Uchambuzi: Kuondolewa Lowassa Urais CCM Ndio Mwanzo wa Siasa za Ukabila/Ukanda Tanzania

Onesmo Kyauke

Member
Feb 9, 2015
67
119
Mwalimu Nyerere alisema " Ukimchana Mtanzania kidogo tu utapata damu ya ukabila na udini ipo karibu sana." Mwl alikuwa sahihi maana umoja wetu uliletwa na kitu kimoja tu, nacho ni "Siasa Safi."

Kwa majirani zetu wa Kenya ambao ukabila umeshamiri, mkoloni hakuacha ukabila. Odinga Snr ndie alikuwa awe Waziri Mkuu wakati huo kenyatta akiwa kizuizini lakini akakataa na akasema wazi kuwa lazima Kenyatta aachiwe na yeye atakuwa Makamu wake. Kungekuwa na ukabila asingeacha kukamata madaraka na kumfunika Kenyatta. Baadae kukaanza siasa chafu za " Jaluo hawezi kuwa Rais." Kilichotokea ni Wajaluo kuhujumiwa na kutengwa na mwishowe walivyoona wanaonewa kana kwamba si wakenya kamili wakaanza kujenga umoja kwa ajili ya kushinikiza maslahi yao na kujilinda pia. Hii dhana ikaenea kwa makabila mengine na ndio Kenya tunayoiona leo.

Hapa Tanzania, huko nyuma zilitolewa kauli za baadhi ya wana CCM kuwa Rais wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini. Sijui kwamba Kaskazini si watanzania au wamefanya dhambi gani. Kwa masikitiko kabisa chama hakikutoa kauli rasmi kukanusha au kuipinga kauli hii.

Yaliyotokea Dodoma tumeyaona. Kwa ufupi kabisa ukiisoma Katiba ya CCM inasema kikao cha mwanzo cha kuchuja majina ya wagombea urais ni Kamati Kuu. Na moja ya kazi za Kamati Kuu kwa mujibu wa Ibara ya 109 (6)(b) ni kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa H/K majina ya wanachama wasiozidi 5 kwa nafasi ya mgombea urais. Kwa makusudi kabisa K/K ilinyang'anywa mamlaka yake ya kikatiba ya kufikiria.... Kamati Kuu ingefikiriaje kama haikupelekewa baadhi ya majina?

Chama cha Mapinduzi kina haki ya kumkataa mtu asigombee. Lakini lazima zitolewe sababu za kukata jina la mtu lakini pia jina linapaswa kukatwa na kikao chenye mamlaka ya kikatiba ya kufanya hivyo. Hatuwezi kujenga umoja wa nchi kwa kuishi kwa hisia kwamba mtu fulani ni fisadi wakati hajawahi kuambiwa rasmi kuwa yeye ni fisadi ili ajipime kama bado anaweza kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Mwalimu Nyerere alivyompinga Malecela aliuelezea umma udhaifu wa Malecela na akamwandikia hadi kitabu kueleza kwanini Malecela hafai. Malecela hakuondolewa kwa hila bali alitakiwa ajipime na aone kama kweli anaweza kupeperusha bendera ya CCM pamoja na udhaifu wake. Malecela baada ya kujipima aliamua kujiondoa mweyewe kwanye mbio za urais. Je, unadhani Malecela angeondolewa kwa hila bila kuambiwa kwa uwazi madhambi yake angeridhika?

Tumekuwa tunasikia kwa chinichini kuwa Lowassa ni fisadi. Kwa miaka nane ya umbea hakuna kiongozi wa juu wa CCM aliyetoka hadharani akataja ufisadi wa Lowassa upo wapi. Hakuna aliyesema Lowassa ameiba kiasi gani. Hatukuambiwa kama Lowassa ni mwizi kwanini asipelekwe mahakamani kama wengine. Tumebaki tunabweka kama mazuzu kwamba fulani fisadi bila hata kusema hasa ufisadi wake ni nini.

