Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, Zanzibar zikiwa zimeanza, Juma Ali Juma mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemkatia rufaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Abdulrazak Khatib Ramadhan mgombea wa Chama cha Wananchi CUF.
Hatua hiyo inatajwa kama mwendelezo wa mbinu za kuhakikisha mgombea wa CCM anapita bila kupigwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo ambaye anatoka CUF.
Juma amekata rufaa hiyo akipinga uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Wilaya ya Magharibi ambaye alilitupa pingamizi lake hapo awali dhidi ya Ramadhan.
Katika pingamizi hilo, mgombea wa CCM anadai kwamba mpinzani wake kutoka CUF hakupitishwa na vikao halali vya chama cha CUF hivyo hafai kushiriki katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, Fatma Gharib Haji msimamizi wa uchaguzi huo, amenukuliwa akisema, “mgombea wa CCM aliwasilisha pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF ambayo yalitupwa, baada ya kuonekana hayakuwa na mashiko. Hatimaye wagombea wote wakapewa fomu za kuwapitisha.”
Fatma amesema utaratibu kuhusu rufaa hiyo unaihusu Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ambayo ndiyo itakayosikiliza katika muda utakaopangwa.
Awali mgombea wa CUF aliweka pingamizi kuwa mgombea wa CCM akidai kuwa katika kiapo chake hakutaja mali zake. Pingamizi hilo pia lilitupwa na NEC kwa madai kuwa halina mashiko.

ukijua kusoma hutauliza hilo swaliMBONA KISHWA CHA HABARI NA HABARI ZENYEWE HAZILINGANI
Tegemeo kubwa la ccm ni vyombo vya dola , ni heri hiki chama kiwe sehemu ya jeshi , bila hivyo hawa ni wepesi kuliko karatasi la mgololo .ccm waoga wa kura za halali
Kubali tu, lugha imekupita. Uwakilishaji wa mada unaendana vizuri na maudhui ya kichwa cha habari!Najua kusoma vizuri ndugu, ila wewe hujui kutumia maneno kama yapaswavyo. You need proper education and a training in writting skills
Umeona uandike na kiingilishi kabisa tujue na wewe wamoNajua kusoma vizuri ndugu, ila wewe hujui kutumia maneno kama yapaswavyo. You need proper education and a training in writting skills
Ebu rudia tena kwa kimombo maneno yoteNajua kusoma vizuri ndugu, ila wewe hujui kutumia maneno kama yapaswavyo. You need proper education and a training in writting skills
Kabisa mdogo wangu, na utanisamehe kama kuna maudhi. Hao wagombea kila mmoja anajaribu kutumia mbino ya kuweza kupunguza makali ya mwenzie. Na hiyo ni part of playing politics. Tuombe mungu wananchi wapate mbunge mwenye uwezo wakuwaletea maendeleo. Tena tuombe uchaguzi usituletea matatizo na wasimamizi watende haki.Umeona uandike na kiingilishi kabisa tujue na wewe wamo