
Donald Trump alikuwa raisi wa Marekani kwa muhula mmoja toka mwaka 2016 hadi mwaka 2020 aliposhindwa na raisi Joe Biden ushindi ambao Donald Trump alidai umepikwa.
Pia tarehe 6, mwezi January mwaka huo wa 2020 dunia ilishuhudia taifa la Marekani likiingia katika vurugu pale wananchi walokuwa wakimuunga mkono Donald Trump walipoamua kwenda Capitol Hill kufanya vurugu.
Donald Trump aliendelea kudai uchaguzi huo wa mwaka 2020 ulidukuliwa na matokeo yake yalipokwa jambo ambalo lilimtia katika matatizo na mahakama nchini humo ambapo hadi leo mwendesha mashtaka bwana Jack Smith ameanza kufikiria kufuta kesi hizo baada ya Donald Trump kuchaguliwa kwa kishindo.
Donald Trump atakuwa ni raisi mwenye nguvu zaidi kuliko maraisi wote wa Marekani walowahi kupita ambapo chama chake cha Republican kitaweza kusimamia mabunge yote mawili yaani lile bunge la la mabwanyenye la Seneti na bunge la wawakilishi baada ya wabunge wengi wa kuwa ni wa chama hicho.
Raisi mtarajiwa Donald Trump ataweza kutoa maamuzi mengi mazito ambayo hayataweza kupingwa na sehemu yoyote ile hususan Bunge ambalo litapitisha sheria nyingi ambazo zitajadiliwa nalo huku mahakama karibu zote za Marekani ambazo zimeshutumiwa na Donald Trump kutumika na chama cha Democrats kutaka kummaliza kisiasa zikijiandaa kusikiliza amri kutoka kwa amiri jeshi mkuu Donald Trump.
Lakini je uchaguzi huu umetufikirisha nini sie mashuhuda ambao tumeshuhudia Donald Trump akipigana kufa na kupona usiku na mchana kujaribu kuingia tena Ikulu ya Marekani au White House?
Ikumbukwe kuwa katika pilikapilika zake hizo Donald Trump amenusurika mara mbili kutaka kuuawa na pia amekumbana na kesi zaidi ya 7 mahakamani huku akikabiliwa na mashtaka zaidi ya 30.
Kilichobakia ni tarehe rasmi za matukio ambazo ni kama zifuatavyo:
Tarehe 26 Novemba, kutakuwa na hukumu juu ya kesi za Donald Trump, tarehe 6 Januari ndo siku Kamala harris atatangaza rasmi ushindi wa Donald Trump na baadae mwezi huhuo yaani tarehe 26 januari ndo siku ya Donald Trump kuapishwa ramsi kuwa raisi wa 47 wa Marekani.
Sasa tuangalie ni sababu zipi ambazo zimechangia kwa Kalama Harris kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu?
1. Kamala Harris hakuwa mtu sahihi kugombea uraisi kushindana na Donald Trump.
Mara tu jina la Kamala Harris kutangazwa kuwa mgombea wa chama cha Democrats wengi tulianza kuwa na uhakika wa ushindi wa Donald Trump.
Chama cha Democrats kilikosa kufanya utafiti wa kina kuona kama Kamala Harris ana sifa za kuwa raisi wa Marekani ukizingatia kuwa amekuwa makamu wa Joe Biden na huku akiwa nyuma ya pazia huku masuala mengi ya kitaifa akiachiwa Joe Biden na wasemaji wa Ikulu akina John Kirby, Jack Sullivan na wengine ambao wengi ni watu wa idara ya usalama ingawa masuala hayo kama suala la Gaza. Hivyo uteuzi wake wa kuwa mgombea wa moja kwa moja kushindana na Donald Trump hakukuwa sahihi.
2. Kukosa ajenda rasmi.
Wakati Donald Trump akiwa na ajenda ya kuahkikisha taifa hilo lajikwamua kiuchumi, na kuhakikisha wahamiaji haramu wote wanaondolewa nchini humo, Kamala Harris alijikita zaidi wkenye mashambulizi binafsi yaani "personal attacks". Kila mara Kamala alikuwa akisifia kuwa yeye ni mwanasheria hivyo anapambana na mhalifu akimaanisha kuwa Donald Trump ni mhalifu tu hivyo hana sifa ya kuwa raisi isipokuwa yeye Kamala Harris.
Kwa mfano suala la mfumuko wa bei lilikuwa ni suala nyeti kwa taifa la Marekani na hivyo lilihitaji chama cha Democrtas kulielezea ni kwa jinsi gani wangelikabili. Hivyo Kamala Harris alipaswa kufanya suala hilo kuwa ni moja ya ajenda kuu.