Kujiuzulu pekee hakutoshi kusema mtu ni fisadi maana hata Mzee Mwinyi alijiuzulu kwa kuwajibika na baadae aliteuliwa kugombea urais. Na ukihesabu utakuta mawaziri waliojiuzulu Tanzania ni wengi ila kwa sababu ambazo hazieleweki Lowassa ndie amekuwa "victim" wa siasa za kuchafuana. Kama nilimwelewa alisema kwa vile nchi ilikuwa gizani ilikuwa lazima hatua za haraka zichukuliwe kutafuta umeme na hivyo utaratibu wa kawaida wa tender ambao ungechukua muda mrefu usingeweza kufanyika katika hali ya dharura. Lakini pia alisema wenzake serikalini waliambiwa na hivyo hakufanya kwa siri. Mwisho wa siku hatukuambiwa aerikali ilipata hasara ya shilingi ngapi kwa maamuzi yaliyofanywa.

Kwa maoni yangu CCM imefanya makosa makubwa ambayo yanaweza kuigharimu nchi kwa kumwondoa Lowassa kwa hila. Wangemweleza makosa yake na akaambiwa ajipime na akaondoka huku akijua makosa yake na watanzania wakaambiwa ukweli ulivyo, asingepata nafasi ya kulalamika.

Kwa vita aliyopigwa ikiambatana na kuvunja katiba ili kuhakikisha anaondolewa inaimarisha hoja ya "Rais hatatoka Kaskazini" maana watu wameanza kujenga hisia hizo kwamba kwa vile hatukuelezwa makosa ya EL huenda aliondolewa kwa ukaskazini wake. Huwezi kuwakataza watu kufikiri hivyo isipokuwa pale watakapopata majibu ya kutosha.

Madhara yake ni nini? Watu wa kaskazini wata fight back kuwa tunaonewa na matokeo yake zitaanza taratibu kujengeka siasa ya ukanda huku zikinyemelewa na udini. Yaliyotokea Monduli si ya kupuuza hata kidogo. Nini kifanyike? CCM itoke hadharani iwaombe radhi wanachama wake kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba na kanuni za chama.

Pili, itueleze bila kumung'unya maneno, tatizo la kimaadili analoshutumiwa nalo Lowassa ni lipi. Baada ya hapo yeye atapata nafasi ya kujitetea lakini angalao yeye na watanzania wengine wataridhika na kuendelea na siasa za umoja. Tukiendeleza vijembe badala ya kutatua tatizo kwa uwazi na ukweli nchi itatumbukia kwenye siasa mbaya za ukanda ambazo zitatuathiri wote.

Nasisitiza, hapa hakuna uchama. Wale wanaoonewa watasahau vyama vyao watajikuta wapo kwenye chama fulani kwa convenience tu ili wapiganie maslahi yao kwa pamoja.

Haya ni maoni yangu tu wala hayana uhusiano na siasa za vyama.

OK.
 
Kuna tatizo kubwa tusilolijua wengi wetu, nalo ni vijana waliosoma kimagumashi walioko CCM wamejikuta kwenye nafasi kubwa ghafla na wana malengo ya baadae ya kuitawala tatizo kama baba zao. Wazee wa CCM wanashtuka late, hawa ni January Makamba, Nape Nnauye, Ridhiwani Kikwete na network yao unachokiona leo ni maandalizi ya baadae.

Watagombea Ubunge watapatiwa Uwaziri watajiandaa kwa 2025 ila nchi itayumba kama hawadhibitiwi ni mtandao hatari Zitto Zuberi Kabwe yupo kundi hili pia.
 
kuna tatizo kubwa tusilolijua wengi wetu, nalo ni vijana waliosoma kimagumashi walioko CCM wamejikuta kwenye nafasi kubwa ghafla na wana malengo ya baadae ya kuitawala tz kama baba zao. wazee wa ccm wanastuka late ,hawa ni j makamba, nape nauye, riz kikwete nanetwork yao unachokiona leo ni maandalizi ya baadae. watagombea ubunge watapatiwa uwaziri watajiandaa kwa 2025 ila nchi itayumba kama hawadhibitiwi ni mtandao hatari zzk yupo kundi hili pia
Mliosoma kihalali mkowapi
 
Powerful analysis. Kwa nini tusiwekwe wazi, badala yake hayo aliyofanyiwa yanaweza kumpa Edward Lowassa political advantage akakimbilia Chama kingine na akashinda urais.

So waliombania wakawa hawajafanya kitu.
 
