1) Kwanza lazima watu wafahamu kwamba Maregesi, si mtu wa kuaminika. Ni mtu wa kukurupuka ndio maana aliamua kujitangaza kuwa anamuunga mkono Sumaye na Sumaye ndiye atakua Rais. Sumaye kwa udhaifu wake, alishindwa kumdhibiti na habari zinasema aliendelea kufanya mambo ya aibu na ambayo kwa kiasi kikubwa pamoja na matatizo ya Sumaye, MAregesi alichangia kutia chumvi katika kidonda. kwa hiyo suala la kua ni mchafu halina ubishi.
2) Pili hapa kumeibuka mjadala wa mtandao kuanza kazi ya kuandaa timu yao kuelekea chaguzi zijazo, na kutawala bila kubanwa.. hilo nalo halina ubishi. Hii ni siasa, hakuna mtu atakayeacha kutumia silaha alizonazo eti kuogopa kelele zenu kuwa oooh, taifa litagawanyika, oooh, sijui CCM itamegeka, hayo yote wanayajua na jinsi ya kuyakabili wamekwishajiandaa pia.
3)Ama kuhusu ni jinsi gani wataweza kutawala wajumbe wa vikao vya Kamati Kuu, hilo halina ubishi kwani wajumbe wengi ni wale walioteuliwa na JK kuunda sekretarieti ya CCM akiwamo Rostam Aziz na EL ambao hukaa pamoja katika vikao hivyo.
4) Kataraiya naye pamoja na kuwa alikua na misimamo yake, hoja yake inabebwa na maana nyingi, ikiwamo mapambano ya kisiasa mkoani Mwanza na zaidi kanda nzima ya ziwa. Kwa walio Mwanza wanajua maana yake nini.
5) Taarifa zote za magazeti ya jana ambazo zimekanushwa leo na CCM ziinaonyesha kutoka katika chanzo kimoja, na sina shaka chanzo hicho ni hao hao akina EL ambao wanapima upepo kuona umma utapokeaje, na hivyo kuwaandaa kisaikolojia kabla ya kufanya vitu vyao... Sawa na mtu ambaye amekufa, anaambiwa kavumishiwa kifo na kwamba anapumua kwa mashine na baada ya siku ama saa kadhaa unaambiwa AMEKWISHAFARIKI DUNIA... Hapana shaka Maregesi na Kataraia si wa kupona, na kama watapona kikao cha sasa basi wajue hawataendelea na nyadhifa zao baada ya uchaguzi ujao wa chama.
TAARIFA ZINASEMA WAZEE WANAOTA