Soma Pia: Donald Trump ashinda Urais wa Marekani kwa 51.05% dhidi ya Harris Kamala aliyepata 47.46%
3. Kukosa Mvuto.
Kamala Harris alikosa mvuto kwa wapiga kura khasa wale wa kilatino na wamarekani weusi. Wengi watashangaa sana kusikia kuwa wamarekani weusi wengi ndo wamechangia kumpa kura nyingi Donald Trump badala la Kamala Harris. Hii ni kwasababu ya mvuto wa kusikiliza hoja ya mtu ambae ana ushawishi.
Donald Trump pamoja na makandokando yake ana mvuto wa kibiashara kwamba ana ufahamu wa namna ya kuvuta wateja wake. Pia idadi kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 26 wengi wamejitokeza kumpa kura Donald Trump kutokana na kuvutiwa nae.Timu ya kampeni ya Kamala Harris ailikosa hii stratejia ya kuvuta watu kwa hoja zako.
4. Kampeni kuwa semina badala ya shughuli za mkutano wa kampeni.
Kamala Harris na timu yake ya kampeni na chama chao cha Democrats waligeuza majukwaa ya kampeni kuwa kama semina badala ya majukwa ya shughuli za kiwandani yaani "factory floor". Hivyo Kamala Harris alipokuwa akizungumza jukwaani hakuwa akishuka hoja baada ya hoja na badala yake alikuwa akichanganya hoja na kuishia katikati hivyo kukosa ule mtiririko. kwa upande wa Donald Trump yeye na timu yake ya kampeni walikuwa kama wako kiwandani wakipiga kazi. Pia walitumia podcast, mitandao ya kijamii kujichanganya na wapoga kuwa watarajiwa huku hata mwanae Baron Trump nae akishiriki kumsaidia baba yake khasa kwenye mitandao ya internet hivyo kuvuta wapiga kura wengi wa kizazi cha Z, au Generation Z.
Pia mapema mwezi Juni mwaka huu Baron alimshauri baba yake kuingia kwenye Podcast ya Logan Paul ambae ni mtu maarufu katika mtandao wa You Tube katika podcast yake iitwayo Impaulsive, hivyo tayari Donald Trump kitambo alikuwa amejikita kwa wapiga kura akiongea nao kwa kubadilishana nao mawazo.
5. Kujitofatisha na Joe Biden kisera na kimtazamo.
Kamala Harris alikosea sana pale alipokosa kutwaa jukwaa na kujitofautisha na Joe Biden. Hii ilikuwa ni fursa kwa Kamala kujimwambafwai na kuwaeleza wapiga kura kuwa yeye angekuja akiwa mtu tofauti na mwenye mtazamo tofauti juu ya masuala mengi hususan suala la Mashariki ya kati na mauaji yanoendelea kufanywa na Israeli huko Gaza na sehemu zingine katika eneo hilo.
6. Utovu wa nidhamu kwa wapiga kura.
Katika moja ya mikutano yake ya kampeni Kamala Harris akiwa Springfield kwenye maji wa Ohio alidai kuwa wahamiaji wa kutoka Haiti wanakula wanyama wa kufugwa majumbani, kama mbwa na paka jambo lilozusha tafrani na hasira kali kutoka kwa jamii wa watu wa kutoka Haiti waishio Marekani hivyo kupoteza kura zao. Kushindilia misumari zaidi kwenye jeneza la chama cha democrats mmoja wa wanasanii wanomuunga mkono Kamala Harris bwana Tony Hinchcliff alitamka jukwaani kuwakashifu wapiga kura wa kutoka kisiwa cha Puerto Ricco kwamba kisiwa hicho ni uchafu unoelea, akiwalenga wapiga kura wa kutoka kisiwa hicho walokuwa walihudhuria mkutano wa kampeni wa Donald Trump pale kwenye bustani za Madison Square.
Kwa kuhitimisha haya machache ni kwamba uchaguzi si lelemama bali ni kazi ngumu unohitaji maandalizi na stratejia iloshiba.
Wengi wanashangaa kuona jinsi ushindi wa Donald Trump ulivyoweza kuitikisa Dunia na kuifanya Dunia hii ikae mkao wa kula kumsubiri Donald Trump aapishwe rasmi mwezi Januari mwaka 2025. Lakini huu ni ushindi halali kabisa ambao umetolewa na wapiga kura wanojitambua na kwmaba wahitaji mtu ambae atakidhi mahitaji yao na kuwahakikishai usalama wao na atakaelinda maslahi ya Marekani.