Hivi hao wengine waliokatwa walielezwa sababu za kukatwa majina yao?

Mi nadhani suala la "Rais hatatoka kaskazini" lisingehusianishwa na kukatwa kwa Lowasa bali kauli hiyo yenyewe inajitosheleza kama ilivyojitosheleza ya "Kuingia Ikulu kwa Bao la Mkono"
 
Wamekatwa wengine 34 akiwemo Lowassa!, hakuna sababu zozote so far zilizotolewa, kwanini wamekatwa, wala sababu za kukatwa kwake sio Ukaskazini wake. Amekatwa mtu aliyekuwa Jaji Mkuu, amekatwa Makamo wa Rais, amekatwa Waziri Mkuu, what the hell is kukatwa kwa Lowassa tuu ndiko kunakopigiwa kelele nyingi humu JamiiForums

Kwani chama ni lazima CCM, kila siku nimesema humu, kama Lowassa ni chaguo la watu, kipenzi cha Watanzania, amegombea kupitia CCM amekatwa, then atoke CCM, agombee kupitia chama kingine chochote, sisi Watanzania tunaompenda, tutamchagua na kumuingiza Ikulu.

Lowassa ni kada mkongwe wa CCM anajua all the games that CCM plays, yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anajua how dirty games that politics plays, na the fomular ni ile ile ya what goes around, comes around,msitake kutuletea tatizo la mkuki ni kwa nguruwe tuu, lakini kwa binadamu mchungu.

Lowassa mwenyewe anajua kila kitu ndio maana amejinyamazia.

Pasco
 
Pasco


Naamini unaelewa kwa upeo wako ni nini athari ya mbwa mwitu wanapoamua kuparurana wao kwa wao.

Hata JK ktk vita hii ni mshindwa ingawa anaweza jifariji.

Mkapa anarejea mamlakani kwa mlango wa nyuma ha ha ha politics bana.

Twende mbele turudi nyuma ile kauli ya Rais hawezi toka kaskazini imekemewa lini na wakuu wa chama?

Weka akiba ya maneno.
 
Last edited by a moderator:
Nyerere ndo wa kwanza kuwabagua watu wa kaskazini na kutataja makabila makubwa km Wa-haya, Wanya-kyusa na Wa-chagga kuwa hawatakiwi kuwa viongozi. #Uongozi unaenda na meritsna sio vigezo vya ukanda, kikabila , udini na rangi.

Historia ya Tanganyika na aliyopropagate Nyerere imewaweka kando viongozi wa makabila ya kaskazini. Mfano Kina Japhet Kirilo na Marealle ambao walikwenda UNO kutafuta haki ya watanzania. Mangi Meli aliwapinga Wajerumani hadi wakamnyonga haradhani. Akina Aikaeli Mbowe nasikia walimchangia nauli wakati wa kutafuta uhuru lakini hakuwathamini?.

Akina Guninita na Ditopile wakaendelea kuwaona wabara wana tongotongo, wasio wastaarabu na wasiofaa kupewa uongozi Tz.

Endelea.
 
Pasco

Hoja si kukatwa hoja je mchakato umefuata taratibu na maamuzi kufanywa na mamlaka husika?

Kama mwana CCM mwanzilishi na sasa mfu walioiteka nyara CCM wanavunja taratibu za chama na kutumia mamlaka vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Mijadala ya masuala! Ahsante Pasco. Kama JF inataka isimame kwenye ukweli, wachangiaje wapunguze mahaba au watangaze maslahi ya wanalolijadili ili tuwajue kwanini wanajadili wanavyojadili.

PM, VP, JM ni watu wazito sana kukatwa bila kujadiliwa, nini hasa cha maalum toka kwa Lowasa?
 
Last edited by a moderator:
Kwani Kamati ya Maadili imeanza mwaka huu? Hawakujua kama haipo kikatiba kabla hawajaingia mchezoni? Au ndo "hamkujiandaa kushindwa?".
Ni sawa na wapinzani mpigwe magoli ya mkono October halafu mje mseme "Tume Huru". Tutawatia bakora.
 
Onesmo Kyauke,

Hivi hizi political obscenities za "MTU wa kaskazini hawezi kuwa rais" ni kitisho kwa nani? Mmeamua kukimbilia kwenye kete ya mwisho mliyobaki nayo - ukabila.

Nyanda za juu hazijatoa rais wala waziri mkuu - Mwandosya kakatwa wako kimya. Kati hawajatoa rais Mwigulu kakatwa, wako kimya! 1995 Malecela alikatwa hakuna aliyesema amekatwa sababu ilisemwa rais hawezi kutoka kati.

Washabiki na wafuasi wa Lowasa kuweni wastaarabu na mtoe analysis na argument zenye akili badala ya kukimbilia ukabila. Inaonekana toka mwanzo mna nia mbaya tu. Kwa nini wakatwaji wengine wote wako kimya? Hizo taratibu mbaya hawakuziona? Au ninyi ndo mlikuwa mnautaka urais kuliko wote? Kwa nia gani?

Hakuna jipya. Hizi hila za ukabila inaonekana mnazo tu! Kaskazini wameshatoa mawaziri wakuu Mara 4! Zaidi ya kanda zote. Acheni uzushi, gilba na hula, hazitawafikisha mbali!! Analysis inatakiwa ziwe balanced, zitueleze kuwa Lowasa hakuvunja kanuni za uchaguzi wa ndani ya Chama!

Ikiwa ni Lowasa mwenyewe anayewatuma kuleta hizi hoja mfu za ukabila, mwambieni ameshashindwa. Mrema alipoona hajaridhika mara moja alikwenda NCCR mageuzi na ilichukua Mwalimu kuingia ulingoni kumsaidia mgombea wa CCM. Wote hatimaye tulijua ni nini kingetokea ikiwa NCCR ya wakati ule ingechukua nchi.

Sasa, na ninyi mshaurini Lowasa wenu aende kwenye vyama vingine tuone kama CCM watapata Mwalimu mwingine wa kuwapigia kampeni. Lakini hakikisheni kuwa Lowasa wenu ni mtu safi.
 
Last edited by a moderator:
Wamekatwa wengine 34 akiwemo Lowassa!, hakuna sababu zozote so far zilizotolewa, kwanini wamekatwa, wala sababu za kukatwa kwake sio Ukaskazini wake!. Amekatwa mtu aliyekuwa Jaji Mkuu, amekatwa Makamo wa Rais, amekatwa Waziri Mkuu!, what the hell is kukatwa kwa Lowassa tuu ndiko kunakopigiwa kelele nyingi humu jf?!.

Kwani chama ni lazima CCM?!, kila siku nimesema humu, kama Lowassa ni chaguo la watu, kipenzi cha Watanzania, amegombea kupitia CCM amekatwa, then atoke CCM, agombee kupitia chama kingine chochote, sisi Watanzania tunaompenda, tutamchagua na kumuingiza Ikulu.

Lowassa ni kada mkongwe wa CCM anajua all the games that CCM plays!, yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, hivyo anajua how dirty games that politics plays, na the fomular ni ile ile ya what goes around, comes around,msitake kutuletea tatizo la mkuki ni kwa nguruwe tuu!, lakini kwa binadamu mchungu!.

Lowassa mwenyewe anajua kila kitu ndio maana amejinyamazia!.

Pasco

This could be your namesake not the really Pasco I know.
 
Waliokuwa wana muunga mkono walitoka pande zote za nchi hii. Visiwani, kusini mpaka kanda ya ziwa. Hawakuwa na mawazo ya kanda wale watu.

Ninachoamin mimi, kwa uwekezaji aliofanya na kama yasingekuwa mawaa wanayosema anayo angepitishwa tu agombee kupitia ccm hata kama ni wa kaskazini au angetoka kabila kubwa.

Na hii huenda isingejalisha kama ana mawasliano mazuri na wakuu wa chama au lah,
Na yeye kama mwanasiasa nashangaa kutokuwa in good terms na wakubwa na wastaafu kadhaa chamani kwake - Kikwete, Mkapa, mwinyi, karume, malecela, na huenda hata warioba etc. Angeshinda ingekuwaje kwao? Anyway mwingine anaweza sema kwani wao ni nani? Lakini wao si kama wengi wetu

Kumekuwa kuna mapungufu mengi huko juu. Wakubwa wamekuwa wakishirikiana kwenye madudu mengi. Siamin kama kuna dudu linafanywa na mtu mmoja. Kwahyo kumshitaki juu ya Richmond na mambo kama hayo ni pamoja na kuridhia wew mwenyewe kujishtak juu ya kashfa hiyo hiyo. Ni kwamba wanajuana. Maana katika kila kashfa wanakuwa pamoja. Wakisema mwenzao si msafi wanakuwa wanajua, wanakuwa wana uhakika

Ndio maana wengine siku zote tumekuwa tukimtaka magufuli. Na hata aLipopitishwa hatukutaka kamwe kuangalia kapitaje. Katika mazingira ya matumizi makubwa ya fedha zisizo julikana hata zimetoka wapi ilikuwa ngumu kwa magufuli kupita.

Tunaamini magufuli ataendeleA kuwa magufuli yule yule.
 
Nyerere ndo wa kwanza kuwabagua watu wa kaskazini na kutataja makabilaya Wahaya, Wanyakyusa na Waxhanga kuwa hawatakiwi kuwa viongozi. Uongozi unaenda na merits sio vigezo vya ukanda, kikabila , udini na rangi.

Historia ya Tanganyika na aliyopropagate Nyerere imewaweka kando viongozi wa makabila ya kaskazini. Mfano Kina Japhet Kirilo na Marealle ambao walikwenda UNO kutafuta haki ya watanzania. Mangi Meli aliwapinga Wajerumani hadi kujinyonga. Akina Aikaeli Mbowe nasikia walimchangia nauli wakati wa kutafuta uhuru lakini hakuwathamini?.

Akina Guninita na Ditopile wakaendelea kuwaona wabara wana tonotongo, wsio wastaarabu na wasiofaa kupewa uongozi Tz.

Endelea.
Sio Mangi Meli ni Mangi Sina, Mangi Meli alinyongwa hadharani na wajerumani. Aliyejinyonga ni Sina.
 
Kwani alie katwa ni luwasa tu?
Kwangu mm ingekuwa kitu cha ajaabu kama luwasa asinge katwa kwa aina yeyote ile iwe halali au haram iwe kwa misingi ya kanuni au sheria au kukiukwa kwa kanuni au sheria.
Ilikuwa lazima akatwe.
Hatuwezi kuwa na chama kitakaho tishwa na mwanachama kama alivyo kuwa luwasa na vibaraka wake.
Nyie munaona ubaya wa vikao na maamuzi yaliomkata luwasa tu.
Hamuoni ubaya wa kali na vitisho alivyo vitoa luwasa na vibaraka wake dhida ya vikao vya maamuzi vya chana na chama kwa ujumla.
Aliwezaje kutamka neno SIJAONA MTU WA KINIKATA.
JE sasa ameona?
 
Narudia kukusoma mkuu Onesmo Kyauke lakini kitendo cha kuja na jina lako halisi (verified user) inaongeza sana uzito wa ulichokiandika.
Kuna watu wakiongozwa na mwenezi wa ccm wamekuwa wakieneza siasa chafu kwa kulinda masilahi yao ambayo ni madogo sana (narrow) huku wasijue yataathiri vipi maslahi mapana ya taifa.
Hebu angalia huu uzi ambao nao sikuwahi kumsikia mwana ccm yeyote akikanusha haya maneno, nayo yamesemwa na huyo huyo aliyepost kwenye mtandao kuwa rais hawezi toka Kaskazini!
[h=1]Ridhiwani achafua hali ya hewa Times FM[/h]
 
Dr. Kyauke, umeongea vizuri sana.

LAKINI, from long experience and public checkability, people have come to realize kuwa Lowasa si msafi. Simple, anawea kutueleza utajiri alio nao aliupataje wakati mshahara wa mfanyakazi wa serikali/waziri mkuu unafahamika? Hilo tu asipowaeleza kutupa jibu la kweli, hatufai. Ripoti ya Mwakyembe ilionyesha kuwa Lowasa has a case to answer!

Mwisho, watu hawabweki, binadamu wanaongea:"Tumebaki tunabweka kama mazuzu kwamba fulani fisadi bila hata kusema hasa ufisadi wake ni nini". Dr. hapo kwa red umekosea kama msomi
 
Back
Top Bottom